Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Kuimarisha Bandari za Mtwara, Dar

Status
Not open for further replies.
Bandari ya Bagamoyo ilikuwa mradi mtu kuendeleza kwao. Mengine yote mbwembwe tu. Ziendelezwe za Tanga na Mtwara.
 
Hongera Prof wa ukweli mbarawa chini ya Dr makini Magufuli kwa suspend huo wizi wa Prof wa kichina
 
Kujengwa banadari mpya na ya kisasa kupisha bandari ya dar ambayo haina nafasi ni uharibifu?

Hakika shule mlienda kusomea ujinga.
Nyiee watoto wa pwani(watoto mchele mchele) usiipeleke nchi yetu mnavyotaka, mmeibomoa nchi hii kwa kufanya kila kitu usela, sasa mtaisoma namba nyumbu nyiee
 
Bado sijaona hoja au mantiki ya kusitisha(kama habari hii sio udaku)

Kama issue ni fedha...basi tukusanye kodi kwa ajili ya ujenzi wa Bagamoyo port ambayo itakuwa ya kisasa kuliko zote katika pwani ya EAC na pia tukusanye fedha kwa ajili ya kuboresha hizo za MTWARA NA TANGA.

Kwa nini basi tujisifu tunakusanya kodi ikiwa tunaogopa kuwekeza??

Nakumbuka Mkapa alijenga uwanja wa Taifa mpya pembeni tu ya uwanja wa Uhuru ambao nao uliboreshwa na sikusikia mtu akisema Uwanja huo ukajengwe Mtwara au Moshi.
 
Katika mradi mkubwa uliokuwa wa kushangaza kabisa kwa serikali iliyopita basi ilikuwa huo wa bandari ya bagamoyo,hapakuwa na sababu ya msingi kuweka bandari moja umbali wa takribani km 40 tu ndani ya bahari bagamoyo mpaka Dar,pesa iliyotengwa kwa mradi huo ilikuwa kubwa nyingi sana,pesa hiyo inatosha kabisa kufufua bandari ambazo tayari tunazo Mtwara na Tanga,ukitazama Tanga na Mtwara tayari miundo mbinu ilishakuwepo toka miaka hiyo,inatakiwa sasa kuboreshwa tu,
mpaka sasa najiuliza washauri wa huu mradi walitumia vigezo gani kuweka bandari hiyo bagamoyo?
nadhani wahandisi wa huu mradi wanattakiwa washtakiwe wote kwa ujinga na upuuzi na ushauri wa hovyo kabisa
 
Hongera sana Magufuli kwa kutumbua jipu hili, kazi ya Kikwete ilikuwa kupiga dili na rafiki zake.

Kama mtu una akili timamu huwezi kujenga bandari mpya katikati ya bandari mbili ya (Dar na Tanga) ambazo haziko umbali hata wa maili 200.
 
Binafsi Sidhani Kama Ni Busara KUSITISHA UJENZI BANDARI YA DARESALAAM Imeelemewa Saana , Haina Eneo Sioni Dhambi Kujengwa Bandari Bagamoyo Ni Sehemu ya Tanzania Na Ilikuwepo Kwenye Mipango.
Daresalaam Hakuna Sehemu ya Miundombinu.
KUINGIA Bandarini Leo Inachukua Lorry Hata 6 Hours Foleni Baadae Itakuwaje?
Mizigo Ikiingezeka???
Tunafanya Mambo Kwa Hisia Na Chuki Tu.
Daresalaam, Mtwara Ni Tanzania Bagamoyo Ni Tanzania Pia
Mkuu ukijenga bandari bagamoyo bado kutakuwa na mlundikano wa watu katika mikoa hii miwili ambayo kiuhalisia ishajaa, tuijenge kusini na mikoa ya pembeni ili nchi ipanukee
 
Watu Wa Ajabu Sana Kwani Akitokea Bagamoyo Maana Yake Bagamoyo MIRADI Isifanyike????
Tuangalie Merits Sio Nani Anatoka Wapi?
Mbona Magufuli Ameanzisha Usanifu wa Daraja Kuvuka Ziwa Victoria BUSISI Akija Rais Mwingine Asitishe??
Mbona JK Alianzisha MIRADI UDOM,MALAGARASI, KIGAMBONI, KILOMBERO Mingi Tu Huko Ni Kwao.
Wanaotizama Kwa Mtazamo Huo Ni WAKABILA TU.
Fedha Hizi Ni Grant Zingejengwa Reli Na Highways Kuelekea Maziwa Makuu Bagamoyo Ni Pori Na Eneo Kubwa DAR Itakuwaje???
Mtaboresha Bandari Msongamano Wa Malori KUINGIA Na Kutoka Port.
Fanyeni Muende Leo Muone Foleni Inaanzia Uwanja wa TAIFA KUINGIA.
Kutoa Unapakia Kutoka Saa 4 Na Zaidi Bagamoyo Tulikuwa Na Option ya Kudesign Tutakavyo.
Nchi Hii Wivu, Cheap Politics Na Uswahili.
Fedha Sio Zetu Wataondoka Wapeleke Kwingine.
Kenya, Uganda Na RWANDA 4 Billion Za Standard Gauge Na 6 Billion Za LAPPSET Wanahangaika Miaka 6 Sasa Nchi 3.
Sisi Tumebahatika SIASA ZA FITNA NA UKABILA Kuliko Mantiki Tunaharibu.
Tutajuta Nipo.
Bagamoyo no ni apaapa dar tu kwanini hakupeleka mkuranga ckunabahari napo, barabara alizojenga zinatosha bana
 
Hapo wawekezaji walioingia mikataba watakula fedha ya bure kama hii habari ni ya ukweli.
Hakuna namna, heri wale hizo chache hata kama ni bure kuliko riba ya mkopo wa miaka nenda rudi kwa mradi usio na tija. Hiyo ndiyo gharama za kuwa na marais wa pwani pwani. Sitashangaa kesho kuona tena mtu anatoka msoga kwenda Magogoni 'kumshauri' rais
 
Ukiangalia yote haya :wizi bandarini,hii bandari ya Bwagamoyo,kubadilisha mfumo wa form four results utashindwa kuelewa tatizo lilikuwa ni IQ ya jamaa ama tamaa? Ukisema tamaa jee hili la form ni tamaa? watu kujenga hovyo hovyo ni tamaa? Nafikiri kakichwa kajamaa........
Nimekuelewa sana japo nina mashaka kama wengine watakuelewa. Maana yangu kukuelewa ni kwamba umenipa point muhimu sana pa kuanzia kufikiri badala ya kulaumu au kusifia!

Kinachonifurahisha zaidi ni kwamba hii ni ahadi ambayo EL aliitoa mjini Tanga wakati wa kampeini zake. Kitendo cha JPM kutolisema hili lakini akalitekeleza kama lilivyo inanifanya kuanzia leo nianze kumfuatilia Dr. Magufuli ili mwishowe niwe miongoni mwa watru wanaoweza kumwamini.
Kwa hatua kama hii ya kuvunja mkataba ambao ulishasainiwa kimitego ni kitendo cha kizalendo na ujasiri uliopitiliza!
Tukichanga karata zetu vizuri na kuifanya Dar es Salaam kufanya kazi at its fully capacity basi tunaweza ifanya Tanga kama centre of export huku Dar ikifanya zaidi imports pamoja na Mtwara.
Kuna hasara hapa tutaingia kwa kusitisha mkataba uliokwisha anza utekelezwaji lakini hii ni sawa na tone katika bahari kulinganisha na hasara halisi ya ukamilishwaji wa huu mradi.
 
Last edited:
Hakuna namna, heri wale hizo chache hata kama ni bure kuliko riba ya mkopo wa miaka nenda rudi kwa mradi usio na tija. Hiyo ndiyo gharama za kuwa na marais wa pwani pwani. Sitashangaa kesho kuona tena mtu anatoka msoga kwenda Magogoni 'kumshauri' rais

Bandari ya Bagamoyo haikuwa na mkopo. Ni wawekezaji wanawekeza na wanakula faida au hasara kutokana na mradi uliopo. Sema ukiusitisha ndiyo umeamua kuwapa faida ukipenda usipende.
 
Itajengwa railway kutoka dar hadi chalinze. Chalinze kutajengwa dry port kubwa ambayo itapokea mizigo yote ya upcountry na nchi za maziwa makuu etc hivyo foleni ya malori dar itapungua as mizigo itachukuliwa na trains from Dar port to dry ports na mingine inaenda direct hadi isaka port
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom