Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Kuimarisha Bandari za Mtwara, Dar

Status
Not open for further replies.
Binafsi Sidhani Kama Ni Busara KUSITISHA UJENZI BANDARI YA DARESALAAM Imeelemewa Saana , Haina Eneo Sioni Dhambi Kujengwa Bandari Bagamoyo Ni Sehemu ya Tanzania Na Ilikuwepo Kwenye Mipango.
Daresalaam Hakuna Sehemu ya Miundombinu.
KUINGIA Bandarini Leo Inachukua Lorry Hata 6 Hours Foleni Baadae Itakuwaje?
Mizigo Ikiingezeka???
Tunafanya Mambo Kwa Hisia Na Chuki Tu.
Daresalaam, Mtwara Ni Tanzania Bagamoyo Ni Tanzania Pia
Hoja iliyopo hapo eti ni kwa sababu JK katokea bagamoyo....
 
Tatizo la Kikwete uwa hafikirii kitu, yeye hujifanyia jambo bila kuangalia ya mbeleni. Kulikuwa na umihimu gani kujenga bandari ya Bagamoyo?
 
Kuna kauli moja aliitoa #lowasa wakati yupo Tanga wakati wa campaign kwamba hamna haja ya kujenga bandari Bagamoyo ili hali hizi ttulizonazo bado hazijaboreshwa hyo kauli waliichukia sana wakwere na wazalamu wa Bagamoyo mpaka wakaamua kumrudisha #Kawambwa bungeni.
 
Kwanini isiwe tanga au mtwara iwe bagamoyo kilomita chache kutoka dar

Kwa sababu Bagamoyo ndio karibu zaidi na kitovu cha biashara cha Afrika Mashariki, Dar Es Salaam.

Na hizo nyingine zote si vibaya kuwepo zenye ubora.
 
Bomoa tu tutajenga kesho. Kajituliza kwake kasuku, hataki maneno, hataki matata anachopata kinamtosha.
 
Watu Wa Ajabu Sana Kwani Akitokea Bagamoyo Maana Yake Bagamoyo MIRADI Isifanyike????
Tuangalie Merits Sio Nani Anatoka Wapi?
Mbona Magufuli Ameanzisha Usanifu wa Daraja Kuvuka Ziwa Victoria BUSISI Akija Rais Mwingine Asitishe??
Mbona JK Alianzisha MIRADI UDOM,MALAGARASI, KIGAMBONI, KILOMBERO Mingi Tu Huko Ni Kwao.
Wanaotizama Kwa Mtazamo Huo Ni WAKABILA TU.
Fedha Hizi Ni Grant Zingejengwa Reli Na Highways Kuelekea Maziwa Makuu Bagamoyo Ni Pori Na Eneo Kubwa DAR Itakuwaje???
Mtaboresha Bandari Msongamano Wa Malori KUINGIA Na Kutoka Port.
Fanyeni Muende Leo Muone Foleni Inaanzia Uwanja wa TAIFA KUINGIA.
Kutoa Unapakia Kutoka Saa 4 Na Zaidi Bagamoyo Tulikuwa Na Option ya Kudesign Tutakavyo.
Nchi Hii Wivu, Cheap Politics Na Uswahili.
Fedha Sio Zetu Wataondoka Wapeleke Kwingine.
Kenya, Uganda Na RWANDA 4 Billion Za Standard Gauge Na 6 Billion Za LAPPSET Wanahangaika Miaka 6 Sasa Nchi 3.
Sisi Tumebahatika SIASA ZA FITNA NA UKABILA Kuliko Mantiki Tunaharibu.
Tutajuta Nipo.
 
dah! sasa uku msoga mananasi tutayasafirisha vipi sasa?? mbona mna vikorosho nyie watu??
 
Khaaa!!!huyu mtani wangu nomaaaa siku nikisikia kafanya anasherehe msoga lazima niende nikachezee mdundiko na vanga huku nikimpa vijembe vyake.hakika hiyo bandari haina tija kwa taifa ukizingatia tuna bandari tatu.big up J P Magufuli
 
mzee wa msoga alikuwa anataka kuujenga mji wake wa bagamoyo sasa mambo yamekwamaa, kweli Magufuli hakuwa chaguo lako
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom