TAMISEMI mbona mnachelewa kufidia watu wa bonde la mto Msimbazi?

ras jeff kapita

JF-Expert Member
Jan 4, 2015
19,728
28,284
Kwenu tamisemi. Serekali imeshaweka nia na kutenga fungu mahususi kwa ajili ya fidia ya wakaazi wa bonde la mto msimbazi.

Ni wazi kwamba wakaazi wengi wasiokuwa na hati (squatters) wamefidiwa flat rate shs mil 4. Pamoja na fidia ya majengo.

Pale kwenye bonde kuna hati nane(8)ambazo serekali ilitoa yenyewe.Tafadhali kwa wenye hati wafidieni kwa mujibu wa sheria ya ardhi msiwadhulumu. Mama Samia ni mtu wa haki hawezi kubali wananchi wake wadhulumiwe.

Waiteni wenye hati sikiliza malalamiko yao. Walipeni fidia stahiki kwa mujibu wa sheria.

Ushauri. Zoezi la kulipa fidia na kusikiliza malalamiko lisichukue muda mrefu.

Kufanya hivyo ni kukaribisha vibaka,vishoka na wahuni.

Pia, soma: Serikali yasema Wananchi 2,102 wanaanza kulipwa fidia ya kuhamishwa Bonde la Mto Msimbazi
 
Back
Top Bottom