Katavi: Wananchi wacheleweshwa kulipwa fidia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Baadhi ya wakazi wa Kata ya Shanwe, Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameiomba Serikali kuwalipa fidia yao ambayo imetokana na kupisha mradi wa maji wa miji 28 unaotekelezwa katika Manispaa ya Mpanda.

Wamesema kila wanapouliza kuhusu kulipwa fidia yao wanapewa majibu yasiyowafurahisha ambapo Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Katavi, Chidiel Mlutu amesema tayari ofisi yake imekwisha kamilisha uthamini wa maeneo.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko amesema ahadi yao iko palepale na Serikali kupitia Wizara husika itawalipa.

Mrindoki amezindua Kliniki ya Kusikikuza na kutatua kero mbalimbali ambapo ameagiza viongozi wa mkoa huo kuwafikia Wananchi popote walipo ili kusikiliza na kutatua kero.
 
Back
Top Bottom