Serikali yapeleka huduma ya mabasi ya Mwendokasi Kibaha

Wamefanya jambo la busara sana na hii yote ni kupunguza msongamano stand ya Mbezi kama ilivyokuwa zamani Kimara.. Kwasasa kimara pameboreshwa mno hakuna tena kugombea magari..Mwanzoni haikuwezekana kabisa
Miundombinu ya Mbezi Kibaha inaruhusu haya magari kufika bila tabu.. Sasa ni vema kukawa na route za moja kwa moja Kibaha Kariakoo na Kibaha Ferry...!

Sijui huku ndio kuupiga mwingi? Kwa BRT lakini!
Jana nilipita palekituo cha sheli Maili moja,nilimkuta dada wa mwendo kasi akiita abiria wanaotaka kwenda Kivukoni moja kwa moja. Kwa hiyo yapo ya kivukoni ila sina uhakika kwa yale ya Gerezani direct
 
Jana nilipita palekituo cha sheli Maili moja,nilimkuta dada wa mwendo kasi akiita abiria wanaotaka kwenda Kivukoni moja kwa moja. Kwa hiyo yapo ya kivukoni ila sina uhakika kwa yale ya Gerezani direct
Safi kabisa.. Nikitoka Msata kituo cha kwa kwanza maili moja
 
wasisahau ruti ya kuingia Hospitali ya Mloganzila.
Wananchi ni wengi sana wanatoka maeneo mbalimbali kufuata huduma.
 
Ule ufalme wa coaster za Mlandizi unafikia tamati!
Na jinsi ambavyo huwa wanajidai wakiwa wanapakia abiria mbezi, sisi tunaoshukia karibu huwa wanatukataza kukalia siti.
Nimekwazana nao sana kuhusu hili, utakuta mpiga debe kawekwa mlangoni anamuuliza kila abiria anayepanda kituo anachoshukia, ukisema unashuka maili moja au Loliondo, hawakuruhusu kupanda.

Hiki kiburi kitakoma sasa kwa ujio mwendokasi
 
Back
Top Bottom