The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 5,462
- 17,278
Juzi hapa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii alikutana na wafanyakazi wa wizara hiyo katika kujadili masuala ya utalii na changamoto zake alikiri kuwa zaidi ya 80% ya watalii wanaotembelea Tanzania huwa hawarudu tena, wakishakuja mara moja wengi wao huwa hawarudi tena.
Maana yake ni kuwa sisi Tanzania kila mwaka tunategemea watalii wapya, hatuwezi kuwatuliza(keep) ama kuwahakikishia watalii wa zamani kurudi tena Tanzania kufurahia vivutio vyetu vya utalii.
Retention yetu ya watalii ni chini ya 20%. Maana yake ukuaji wa utalii wetu bado una changamoto kubwa sana.
Nikitoa my personal experience, nilitembelea Kisiwa cha Saa Nane, Mwanza, tukakutana na tour guide wa kike, wote tuliofika pale siku hiyo hatuwezi kutamani kurudi tena, mimi na wenzangu siku hiyo tulikuwa disappointed, siwezi kutamani hata kwa bunduki kutembelea tena hiyo hifadhi.
Nimewahi kwenda Serengeti National park mara 2, kwa pale niko tayari kurudi maana mategemeo yangu yalikamilika kwa zaidi ya 80%.
Je, unadhani ni kwanini watalii wa nje hawarudi tena baada ya kutembelea Tanzania.
=============
ARUSHA
Wamiliki wa makampuni ya watalii, wadau ya sekta ya utalii nchini Tanzania ikiwemo wahifadhi wastaafu wameelezea sababu tano zinazowafanya watalii waliotembelea nchini wasirudi kwa mara ya pili.
Sekta ya utalii inachangia asilimia 17.5 ya pato la Taifa pia asilimia 25 ya mapato ya fedha zote za kigeni nchini ambapo kwa sasa inatembelewa na watalii milioni 1.2. Serikali inalenga mpaka 2025, Tanzania inatakiwa kupokea angalau watalii milioni tano na kukuza mapato ya fedha za kigeni kutokana na utalii mpaka dola bilioni 6 kutoka dola bilioni 2.5 kwa mwaka.
Wakiongea na gazeti la Citizen, washika dau wameainisha sababu kama gharama kubwa ambazo watalii wanaingia wakitembelea Tanzania, huduma kwa wateja isiyoridhisha kwenye mahoteli na watoa huduma wengine.
Kulingana na wao, miundombinu mibovu, makampuni ya watalii yanayoshindwa kutimiza ahadi zao walizowapa wateja na wafanyakazi kukosa uadilifu ikiwemo kuwalangua watalii. Akiongea na Citizen, mhifadhi mstaafu, Erastus Lufungilo ambae kwa sasa ni mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Burudika amesema watalii walilazimika kutumia fedha zaidi kutokana na kukosekana kwa ndege za moja kwa moja kutoka kwenye nchi zao ikiwemo Ulaya na Marekani kuja Tanzania. "Utalii ni gharama, hii ni kwasababu kutembelea Tanzania kwasasa ni gharama kuliko kutembelea Kenya au Afrika kusini" Alieleza.
Kulingana na yeye, makampuni mengi ya utalii yana mapungufu katika kuendesha biashara na kuongoza watalii kunakosababishwa na upungufu wa wafanyakazi wataalam na kusababisha matatizo.
"Baadhi ya waongoza watalii wanachukua hela kutoka kwa watalii lakini chaajabu huwezi kuwakuta uwanja wa ndege kuwapokea watalii. Hata wakijitokeza kuwapokea ambao wanalipwa hela nyingi, hawatoi huduma bora" Alisema Lufungilo
Kwa upande wake, mwenyekiti wa chama cha waongoza watalii(TTGA) amesema wingi wa kodi zinazotozwa kwa makampuni ya watalii na waongoza watalii imesababisha watalii kutomudu gharama kwa watalii wengi ambao wanashindwa kuitembelea tena Tanzania.
"Kuna kodi nyingi sana na kila siku kodi mpya zinatangazwa na kuwalazimu wamiliki kupandisha gharama ili kupata faida. Alisema ndugu Mollel. Alihoji kwanini baadhi ya mashrika ya ndege kuchaji dola 500 zaidi kwa tiketi safari kutoka Ulaya kuja Tanzania ikilinganishwa na viwanja vingine vya ndege kwenye nchi za jirani.
Akifungua mkutano wa mwaka kwa wahariri na waandishi waandamizi kwenye sekta ya utalii, katibu mkuu wizara ya Utalii na maliasili, Aloyce Nzuki amewataka wanahabari wafikiri kwa makini kwanini asilimia 20 pekee ya watalii wanaitembelea tena Tanzania.
Dr. Nzuki amevitaka vyombo vya habari nchini kutoa taswira nzuri ya nchi kabla na baada ya watalii kutembelea Tanzania