Tanzania yanadi Vivutio vyake kwa watalii na wawekezaji mahiri duniani

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amewahakikishia kundi maalum la wawekezaji na watalii mahiri duniani zaidi ya 150 kutoka nchini Marekani na nchi nyingine duniani lililowasili nchini Novemba 4,2023 kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana nao kikamilifu katika jitihada za kukuza uchumi wa Tanzania kupitia sekta ya utalii

Akizungumza katika hafla iliyofanyika leo Novemba 12,2023 katika ukumbi wa Hoteli ya Mout Meru jijini Arusha, Mhe.Kairuki amesema moja ya lengo kuu la hafla hiyo ni kuitangaza Tanzania kama kivutio cha utalii na pia soko la utalii la kuvutia na la uhakika kwa wageni wa Marekani.

“Serikali ya Tanzania inahimiza uwekezaji katika miundombinu na maendeleo ya masoko ya utalii na hii ni fursa nzuri kwa makampuni ya Marekani kuongeza mauzo na kupata maeneo ya kimkakati ya kukuza uwekezaji barani Afrika” Mhe. Kairuki amesisitiza.

Aidha Mhe. Kairuki ametumia fursa hiyo kuyakaribisha makampuni ya Marekani kushiriki katika kukuza sekta ya utalii ya Tanzania.

Amefafanua kuwa Sekta ya utalii nchini Tanzania huzalisha zaidi ya dola Bilioni 2.6 katika pato la Taifa pamoja na kutoa ajira zaidi milioni 1.5 kwa wananchi wake.

Kuhusu ongezeko la Idadi ya watalii wanaotembelea nchini Tanzania Mhe. Kairuki amesema mwaka jana ulikuwa mwaka wa rekodi kwa utalii nchini Tanzania, ambapo zaidi ya wageni milioni moja walikuja kufurahia maeneo ya ikolojia ambapo jumla watalii 100,600 walikuwa ni kutoka nchini Marekani.

Amesema ongezeko la idadi ya watalii linatokana na kuongezeka kwa utangazaji wa Utalii kupitia Filamu ya “Tanzania the Royal Tour” pamoja na matangazo ya television ya CNN ambapo vivutio vya utalii vinaendelea kutangazwa duniani kote.

Katika hatua nyingine, Mhe. Kairuki amesema Tanzania itakaribisha kikundi cha wachezaji 120 maarufu wa tenisi na wapenda tenisi kutoka Marekani ambao watakuwa kwenye McEnroe Luxury Safari Tour, na Mashindano ya Tenisi yatakayofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mwezi Desemba,2023.
WhatsApp Image 2023-11-12 at 21.11.51 (1).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-12 at 21.11.53.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-12 at 21.11.51.jpeg
 
Tuna zaidi ya vivutio vya utalii shida ni kuvitangaza, Rwanda haina utalii wa maana hata kidogo lakini vile vichache walivyo navyo wanajua namna ya kuvitangaza vizuri, hadi leo Tanzania imeshindwa kuweka "visit Tanzania" kwenye timu hata moja ulaya alafu Rwanda wameweza kwamba wao wana pesa Sana kushinda Tanzania 🤔🤔

timu kama Manchester united na Real Madrid ni sehemu nzuri Sana za kuongeza watalii Tanzania kwa sababu ndio timu zinazo uza zaidi jezi duniani,
au visit Tanzania ingekua inaonekana kwenye viwanja vya ligi ya Saudi Arabia ingekua bado ni bora zaidi, lakini wenye mamlaka walivyo kua na akili fupi walitaka kwenda kuweka "Visit Tanzania" kwenye uwanja wa mazoezi kwenye kitimu kimoja cha uholanzi huko, hovyo kabisa
 
Upo sahihi, tuwekeze kwenye kuvitangaza
 
Back
Top Bottom