Serikali yakanusha taarifa za kuanza kutoa ajira

SniperBoi

JF-Expert Member
Feb 3, 2016
1,103
1,125
Presentation1.jpg
Presentation155.jpg

YAH: KUKANUSHA HABARI ILIYOSAMBAA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII IKIMNUKUU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA) MHESHIMIWA ANGELLAH J. KAIRUKI (MB), KUWA SERIKALI ITAANZA KUTOA AJIRA, KUPANDISHA VYEO NA KULIPA STAHIKI MBALIMBALI ZA WATUMISHI WA UMMA MWEZI FEBRUARI, 2017.

1. Ipo taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikimnukuu Waziri wa Nchi -Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb), kuwa Serikali itaanza kutoa ajira, kupandisha Vyeo na kulipa Stahiki mbalimbali za Watumishi wa Umma mwezi Februari, 2017. Chanzo cha habari hiyo ni mtandao wa Jamii Forum kupitia mjadala ulioanzishwa na nkanga chief (JF-Expert Member) na baadaye kusambazwa katika mitandao mingine.

2. Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inapenda kuwafahamisha Watumishi wa Umma na Umma kwa ujumla kuwa, taarifa hiyo haina ukweli wowote na ina lengo la kuupotosha Umma. Hivyo watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla wanaombwa kuipuuza taarifa hiyo na kuendelea na majukumu yao kama kawaida.

3. Serikali inasisitiza kuwa, suala la Ajira mpya na upandishaji Vyeo litafanyika kwa kuzingatia Bajeti ya Serikali ya Mwaka wa Fedha

2016/17. Malipo ya stahili za watumishi wa umma yatafanywa na Serikali kwa kuzingatia, Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo.

4. Ikumbukwe, Serikali ina utaratibu maalum wa kutoa taarifa kwa Umma, hivyo Serikali itatoa taarifa rasmi kwa Umma kupitia mamlaka husika.

5. Serikali kupitia taarifa hii inawaasa wananchi kuacha tabia ya kusambaza habari za uongo au zisizothibitishwa dhidi yake. Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kuzusha na kusambaza habari za upotoshaji kuhusu shughuli za Serikali.

Imetolewa na:

Florence Temba

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora)

24 Oktoba, 2016

=======

Habari hii imetumika kwenye Kipindi cha JamiiLeo kinachorushwa kila siku jioni katika Channel ya JamiiForums kwenye mtandao wa YouTube.

Kuona kipindi hicho angalia video ifuatayo, acha maoni yako na kisha Subscribe kwenye Channel ya JamiiForums.

Hii taarifa ya kukanusha imezidi kuchochea moto wa kilio cha Ajira kuliko kuuzima.
Ni kweli taarifa imekanusha, lakini hapo hapo ameacha pengo la taarifa.

Swali kuu kuliko yote hapa ni "LINI SERIKALI ITATOA AJIRA MPYA, KUPANDISHA VYEO, KULIPA MALIMBIKIZO NA KURUHUSU UHAMISHO?"

Pasipo kupata majibu ya swali hilo, tutaendelea kuona uzushi mpya wa taarifa mitandaoni kila siku.
 
Hapa naona kuna point JF na viongoz wote kina Max Melo na wana JF wote inabidi kushauriana ili kujua jinsi ya kuleta heshima kwenye forum yetu.
JF imeanza zamani sana ikiwa Jambo forum back 2006.

Viongozi wengi waliopo madarakani wanaijua sana Jf na wengi wao ni member wa hapa ndani na wanaitembelea sana na wengine lazima wana ID zao verified ama kama sisi.

Sasa ushauri wangu kwa members wote tusitunge habari za uongo tunaishushia hadhi forum yetu wakati ina mambo mengi sana ya maana . Kuna thread nyingi sana zinajenga na zinaelimisha.
Watu wengine wamekuwa addicted kabisa kwenye majukwaa tofauti mpaka wale wadau wa jukwaa la kule chini mwisho japo mimi sipo kule wengi hawalijui.
Tujiheshimu wadau.

Ushauri mwingine kwa viongozi wa JF inatakiwa mtu akileta thread inayohusu tamko ama taarifa kama hii, muwasiliane na wahusika ili kujua kama je hii taarifa ni ya kweli?
Nawapongeza sana Mods waliokuwa online siku ile ilipokuja barua ya uongo ya kujiuzulu ya Mrisho Gambo kwa sababu kila baada ya dakika ilikuwa inaletwa na mods wanaidungua muda huo huo . Hapa niliwakubali sana.
Nadhani ushauri wangu sio mgumu kutekelezwa kwa sababu watu wanatofautiana kuna watu na viatu.
Gonga likes kama umekubaliana na mimi.
Ni mtizamo wa Saint Ivuga.
Viva JF
 
mmekanusha tumekubali mseme ni lini sasa mtatoa hzo mambo
Presentation1.jpg
Presentation155.jpg

YAH: KUKANUSHA HABARI ILIYOSAMBAA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII IKIMNUKUU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA) MHESHIMIWA ANGELLAH J. KAIRUKI (MB), KUWA SERIKALI ITAANZA KUTOA AJIRA, KUPANDISHA VYEO NA KULIPA STAHIKI MBALIMBALI ZA WATUMISHI WA UMMA MWEZI FEBRUARI, 2017.

1. Ipo taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikimnukuu Waziri wa Nchi -Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb), kuwa Serikali itaanza kutoa ajira, kupandisha Vyeo na kulipa Stahiki mbalimbali za Watumishi wa Umma mwezi Februari, 2017. Chanzo cha habari hiyo ni mtandao wa Jamii Forum kupitia mjadala ulioanzishwa na nkanga chief (JF-Expert Member) na baadaye kusambazwa katika mitandao mingine.

2. Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inapenda kuwafahamisha Watumishi wa Umma na Umma kwa ujumla kuwa, taarifa hiyo haina ukweli wowote na ina lengo la kuupotosha Umma. Hivyo watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla wanaombwa kuipuuza taarifa hiyo na kuendelea na majukumu yao kama kawaida.

3. Serikali inasisitiza kuwa, suala la Ajira mpya na upandishaji Vyeo litafanyika kwa kuzingatia Bajeti ya Serikali ya Mwaka wa Fedha

2016/17. Malipo ya stahili za watumishi wa umma yatafanywa na Serikali kwa kuzingatia, Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo.

4. Ikumbukwe, Serikali ina utaratibu maalum wa kutoa taarifa kwa Umma, hivyo Serikali itatoa taarifa rasmi kwa Umma kupitia mamlaka husika.

5. Serikali kupitia taarifa hii inawaasa wananchi kuacha tabia ya kusambaza habari za uongo au zisizothibitishwa dhidi yake. Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kuzusha na kusambaza habari za upotoshaji kuhusu shughuli za Serikali.

Imetolewa na:

Florence Temba

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora)

24 Oktoba, 2016
 
Kwa maana bajeti ya mwaka fedha 2016/2017 haina ajira!! Poleni sana wahanga wa ajira, na kwa serikali hii yenye roho mbaya kwa watu wake nawashauri muanzishe vikundi vya ujasiriamali mjichangishe, kila mmoja aje na idea ya nini cha kufanya ili kujikwamua na hili janga kubwa kama la tsunami, hii serikali imeelekeza nguvu kwa majeshi ya ulinzi ili kujilinda kwa kuwa wamechokwa hivyo wanawekeza kwenye mabomu, na kusahau kada zingine make hata mishahara imekua shida, rejea taarifa ya habari wauguzi muheza hawajapata mshahara miezi miwili sasa, poleni sana tena Sana, tuliyataka wenyewe na bado.
 
Back
Top Bottom