Waziri mkanushaji ungetuambia ni kitu gani kilisababisha au kukwaza haya kufanyika kwa kipindi cha kuanzia july 2016 hadi sasa. Kusema tu serikali ina sheria na taratibu zake za kutenda hayo ni sawa na kusema serikali ina yaratibu zake za kutokutenda kwa mujibu wa sheria zisizoonekana kwenye katiba iliyopo. Tuambie lilipo tatizo na kwanini limechukua muda mrefu hivi kutafutiwa ufumbuzi. Nakujua waziri umetokea kwenye vyama vya wafanyakazi, ni kwanini basi huusemi ukweli au umesaidia kuwafunga midomo viongozi wa vyama vya wafanyakazi ili wasiitishe hata vikao? Ni sheria ya ajira ya 1979 inayosisitiza mwajiriwa kupata nyongeza ya mshahara wake kila ifikapo july, sheria hii imefutwa lini na bunge gani? Mtaua morali ya wafanyakazi wa nchi hii kwa hakika.