Serikali yakanusha taarifa za kuanza kutoa ajira

Serikali yakanusha taarifa za kuanza kutoa ajira

nkanga chieffffffffff ... dedication song to you iiiiiiis... natafuta kiki by raymond
 
kapigwa ban ndo ni mimi[emoji212] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] just kidding
 
Labda kosa la mleta uzi wa mwanzo ni kutaja muda wa karibu sana......
Inawezekana ajira hakuna mwaka huu wa fedha.....maana mkanushaji hataji lini ajira na vyeo vitapanda.
Mkanushaji alitakiwa kusema lini zitatoka hizo ajira na mambo mengine.
 
Hii taarifa ya kukanusha imezidi kuchochea moto wa kilio cha Ajira kuliko kuuzima.
Ni kweli taarifa imekanusha, lakini hapo hapo ameacha pengo la taarifa.

Swali kuu kuliko yote hapa ni "LINI SERIKALI ITATOA AJIRA MPYA, KUPANDISHA VYEO, KULIPA MALIMBIKIZO NA KURUHUSU UHAMISHO?"

Pasipo kupata majibu ya swali hilo, tutaendelea kuona uzushi mpya wa taarifa mitandaoni kila siku.
"3. Serikali inasisitiza kuwa, suala la Ajira mpya na upandishaji Vyeo litafanyika kwa kuzingatia Bajeti ya Serikali ya Mwaka wa Fedha

2016/17. " wamejibu kihuni sana bila kutaja ni lini
 
Labda kosa la mleta uzi wa mwanzo ni kutaja muda wa karibu sana......
Inawezekana ajira hakuna mwaka huu wa fedha.....maana mkanushaji hataji lini ajira na vyeo vitapanda.
Mkanushaji alitakiwa kusema lini zitatoka hizo ajira na mambo mengine.
Hapa matumizi yamebanwa na mwakan sijui kama watafanya double increment na Dabo kupandisha madaraja ila kwa wahitim wa mwaka juz cjui kama wanakumbuka walichosomea bila practice yyte good morning GAVUMENDI
 
Serikali Yakanusha Taarifa Iliyosambaa Katika Mitandao Ya Kijamii Kuwa Itaanza Kutoa Ajira.

1.Ipo taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikimnukuu Waziri wa Nchi -Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb), kuwa Serikali itaanza kutoa ajira, kupandisha Vyeo na kulipa Stahiki mbalimbali za Watumishi wa Umma mwezi Februari, 2017. Chanzo cha habari hiyo ni mtandao wa Jamii Forum kupitia mjadala ulioanzishwa na nkanga chief (JF-Expert Member) na baadaye kusambazwa katika mitandao mingine.

2.Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inapenda kuwafahamisha Watumishi wa Umma na Umma kwa ujumla kuwa, taarifa hiyo haina ukweli wowote na ina lengo la kuupotosha

Umma. Hivyo watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla wanaombwa kuipuuza taarifa hiyo na kuendelea na majukumu yao kama kawaida.

3.Serikali inasisitiza kuwa, suala la Ajira mpya na upandishaji Vyeo litafanyika kwa kuzingatia Bajeti ya Serikali ya Mwaka wa Fedha 2016/17. Malipo ya stahili za watumishi wa umma yatafanywa na Serikali kwa kuzingatia, Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo.

4. Ikumbukwe, Serikali ina utaratibu maalum wa kutoa taarifa kwa Umma, hivyo Serikali itatoa taarifa rasmi kwa Umma kupitia mamlaka husika.

5. Serikali kupitia taarifa hii inawaasa wananchi kuacha tabia ya kusambaza habari za uongo au zisizothibitishwa dhidi yake. Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kuzusha na kusambaza habari za upotoshaji kuhusu shughuli za Serikali.
 
Lini Ajira mpya zitatoka?............


Nyie kweli ni mwendokasi baada mjibu Ajira lini .......

Mnakuja na polojo kama za kahawa........


Kwahiyo hii taarifa hapo juu ndio majibu ya serikali inavyotakiwa kujibu?.......

Nikisema na huyo aliyetoa taarifa hii ni kila,za nitakuwa nakosea?..........
 
Lini Ajira mpya zitatoka?............


Nyie kweli ni mwendokasi baada mjibu Ajira lini .......

Mnakuja na polojo kama za kahawa........


Kwahiyo hiyo taarifa hapo juu ndio majibu ya serikali inavyotakiwa kujibu.....

Nikisema na huyo aliyetoa taarifa hii ni kila,za nitakuwa nakosea?..........
hawa ni viongozi wa kukanusha sio kutekeleza
 
nkanga chief njoo huku.Walau wewe ulitoa matumaini kuwa hali itakuwa nzuri February 2017,lkn serikali inaonyesha itakuwa mbele zaidi yaani hata 2019.Hatari sana.

Huyu Kairuki sijui anataka nini?Tunamsubiri Jimbo la Same Magharibi 2020 maana kashaanza kupiga jaramba la kuutaka Ubunge,kwa mtindo huu tutamfutilia mbali
 
Namashaka na elimu ya kailuki....naomba ichunguzwe inaweza kuwa alinunua jina
 
Back
Top Bottom