Serikali yakana hukumu ya kuilipa ESCROW dola Mil 185. Dk. Abbasi asema Serikali haidaiwi

Sasa munaona umuhimu wakuwa na umeme wetu wenyewe? Kesi za kijinga kama hizi huwezi kukutana nazo tena. Kweli Umeme wa Rufiji utakuwa mkombozi kwetu ndo maana upande wa wazungu hawakupenda project hiyo.
Hayo yote yalifanyika chini ya serikali ya ccm
 
Unaweza ukasaini kama kugaranti mtu kwamba deni litalipwa lakini sio mdaiwa wa kwanza. Kwasababu mkopaji/mdaiwa wa kwanza yupo(IPTL) hajafa ajilipie deni lake.
Ebu kama hujui unacho ongelea ni vema ukaenda kujiandikisha maana unatoa vibweka kwenye mambo yanayo hitaji kutumia weledi
 
Short and clear
Hukumu kwa Kwa kifupi imesema;-
V. The Government of United Republic of Tanzania shall;-
Pay to climant the sum of USD 185,449,440.04 together with interest thereonat the rate of LIBOR (6-Months) +2% from the 1 September 2018until the date of full and final payment and
VI. Bear its own legal costs and expenses
 
Sasa munaona umuhimu wakuwa na umeme wetu wenyewe? Kesi za kijinga kama hizi huwezi kukutana nazo tena. Kweli Umeme wa Rufiji utakuwa mkombozi kwetu ndo maana upande wa wazungu hawakupenda project hiyo.
Wacha kushona mbeleko kabla mtoto hajazaliwa. Ni mapema mno kusherehekea umeme wa Stiglers Gorge. Changamoto zilizoikumba miradi ya ya Mtera na Kihansi hamna namna Rufiji itazikwepa. Tuombe uzima kuna mtu pale Magogoni hashauriki, analoamini yeye ndiyo hilo hilo
 
Na hizo ndege tatu zitakazokuja November haziji mpaka tzs 426 bilioni zilipwe wa SCB!
Kule Afrika Kusini ndege haiendi tena.
London ndege haiendi tena.

Bado wale jamaa wa Bagamoyo
Bado Symbion mmmmmh
Kweli Mabeberu si mchezo
 
Akizungumzia hukumu hiyo iliyotolewa Oktoba 9, mwaka huu, Dk. Abbasi amesema ameulizwa kuhusu hukumu hiyo, na hivyo amelazimika kutoa ufafanuzi.

“Msingi wa kesi zote mdaiwa siyo serikali wala Tanesco, ni deni la benki dhidi ya IPTL (kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited) walilorithi miaka mingi kutoka kwa wakopeshaji wa Malaysia.

Kwa muktadha huo na kisheria, serikali na Tanesco ziliunganishwa tu kama kanuni za kisheria zinavyomruhusu mdai kuwaunganisha wahusika wengine kwenye kesi ili kupata uhakika kuwa analipwa madai yake," amesema Dk. Abbasi.

“Kwa muktadha huo, natumia fursa hii kuwatoa wasiwasi Watanzania, serikali haidawi, haijawahi kukopa Standard Chartered ya Hong Kong, ila kama Baraza la Usuluhishi lilivyoamua, tutahakikisha tunasimamia utawala wa sheria kwa kuona IPTL wanalipa deni lao,” amesema Dk. Abbasi.

Katika kesi hiyo ya ICSID yenye namba ARB/15/41, benki hiyo ilifungua kesi dhidi ya serikali ikidai kiasi hicho cha fedha kwa kile ilichodai ni kutokana na kukiukwa kwa mkataba wa manunuzi ya umeme uliokuwa umetiwa saini baina yao na pande tatu za mkataba huo.

Benki hiyo ilikuwa ikiwakilishwa na Matthew Weiniger wa QC Linklaters LLP One, Iain Maxwell, Aaron McDonald, Elizabeth Kantor, Harry Ormsby, Gavin Creelman na Herbert Smith wa Freehills LLP, wote kutoka Uingereza.

Hukumu hiyo inaonyesha Serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Adelardus Kilangi, Wakili Mkuu wa Serikali, Dk. Clement Mashamba, Beredy Malegesi wa Crax Law Partners, Richard Karumuna Rweyongeza wa R. K. Rweyongeza & Co. Advocates, Galileo Pozzoli, Mark Handley, Profesa Tullio Treves, Luciana Ricart, Irene Petrelli, Renato Treves na Valerio Salvatori Curtis wa Mallet-Prevost, Colt & Mosle LLP.

Chanzo: Nipashe

Mwanasheria Mkuu wa Serikali leo katika mahojiano maalum na TBC amesisitiza kauli ya jana ya Serikali kupitia kwa
Msemaji Mkuu wa Serikali kuwa Serikali haidaiwi na katika uhusiano wa kibiashara kati ya IPTL na Benki ya SCB Hong Kong.

Serikali kama msimamizi wa utekelezaji itaibana kampuni ya IPTL ambayo bado ipo hapa nchini ikiwa na mitambo na raslimali nyingine, ikamilishe deni wanalodaiwa.


Hukumu kwa Kwa kifupi imesema;-
V. The Government of United Republic of Tanzania shall;-
Pay to climant the sum of USD 185,449,440.04 together with interest thereonat the rate of LIBOR (6-Months) +2% from the 1 September 2018until the date of full and final payment and
VI. Bear its own legal costs and expenses

Pia soma

Maneno meengi,mdaiwa IPTL ambae huduma alimpa serikali atumie,mlipaji ni serikali ultimately!

What a douche!

Abbas yupo kama mwizi mwizi hivi!

Halafu eti ni DK!
 
Serkali hawahusiki hapo ufafanuzi mzuri sana


Yalipe yale mafisadi yaliyojificha nyuma ya IPTL
Changanya na zako wewe bwege,unapokeaje maelezo yasiyo na tija kwa mwanasheria wa serikali bila kwanza kutafuta ukweli wa hoja yake?
Walau ungejiuliza,kama serikali haihusiki na hilo deni,ni kwa nini walipeleka wanasheria wao huko mahakamani?
Na ni kwa nini serikali imetajwa kama mdaiwa kwenye kesi hii???
Ukiwa na majibu sahihi basi unaweza kusema unachosema
 
Sasa munaona umuhimu wakuwa na umeme wetu wenyewe? Kesi za kijinga kama hizi huwezi kukutana nazo tena. Kweli Umeme wa Rufiji utakuwa mkombozi kwetu ndo maana upande wa wazungu hawakupenda project hiyo.

Umeme wako mwenyewe huku tumekopa zaidi ya 6 trillioni? Na inaweza kufika karibu 10 mpaka mradi ukamilike? Tunalipaje?
 
Si kweli, bahati nzuri hukumu tunayo. Imesema kabisa kuwa serikali ya Tanzania kwa kukatisha mkataba.... Go and read!
Mhe. Ndo maana akina Sethi na Ruge wapo katika nondo ili wao walipe. Hukumbuki JK alisema ile hela ilikuwa yao? Acheni kupotosha, kazi ya serikali ni kuhakikisha hiyo hela imelipwa. Tatizo lipo wapi?
 
Mkuu jamaa anacho hitaji ni assurance ya mkono kwenda kinywani
Huyu Dr Hassan Abas ni kama Comical Ali au Mohamed Sared AlSahhaf aliyekuwa Msemaji wa Saddam Hussein wakati wa vita vya ghuba mwaka 2003.

Nchi nzima ilishatekwa mpaka Airport ya Baghdad lakini yeye alikuwa anasema US Marines watakatwa vichwa wote wakitua Iraq na kwamba Saddam bado yuko in control.

Hawa wasemaji tuwahurumie tu, hawaruhusiwi kutumia akili zao. Huyu Dr Abbasi angekuwa na soko kwenye profession yake asingekubali kazi ya kijinga kama hii. Kazi ya kukanusha tu
 
Back
Top Bottom