Serikali yakana hukumu ya kuilipa ESCROW dola Mil 185. Dk. Abbasi asema Serikali haidaiwi

a836a50cd8eefc644d88116df6b26259

MSEMAJI Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi, amesema Serikali haihusiki na hukumu iliyotolewa na Baraza la Kimataifa la Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICSID), ambayo imetaka Benki ya Standard Chartered (Hong Kong) Ltd ilipwe dola za Marekani milioni 185.

Akizungumzia hukumu hiyo iliyotolewa Oktoba 9, mwaka huu, Dk. Abbasi alisema amekuwa akiulizwa kuhusu hukumu hiyo, hivyo analazimika kutoa ufafanuzi

“Msingi wa kesi zote mdaiwa si Serikali wala Tanesco, ni deni la benki dhidi ya IPTL (kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited) walilorithi miaka mingi kutoka wakopeshaji wa Malaysia.

“Kwa muktadha huo na kisheria, Serikali na Tanesco ziliunganishwa tu kama kanuni za kisheria zinavyomruhusu mdai kuwaunganisha wahusika wengine kwenye kesi ili kupata uhakika kuwa analipwa madai yake.

“Kwa muktadha huo, natumia fursa hii kuwatoa wasiwasi Watanzania, Serikali haidawi, haijawahi kukopa Standard Chartered ya Hong Kong, ila kama Baraza la Usuluhishi lilivyoamua, tutahakikisha tunasimamia utawala wa sheria kwa kuona IPTL wanalipa deni lao,” alisema.

Katika kesi hiyo ya ICSID yenye namba ARB/15/41, benki hiyo ilifungua kesi dhidi ya Serikali ikidai kiasi hicho cha fedha kwa kile ilichodai ni kutokana na kukiukwa kwa mkataba wa manunuzi ya umeme uliokuwa umetiwa saini baina yao na pande tatu za mkataba huo.

Benki hiyo ilikuwa ikiwakilishwa na Matthew Weiniger wa QC Linklaters LLP One, Iain Maxwell, Aaron McDonald, Elizabeth Kantor, Harry Ormsby, Gavin Creelman na Herbert Smith wa Freehills LLP, wote kutoka Uingereza.

Hukumu hiyo inaonyesha Serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Adelardus Kilangi, Wakili Mkuu wa Serikali, Dk. Clement Mashamba, Beredy Malegesi wa Crax Law Partners, Richard Karumuna Rweyongeza wa R. K. Rweyongeza & Co. Advocates, Galileo Pozzoli, Mark Handley, Profesa Tullio Treves, Luciana Ricart, Irene Petrelli, Renato Treves na Valerio Salvatori Curtis wa Mallet-Prevost, Colt & Mosle LLP.
Mara ya mwisho kusikia mtu anaunganishwa kwenye kesi mtu huyo aliyeunganishwa alilala ndani. Ilikua ni pale Mbowe na wenzake walipounganishwa kwenye kesi iliyopelekea maandamano na mauaji ya bint Akwilina (RIP), pia akina Rose Sanare na mkwe wa Lowasa walipounganishwa kwenye kesi ya uhujumu uchumi, nao wapo ndani hadi leo.
Hivi huyu Dr. Abbas ni msemaji wa Simba au Serikali? Anaongea vitu bila ya weledi kabisa, yaani uunganishwe kwenye kesi bila kuwa sehemu ya kutuhumiwa au andhani wanaounganishwa kwenye kesi ni huwa ni kama wale ma maid na wapambe wa kwenye harusi kwamba wao ni wapambe tu lakini siyo waoaji?
 
Anajidanganya yeye mwenyewe maana hakuna mwenye jeuri na mahakama za kimataifa
Akizungumzia hukumu hiyo iliyotolewa Oktoba 9, mwaka huu, Dk. Abbasi amesema ameulizwa kuhusu hukumu hiyo, na hivyo amelazimika kutoa ufafanuzi.

“Msingi wa kesi zote mdaiwa siyo serikali wala Tanesco, ni deni la benki dhidi ya IPTL (kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited) walilorithi miaka mingi kutoka kwa wakopeshaji wa Malaysia.

Kwa muktadha huo na kisheria, serikali na Tanesco ziliunganishwa tu kama kanuni za kisheria zinavyomruhusu mdai kuwaunganisha wahusika wengine kwenye kesi ili kupata uhakika kuwa analipwa madai yake," amesema Dk. Abbasi.

“Kwa muktadha huo, natumia fursa hii kuwatoa wasiwasi Watanzania, serikali haidawi, haijawahi kukopa Standard Chartered ya Hong Kong, ila kama Baraza la Usuluhishi lilivyoamua, tutahakikisha tunasimamia utawala wa sheria kwa kuona IPTL wanalipa deni lao,” amesema Dk. Abbasi.

Katika kesi hiyo ya ICSID yenye namba ARB/15/41, benki hiyo ilifungua kesi dhidi ya serikali ikidai kiasi hicho cha fedha kwa kile ilichodai ni kutokana na kukiukwa kwa mkataba wa manunuzi ya umeme uliokuwa umetiwa saini baina yao na pande tatu za mkataba huo.

Benki hiyo ilikuwa ikiwakilishwa na Matthew Weiniger wa QC Linklaters LLP One, Iain Maxwell, Aaron McDonald, Elizabeth Kantor, Harry Ormsby, Gavin Creelman na Herbert Smith wa Freehills LLP, wote kutoka Uingereza.

Hukumu hiyo inaonyesha Serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Adelardus Kilangi, Wakili Mkuu wa Serikali, Dk. Clement Mashamba, Beredy Malegesi wa Crax Law Partners, Richard Karumuna Rweyongeza wa R. K. Rweyongeza & Co. Advocates, Galileo Pozzoli, Mark Handley, Profesa Tullio Treves, Luciana Ricart, Irene Petrelli, Renato Treves na Valerio Salvatori Curtis wa Mallet-Prevost, Colt & Mosle LLP.

Chanzo: Nipashe

Mwanasheria Mkuu wa Serikali leo katika mahojiano maalum na TBC amesisitiza kauli ya jana ya Serikali kupitia kwa
Msemaji Mkuu wa Serikali kuwa Serikali haidaiwi na katika uhusiano wa kibiashara kati ya IPTL na Benki ya SCB Hong Kong.

Hukumu kwa Kwa kifupi imesema;-
V. The Government of United Republic of Tanzania shall;-
Pay to climant the sum of USD 185,449,440.04 together with interest thereonat the rate of LIBOR (6-Months) +2% from the 1 September 2018until the date of full and final payment and
VI. Bear its own legal costs and expenses

Pia soma
Screenshot_20191017-161356.jpeg
 
Anajidanganya yeye mwenyewe maana hakuna mwenye jeuri na mahakama za kimataifaView attachment 1236124
Huyu Dr Hassan Abas ni kama Comical Ali au Mohamed Sared AlSahhaf aliyekuwa Msemaji wa Saddam Hussein wakati wa vita vya ghuba mwaka 2003.

Nchi nzima ilishatekwa mpaka Airport ya Baghdad lakini yeye alikuwa anasema US Marines watakatwa vichwa wote wakitua Iraq na kwamba Saddam bado yuko in control.

Hawa wasemaji tuwahurumie tu, hawaruhusiwi kutumia akili zao. Huyu Dr Abbasi angekuwa na soko kwenye profession yake asingekubali kazi ya kijinga kama hii. Kazi ya kukanusha tu
 
Tunashangaa nini wakati Kikwete nae alishasema pesa ile haikuwa ya serikali?
 
Sawa, tunaendelea na mikakati yetu ya viwanda....Naipenda nchi yangu Tanzania......
Kweli hayatuhusu IPTL iliyokopa hizo pesa bado ipo haijafa ilipe madeni ya benki. Tanesco na Nchi ya Tz hayatuhusu!!!!!!!!!!
Niliona kuna watu wasio wazalendo wananza kufurahia uamuzi wa kesi hii. Watasubiri sana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Si kweli, bahati nzuri hukumu tunayo. Imesema kabisa kuwa serikali ya Tanzania kwa kukatisha mkataba.... Go and read!
Hukumu kwa Kwa kifupi imesema;-
V. The Government of United Republic of Tanzania shall;-
Pay to climant the sum of USD 185,449,440.04 together with interest thereonat the rate of LIBOR (6-Months) +2% from the 1 September 2018until the date of full and final payment and
VI. Bear its own legal costs and expenses
 
Brother una akili fupi sana!!!, hivi watu waliosaini walisaini kwa niaba ya???. Ni nani kashitakiwa na Nani kaumliwa kulipa??. Akili za kipoyoyo kujimwamba....
Unaweza ukasaini kama kugaranti mtu kwamba deni litalipwa lakini sio mdaiwa wa kwanza. Kwasababu mkopaji/mdaiwa wa kwanza yupo(IPTL) hajafa ajilipie deni lake.
 
Mara ya mwisho kusikia mtu anaunganishwa kwenye kesi mtu huyo aliyeunganishwa alilala ndani. Ilikua ni pale Mbowe na wenzake walipounganishwa kwenye kesi iliyopelekea maandamano na mauaji ya bint Akwilina (RIP), pia akina Rose Sanare na mkwe wa Lowasa walipounganishwa kwenye jesinya uhujumu uchumi, nao wapo ndani hadi leo.
Hivi huyu Dr. Abbas ni msemaji wa Simba au Serikali? Anaongea vitu bila ya weledi kabisa, yaani uunganishwe kwenye kesi bila kuwa sehemu ya kutuhumiwa au andhani wanaounganishwa kwenye kesi ni huwa ni kama wale ma maid na wapambe wa kwenye harusi kwamba wao ni wapambe tu lakini siyo waoaji?
Sasa munaona umuhimu wakuwa na umeme wetu wenyewe? Kesi za kijinga kama hizi huwezi kukutana nazo tena. Kweli Umeme wa Rufiji utakuwa mkombozi kwetu ndo maana upande wa wazungu hawakupenda project hiyo.
 
Gesi imetushinda nini?

Back
Top Bottom