Serikali yakana hukumu ya kuilipa ESCROW dola Mil 185. Dk. Abbasi asema Serikali haidaiwi

I
Yaani Serikali ya huyu jiwe imekuwa na sifa zote za kibinadamu sasa.. Maana serikali inaongopa, serikali ina roho mbaya, serikali ina husuda, serikali inatapeli, serikali inapora, serikali inaua, inafunga..
Na kwa hakika awamu ya tano itakumbukwa kwa Mambo haya na ndio maana wanajitahidi kujenga mamiundo mbinu hata yasiyolipa Leo Wala kesho ili tusiikumbuke kwa ubaya unayoifanya sasa
 
Yaani Serikali ya huyu jiwe imekuwa na sifa zote za kibinadamu sasa.. Maana serikali inaongopa, serikali ina roho mbaya, serikali ina husuda, serikali inatapeli, serikali inapora, serikali inaua, inafunga..
Na nibahati mbaya watu kama kina Samia kuwemo na majaliwa ambao ni wastaarabu watakapostahafu wataumia sana na mambo yaliyofanyika pindi wao wapo kwenye gvt mama samia hawezi kuwa na amani huku damu ya ben sanane ikimlilia "mama nilitendewa haya wewe ukiwa no 2" akwilina akwilina atamtokea kwenye ndoto mama niliuliwa kwasababu ya siasa za chama chako damu ya lisu zote hizi zitawatesa sana majaliwa na mama samia hata kama hawahusiki huyo mwingine simtaji maana yeye Moto ameanza kuuonja mapema ndio maana kila siku anaweweseka aombewe
 
Huwezi kuumiza watu jumamosi halafu jumapili unaenda kanisani ukiomba watu wale uliowaumiza wakuombee badala ya wewe kuwaomba msamaha yani Kuna watu kustahafu kwao utakuwa Ni msiba kwao na kwa vizazi vyao siku hazigandi
 
Huyu Dr Hassan Abas ni kama Comical Ali au Mohamed Sared AlSahhaf aliyekuwa Msemaji wa Saddam Hussein wakati wa vita vya ghuba mwaka 2003.

Nchi nzima ilishatekwa mpaka Airport ya Baghdad lakini yeye alikuwa anasema US Marines watakatwa vichwa wote wakitua Iraq na kwamba Saddam bado yuko in control.

Hawa wasemaji tuwahurumie tu, hawaruhusiwi kutumia akili zao. Huyu Dr Abbasi angekuwa na soko kwenye profession yake asingekubali kazi ya kijinga kama hii. Kazi ya kukanusha tu

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema "Mtu akikuambia jambo la kipumbavu na akijua kuwa nawe unafahamu kuwa ni jambo la kipumbavu lakini ukamkubalia, ANAKUDHARAU". Huyu Abbasi amedharauliwa hata na bosi wake.
 
Kweli hayatuhusu IPTL iliyokopa hizo pesa bado ipo haijafa ilipe madeni ya benki. Tanesco na Nchi ya Tz hayatuhusu!!!!!!!!!!
Niliona kuna watu wasio wazalendo wananza kufurahia uamuzi wa kesi hii. Watasubiri sana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Kama huna akili ya kuelewa mambo ni vyema ukakaa kimya.
 
Na nibahati mbaya watu kama kina Samia kuwemo na majaliwa ambao ni wastaarabu watakapostahafu wataumia sana na mambo yaliyofanyika pindi wao wapo kwenye gvt mama samia hawezi kuwa na amani huku damu ya ben sanane ikimlilia "mama nilitendewa haya wewe ukiwa no 2" akwilina akwilina atamtokea kwenye ndoto mama niliuliwa kwasababu ya siasa za chama chako damu ya lisu zote hizi zitawatesa sana majaliwa na mama samia hata kama hawahusiki huyo mwingine simtaji maana yeye Moto ameanza kuuonja mapema ndio maana kila siku anaweweseka aombewe
Ben atakuwa jini la kuzui maendeleo na amani ya watu ? Mtu akitoweka au kufa huo no mwisho wa wake .Roho haiwezi kurudia mwili tena. Hata Masalia ya mwili wake huliwa na funza. Roho haina ubongo wa kufikiri, Mawazo yake siyo ya mwili huu (haina mawazo)
Ben hana chochote cha kuzuia maendeleo na amani ya Tanzania.
 
Amina wapenda amani wanakuja kunisaidia kukujibu baradhuli wewe
 
Akizungumzia hukumu hiyo iliyotolewa Oktoba 9, mwaka huu, Dk. Abbasi amesema ameulizwa kuhusu hukumu hiyo, na hivyo amelazimika kutoa ufafanuzi.

“Msingi wa kesi zote mdaiwa siyo serikali wala Tanesco, ni deni la benki dhidi ya IPTL (kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited) walilorithi miaka mingi kutoka kwa wakopeshaji wa Malaysia.

Kwa muktadha huo na kisheria, serikali na Tanesco ziliunganishwa tu kama kanuni za kisheria zinavyomruhusu mdai kuwaunganisha wahusika wengine kwenye kesi ili kupata uhakika kuwa analipwa madai yake," amesema Dk. Abbasi.

“Kwa muktadha huo, natumia fursa hii kuwatoa wasiwasi Watanzania, serikali haidawi, haijawahi kukopa Standard Chartered ya Hong Kong, ila kama Baraza la Usuluhishi lilivyoamua, tutahakikisha tunasimamia utawala wa sheria kwa kuona IPTL wanalipa deni lao,” amesema Dk. Abbasi.

Katika kesi hiyo ya ICSID yenye namba ARB/15/41, benki hiyo ilifungua kesi dhidi ya serikali ikidai kiasi hicho cha fedha kwa kile ilichodai ni kutokana na kukiukwa kwa mkataba wa manunuzi ya umeme uliokuwa umetiwa saini baina yao na pande tatu za mkataba huo.

Benki hiyo ilikuwa ikiwakilishwa na Matthew Weiniger wa QC Linklaters LLP One, Iain Maxwell, Aaron McDonald, Elizabeth Kantor, Harry Ormsby, Gavin Creelman na Herbert Smith wa Freehills LLP, wote kutoka Uingereza.

Hukumu hiyo inaonyesha Serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Adelardus Kilangi, Wakili Mkuu wa Serikali, Dk. Clement Mashamba, Beredy Malegesi wa Crax Law Partners, Richard Karumuna Rweyongeza wa R. K. Rweyongeza & Co. Advocates, Galileo Pozzoli, Mark Handley, Profesa Tullio Treves, Luciana Ricart, Irene Petrelli, Renato Treves na Valerio Salvatori Curtis wa Mallet-Prevost, Colt & Mosle LLP.

Chanzo: Nipashe

Mwanasheria Mkuu wa Serikali leo katika mahojiano maalum na TBC amesisitiza kauli ya jana ya Serikali kupitia kwa
Msemaji Mkuu wa Serikali kuwa Serikali haidaiwi na katika uhusiano wa kibiashara kati ya IPTL na Benki ya SCB Hong Kong.

Serikali kama msimamizi wa utekelezaji itaibana kampuni ya IPTL ambayo bado ipo hapa nchini ikiwa na mitambo na raslimali nyingine, ikamilishe deni wanalodaiwa.

Hukumu kwa Kwa kifupi imesema;-
V. The Government of United Republic of Tanzania shall;-
Pay to climant the sum of USD 185,449,440.04 together with interest thereonat the rate of LIBOR (6-Months) +2% from the 1 September 2018until the date of full and final payment and
VI. Bear its own legal costs and expenses

Pia soma
Yakijirudia yale ya south africa ndio tutajua mbivu na mbichi.
 
Amina wapenda amani wanakuja kunisaidia kukujibu baradhuli wewe
Hicho ni sawa na kuita waliokufa waje kupiga selfie.Hakika Hutawaona kamwe kwenye hiyo movie yako.
Waliokufa ni roho tupu. Selfie zao ni za kiroho roho siyo digital camera za techno

Any how, Amani yao ni ya kiroho zaidi huko waliko.
Ya hapa duniani waachie wenye mwili na Mungu wao. Siyo Ben
 
Serikari sio mdhamini wa deni la IPTL wala aliwahusu guarantee waliyoitoa kwa mkopaji iwapo IPTL watashindwa lipa deni au wakiingia kwenye liquidation provided kampuni inauwezo wa kuzalisha na kuuza umeme wao wataendelea kununua mpaka mkataba utakapoisha. Na wametiza wajibu sasa unajiuliza why on earth huu dili na standard charter kabla ya kumtaka aanze ku deal na management ya IPTL kwanza, siasa uchwara zina madhara sana.
 
Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID), imeiamuru Tanzania kulipa Dola za Marekani milioni 185 pamoja na riba kwa madai ya uharibifu ilioufanya kwenye Benki ya Standard Chartered (Hong Kong) kuhusu mzozo wa akaunti ya IPTL Escrow.

Hata hivyo, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbas jana kupitia ukurasa wake wa Twitter, alitoa ufafanuzi wa hukumu hiyo na kusema kuwa deni hilo siyo la serikali bali ni la Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).

Katika maelezo yake Dk. Abbas alisema kuwa serikali itahakikisha wanasimamia utawala wa sheria ili IPTL ilipe deni lao.

"Nimekuwa nikiulizwa kuhusu kesi zilizoamuliwa za Benki ya Standard Chartered (Hong Kong) dhidi ya Tanesco na sasa serikali. Msingi wa kesi zote mdaiwa si serikali wala Tanesco, ni deni la Benki dhidi ya IPTL walilorithi miaka mingi kutoka wakopeshaji wa Malaysia."

"Kwa muktadha huo na kisheria serikali na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ziliunganishwa tu kama kanuni za kisheria zinavyomruhusu mdai kuwaunganisha wahusika wengine kwenye kesi ili kuhakikisha au kupata uhakika kuwa analipwa madai yake," alifafanua.

Dk. Abbas aliwatoa wasiwasi Watanzania kuwa serikali haidaiwi na haijawahi kukopa Standard Charterd ya Hong Kong.

"Ila kama Baraza la Usuluhishi lilivyoamua, tutahakikisha tunasimamia utawala wa sheria kwa kuona IPTL wanalipa deni lao," alisema.

Hukumu ya kesi hiyo ilifanyika Oktoba 11, mwaka huu na jopo lililosikiliza shauri hilo liliundwa na David Unterhalter kutoka nchini Afrika Kusini, aliyeteuliwa na mlalamikaji na Kamal Hossain kutoka nchini Bangladeshi aliyeteuliwa na mlalamikiwa.

Julai 11, mwaka 2016 Unterhalter aliteuliwa baada ya kujiuzulu kwa Stanley Burnton kutoka Uingereza.Wawakilishi wa mlalamikaji walikuwa ni Herbert Freehills kutoka Uingereza na wa mlalamikiwa ni kampuni ya uwakili ya Crax Low Partners na Rweyongeza and Company Advocates za jijini Dar es Salaam.

Mwaka jana pia, mahakama hiyo ya ICSID iliikataa rufani ya Tanesco ya kupinga hukumu ya kuilipa Benki ya Standard Chartered Dola za Marekani milioni 148.4 sawa na Sh. bilioni 336.

Katika kesi hiyo, Rais wa ICSID, Claus von Wobeser alitupilia mbali hoja za Tanesco za kuitaka mahakama hiyo kutengua uamuzi wa awali ulioipa ushindi benki hiyo ya Hong Kong, nchini China.

Fedha hizo ni madai ya malipo ya umeme baina ya Tanesco na IPTL iliyopewa zabuni ya kufua umeme wa dharura kuanzia Mei 26, mwaka 1995 huku ikidaiwa na benki hiyo.

Chanzo: IPP Media
 
Kujiandikisha ni jambo moja, kupiga kura kwa usahihi ni kitu kingine. Mnakumbuka kura za maruhani?
 
Changanya na zako wewe bwege,unapokeaje maelezo yasiyo na tija kwa mwanasheria wa serikali bila kwanza kutafuta ukweli wa hoja yake?
Walau ungejiuliza,kama serikali haihusiki na hilo deni,ni kwa nini walipeleka wanasheria wao huko mahakamani?
Na ni kwa nini serikali imetajwa kama mdaiwa kwenye kesi hii???
Ukiwa na majibu sahihi basi unaweza kusema unachosema
Mku serikali ni mdhamini mkopaji ni IPTL na bado yupo atajilipia madeni yake
 
Back
Top Bottom