Bashe: Serikali imeamua korosho yote itabanguliwa Mtwara 2025/26. Asema kuuza korosho ghafi ni biashara ya kizamani

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,446
7,817
Akiwa kwenye ziara ya Rais Samia leo Septemba 16, 2023 waziri Bashe ameongelea suala la korosho alipotakwa na Rais Samia aelezee bei ya msimu huu.

Bashe amesema bei ya mbaazi na ufuta ilikuwa ilikuwa inaridhisha na wanaomba Mungu wakitaraji pia bei ya korosho itakuwa njema.

Pia Bashe amesema kwasasa duniani uzalishaji na kuuza korosho ghafi imekuwa ni biashara ya kzamani. Bashe amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia imeamua itakapofika mwaka 2025/26 korosho yote itabanguliwa Mtwara eneo la kijiji cha Maranje na Serikali imeanza kulipa fidia eneo la ukubwa wa ekari 1500 na linaanza kusafishwa mwezi wa 11 na ujenzi wa viwanda unaanza mara moja.

Bashe amesema bei itaimarika na soko litakuwa la uhakika kuliko kuwategemea wa-vietnam.
 

Attachments

  • Bashe_Bei ya Korosho.mp4
    62.4 MB
Nenda kwenye hoja ya bei ya korosho, kumu attack Bashe personally ni udhaifu na wivu. Na wale wenye mediocre minds ndiyo wanaokufa kwa wivu.

Wewe huna ubavu wa kuwashinda IQ hao washikaji wa Bashe
Wizara yake amewajaza maswaiba wake hata wasio na sifa. Vibali hutolewa kama njugu kwa wasio na sifa alimradi wewe ni mshikaji. Bashe anaendelea kusimika mtandao hatari sana ndani ya chama na Serikali
 
Back
Top Bottom