Serikali yadai nusu ya walioenda COP28 wamejigharamia wengine wamegharamiwa na sekta binafsi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
1701617288167.png
Serikali imesema karibu nusu ya ujumbe wa Tanzania ulioshiriki Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28), umegharamiwa na sekta binafsi.

Ufafanuzi huo, umekuja baada ya juzi na jana kusambaa kwa taarifa katika mitandao ya kijamii kuhusu idadi kubwa ujumbe wa Tanzania ulioshiriki COP 28 ukilinganisha na mataifa mengine.

Mkutano COP 28 ambao Tanzania ni mwanachama umeanza Novemba 30 Novemba hadi 12 Desemba 2023, Dubai.

Idadi hiyo iliibua maswali na majadala katika mitandao ya kijamii huku watu wakihoji wingi wa watu hao, wengine walikwenda mbali wakisema hakukuwa na ulazima wa wingi wa watu hao.

Lakini leo Jumapili Desemba 3,2023 Serikali kupitia Ofisi ya Makamu ya Rais,(Muungano na Mazingira) imesema Watanzania 763 walijiandikisha kushiriki mkutano huo kati yao 391 walitoka wizara na taasisi za Serikali.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa watu 372 walijiandikisha kutoka mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, sekta binafsi, vijana na watoto.

“Hata hivyo idadi ya Watanzania wanaoshiriki kutoka Serikalini ni 66 kati yao 56 wanatoka Tanzania Bara na 10 Zanzibar sawa na asilimia 8.7 ya Watanzania waliojiandikisha.

“Sehemu kubwa ya washiriki wanatoka katika sekta binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na vijana na watoto ambayo ni 340 sawa na asilimia 45,” imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa baadhi ya washiriki kutoka wizara na taasisi za Serikali wamefadhiliwa na mashirika ya kimataifa huku wale wa sekta binafsi, taasisi za kiraia, vijana na watoto wanashiriki kwa gharama zao wenyewe, hatua inayonyesha mwamko kwa Watanzania

Msimao wa Tanzania kwenye mkutano huo

Tanzania ilitaja mambo makubwa manne itakayosimamia kwenye mkutamno huo ambayo ni fedha za ufadhili kwa kuzingatia athari za mabadiliko ya tabianchi, mfuko wa pamoja wa majanga na maafa, matumizi ya nishati safi na jumuishi na mjadala wa jinsia unaompa mwanamke kipaumbele imetajwa kama misimamo ya nchi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na wadau mbalimbali kutoka nchini wameshiri mkutano utahudhuriwa na washiriki zaidi ya 70,000 kutoka nchi takribani 190.

Taarifa iliyotolewea na Ikulu ilibainisha , “Tanzania inaunga mkono hoja ya kuongeza fedha za ufadhili kwa kuzinga tia athari zinazozidi kuongezeka kwa sasa na kuhakikisha ahadi ya nchi zilizoendelea kutoa dola 100 bilioni (Sh250 trilioni) kila mwaka kwa nchi zinazoende-lea kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi zinatimizwa”.

Jambo jingine ni “Kuhakikisha mkutano unaridhia uanzishwaji wa mfuko wa kupambana na majanga na maafa, Kuhakikisha juhudi za kuelekea matumizi ya nishati safi zinakuwa jumuishi na mjadala wa masuala ya jinsia unazingatia maadili ya kitaifa na kijamii na wanawake wanapewa kipaumbele”.
 
Maswali ni mengi kuliko majibu. Kwa mfano;

1. Ni sekta binafsi gani hiyo inayoweza kupoteza pesa zake ili kugharamia maafisa wa serikali, umma, makada, mahawala na chawa kwenda Dubai?

2. Sekta binafsi ina maslahi gani ya moja kwa moja na mambo ya tabia nchi mpaka iwagharamie watu ovyo ovyo kwenda Dubai kwenye huo mkutano?

3. Tangu lini serikali imeanza utaratibu wa kuruhusu uholela wa watu binafsi kudandia kama wajumbe katika safari za Rais za nje ya nchi hata kama watajigharamia wenyewe? Serikali inajua athari na hatari zake?

4. Kwanini wameshindwa kutoa orodha ya majina na taasisi husika zilizogharamia hao watu kwenda Dubai kama wajumbe ili umma uweze kuamini na kuelewa.

Yaani hiyo taarifa inataka kusema, ujumbe wa Tanzania wa Rais nje ya Tanzania huwa hautegemei mipango, malengo na bajeti ya serikali bali hutegemea mwitikio na uwezo wa sekta binafsi kufadhili hilo. Ni kichaka cha sababu za kijinga na kipuuzi kabisa.
 
Waweke evidence sio kutufanya wajinga
Hata kama mashirika binafsi wote hawa walienda kufanya nini

Halafu Wazungu wanajua sana kutugeuza mazezeta
Mkutano wa climate uharo halafu ndege ngapi zilikuwa angani kwenda kwenye mkutano fake
Wangetumia ZOOM tungewaelewa

Back kwa mada….

Siri kali wekeni evidence hapa ama sivyo rudisheni pesa yetu
 
nimekumbuka tu ile sherehe iliyofanywa na na Shaha wa Iran kule jangwani... zile akili zinafanana na hizi.
 
Chadema sasa watafute hoja nyingine
Wewe nawe sasa umezidi upumbavu! Hii si hoja ya CHADEMA! Hii ni hoja ya Watanzania wote!
Serikali haiwezi kuwa na matumizi ya kiwendawazimu halafu watu wakae
kimya tu!
Wewe ni mpuuzi sana na unaleta hapa ushamba wako wa kisukuma hapa!
Mara umshabikie Makonda eti anawazidi kisiasa viongozi wengi wakati unaona Makonda anafanya kazi bila kuzingatia sheria wala mipaka yake ( Utra vires)!
Hako ka knowledge ka sheria sijui kanakusaidia nini?!
Wewe ni Kilaza sana !
 
Wewe nawe sasa umezidi upumbavu! Hii si hoja ya CHADEMA! Hii ni hoja ya Watanzania wote!
Serikali haiwezi kuwa na matumizi ya kiwendawazimu halafu watu wakae
kimya tu!
Wewe ni mpuuzi sana na unaleta hapa ushamba wako wa kisukuma hapa!
Mara umshabikie Makonda eti anawazidi kisiasa viongozi wengi wakati unaona Makonda anafanya kazi bila kuzingatia sheria wala mipaka yake ( Utra vires)!
Hako ka knowledge ka sheria sijui kanakusaidia nini?!
Wewe ni Kilaza sana !
😂😂😂
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA MAKAMU WA RAIS

TAARIFA YA KWA VYOMBO VYA HABARI

02 Desemba 2023, DUBAI - UAE

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inashiriki katika Mkutano wa 28 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi.
Mkutano huo umeanza tarehe 30 Novemba hadi 12 Desemba 2023, Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu ambapo washiriki wakiwemo wakuu wa nchi na Serikali zaidi ya elfu themanini na moja kutoka nchi takriban 190 wanahudhuria mkutano huo.

Ikumbukwe kwamba jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya Tabinchi zinahusisha wadau mbalimbali ikiwemo Serikali, Asasi za Kiraia, Sekta Binafsi, Vijana na Watoto, hivyo, Idadi kubwa ya Watanzania ilionyesha nia ya kushirki katika mkutano huo wa kimataifa ambapo Jumla ya Watanzania 763 walijiandikisha kwa nia ya kushiriki.

Kati ya idadi hiyo Watanzania 391 walijiandikisha kutoka Wizara na Taasisi za Serikali,

wakati 372 walijiandikisha kutoka Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, Sekta binafsi, Vijana na Watoto.

Hata hivyo idadi ya Watanzania wanaoshiriki kutoka Serikalini ni 66 ambapo hamsini na sita (56) wanatoka Tanzania Bara na 10 kutoka Zanzibar ambayo ni sawa na asilimia 8.7 ya watanzania waliojiandikisha.

Aidha, sehemu kubwa ya washiriki inatoka katika Sekta Binafsi, Mashirika yasiyo ya Kiserikali pamoja na vijana na Watoto ambayo ni 340, sawa na asilimia 91.3.

Baadhi ya Washiriki kutoka Wizara na Taasisi za Serikali wamefadhiliwa na Mashirika ya Kimataifa aidha washiriki kutoka Sekta Binafsi, Taasisi za kiraia, vijana na watoto
wanashiriki kwa gharama zao wenyewe.

Hii inaonyeha mwamko wa Watanzania kuhusiana na masuala ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabia nchi.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
Ofisi ya Makamu wa Rais ( Muungano na Mazingira)
 
Back
Top Bottom