Kwa sasa hivi pesa ya kigeni hususani dola haipatikani hata kwenye mabenki ambayo sekta zetu binafsi zinafanya nazo biashara. Mambo yanakwama inapofika kuagiza mahitaji kutoka nje ambavyo ni sehemu ya utekelezaji wa kazi yoyote au mradi. Hata dola 1000 kupata ni tatizo.
Je, kitu gani kinaendelea? Mimi na umri wangu mkubwa tumepitia changamoto nyingi za kiuchumi toka enzi za Mwalimu lakini jambo kama hili halikuwahi kutokea. Sasa tunaelekea wapi? Mbona hata hakutolewi tamko kuelezea hili jambo? Je, waziri wa fedha haoni kwamba hili ni tatizo?
Miaka michache ya nyuma na hususan wakati wa Hayati Magufuli tulikuwa tunapewa taarifa kuwa nchi yetu ina akiba ya kutosha na wakawa wanataja hata kipindi ambacho kama itokee dhiki ya namna gani, kwa akiba iliyopo tungeweza kumudu kuagiza nje kwa miezi kadhaa. Sasa hii akiba imeenda wapi?
Jamani tuzidi kujitafakari, kuna tatizo mahali.