Serikali yaanza rasmi Biashara ya kuuza mafuta nchini

Hiyo ni kampuni imeazishwa itafanya kazi kama kampuni nyingine zinavyofanya kazi.Mbona serikali inamiliki 50% kwenye PUMA Energy hakuna shida kama kuna usimamizi mzuri tuu.Na ikwa inalipa kodi na kutoa gawio kama wengine ni jambo zuri.Kutaleta ushindani kama wengine
Mkuu naomba kueleweshwa. Kwa nini serikali isiongeze hisa zake PUMA ENERGY badala ya kuanzisha kampuni mpya kabisa? Tukumbuke pia serikali yenyewe ni "Regulator" pia.
 
Mimi nadhani serikali ibaki na Umeme. Maji. Na labda treni tu. Hizo ni biashara nyeti na serikali inahitaji kusimamia. Nyingine iachie private sector tu na kuisimamia.
 
kwenye sekta ya mafuta serikali imeshindwa kabla ya kuanza maana mbali na TANOIL kuna GPSA ni wauzaji na wasambazaji wa mafuta ya serikali lakini hakuna ubunifu wowote katika hiyo tasisi miaka nenda miundo mbinu ya pump zao ni ile ile na uendeshaji wake umejaa magumashi
 
View attachment 1472096

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amezindua rasmi biashara ya kuuza na kusambaza mafuta nchini kwa kufungua kituo cha kwanza kuuza mafuta ya Petroli na Dizeli cha Serikali kitakachosimamiwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) kupitia Kampuni yake Tanzu ya Mafuta ( TANCOIL). Aidha Dkt. Kalemani alisema kuwa kuzinduliwa na kufunguliwa kwa biashara hiyo ni kutimiza azma na nia njema ya Serikali ya kuboresha shirika lake la TPDC,kuwapatia na kuwasogezea karibu wananchi wake huduma ya kupata mafuta yenye viwango vya ubora unaotakiwa, bei nafuu, na yatakayopatikana kwa wingi muda wote.

Dkt. Kalemani alifanya Uzinduzi huo pamoja na kufungua kituo hicho wilayani Musoma, mkoani Mara Juni 6, 2020, wakati wa ziara yake ya kikazi katika Mkoa huo, akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Zena Said pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Wizara hiyo na Taasisi zilizochini yake. Alisema baada ya kuanza rasmi kwa biashara hiyo, TPDC kupitia TANCOIL itashirikiana na Halmashauri zote nchini kuhakikisha inafanikisha azma ya Serikali ya kufungua na kuweka vituo vya kuuza na kusambaza mafuta katika kila halmashauri nchini pamoja na miundombinu ya kuhifadhi na kusafirisha mafuta.

Dkt. Kalemani aliwaeleza watanzania kuwa TPDC na TANOIL watashiriki katika biashara ya uagizaji na usambazaji mafuta kama zinavyofanya kampuni zingine za mafuta nchini ili kuongeza ushindani na kutanua wigo wa kampuni za kizalendo kushiriki katika biashara ya mafuta, ambayo kwa sasa inafanywa na makampuni kutoka nje ya nchi tu. Alisema kuwa serikali kupitia TPDC itajenga vituo 100 kwa kipindi cha miaka 5 ijayo, tayari baadhi ya Halmashauri zimeanza kutenga maeneo yatakayojengwa vituo hivyo: Aidha itahakikisha kuwa nusu ya mafuta yote yanayoingizwa nchini yanasimamiwa TPDC.
Naanza kuelewa sasa "...yule aliyesema 'ya fastjet" shaka ni kuwa kwanini waliwaruhusu waagizaji binafsi? Kwanini Tipper iliacha kusafisha mafuta ghafi nchini? Kwanini kulikuwa na bei elekezi...? Kwanini....??? Je zile changamoto zilizofanya serikali ijitoe wamezipatia ufumbuzi?
Aaaaah na tunyamaze tu
 
Hawa jamaa hawashauriwi vizuri. Mtu akiamka na mke wake ana wazo flani basi linatekekezwa. Wanahisi sekta binafsi inafaidi sana.


Ni mpamgo wa kunyon'gonyesha sekta binafsi... Kodi kubwa, kufungiwa biashara, na serikali kuingia ktk biashara...
 
Polisi jijini Dsm imewakamata wakurugenzi wakuu wa kampuni za mafuta za Puma, Total na Oryx waliokuwa kwenye kikao cha kibiashara.
Kadhalika polisi wanamsaka mkurugenzi mkuu wa Lake Oil ili aunganishwe na wenzake.

Imeelezwa wakurugenzi hao wanadaiwa kuvuruga mfumo wa usambazaji mafuta nchini.

Source ITV habari!
 
Mafuta sio biashara kama biashara nyingine.

Unapozungumzia mafuta unazungumzia national security ya nchi.

Mataifa yenye kuzalisha mafuta utakuta National Oil Companies (NOC) zao zina shiriki kwenye value chain zote kuanzia kwenye kutafuta mpaka retail and petrochemical industries too. Na nchi nyingi tu state companies zinauza retail ata kama awachimbi mafuta.

Na nchi zisizo shiriki basi zinashirikiana kimkakati na kampuni binafsi mfano hakuna mtu anaweza chimba mafuta North Sea upande wa UK zaidi ya Shell, ukichezea maslahi ya makampuni ya marekani USA hayo yanayoitwa private popote duniani subiri fujo za serikali yao. Ukienda India karibu makampuni yote ya mafuta shareholder ni serikali.

Kwa nchi kama Tanzania TPDC ushiriki wake kwenye energy security ni mdogo sana it’s about time waanze kufanya investment storage yenyewe ya nchi nzima sidhani kama inamudu mwezi wakati ushauri wa ‘International Energy Agency’ kila nchi inatakiwa walau iwe na uwezo wa kuweka akiba ya miezi mitatu.

Nani atawekeza kwenye hizo infrastructure zaidi ya TPDC na kama unajukumu hilo ni bora pia uuze mafuta upate kipato faida uwekeze kwenye infrastructure za mkakati.

Bado kuna swala la military strategies na mafuta.

In short biashara na umuhimu wa mafuta ulimwengu wa leo ni swala la kimkakati na ukikosea it could be very costly government have been toppled kwa sababu ya mafuta.

Upuuzi ni kusema TPDC ndio itakayokuwa inaagiza nusu ya mafuta yanayoingia nchini wao pekee au wakianza sabotage zingine za sector kama ilivyo adha kisa kukurupuka bila ya business plan.
Aijachukua hata muda utabiri kutokea watavuruga soko tu.
 
Polisi jijini Dsm imewakamata wakurugenzi wakuu wa kampuni za mafuta za Puma, Total na Oryx waliokuwa kwenye kikao cha kibiashara.
Kadhalika polisi wanamsaka mkurugenzi mkuu wa Lake Oil ili aunganishwe na wenzake.

Imeelezwa wakurugenzi hao wanadaiwa kuvuruga mfumo wa usambazaji mafuta nchini.

Source ITV habari!
Imagine akili gani unaenda kukamata watu ambao wapo kwenye kikao cha dispute resoulution.
 
Mafuta ni utajiri mkubwa sana serikali wasichukue nusu wachukue full business na kutimua wawekezaji mabeberu wa kampuni binafsi
Serikali wajiongeze kwa kuchukua tenda za mafuta nchi jirani nao tuwaagizie na tuwauzie
 
Vichwa vyetu vimegubukwa na siasa kuliko uhalisia, tunato mifano mibgi iliyotuzunguka ila tunachowaza ni siasa na negative thinking tu!

BP - British Petroleum
TOTAL - Wafaransa
AGIP - Wajerumani

Aidha hofu ya wafanya biashara ya mafuta inatoka wapi mbona tuna TTCL na VODACOM, TiGO, AIRTEL, ZANTEL, HALOTEL, SMART, nao wanaendelea na biashara zao tena far much better kuliko hao TTCL?

TBC wanafanya biashara lakini hawamshiki mkono ITV, AZAM TV, CLAUDS TV, WASAFI TV wala ETV, tena ukiangalia ufanisi pamoja na TBC kuwa na facilities zote na man power kubwa yenye kuongozwa na Dr. Ayubu Chacha Ryoba mmbobezi katika tasnia lakini hawafanyi vyema kama AZAM TV hofu yenu ni ipi wakulungwa.

Mifano ni mingi sana naomba tusitushane. Serikali iendelee kufungua vituo vya mafuta na Oilcom, PUMA, GAPCO, wataendelea kufanya kazi.
 
Biashara ya Mafuta kwa wafanyabiashara Binafsi Ndio kwaheri hio. Mark my words.
 
Mimi ni kijani naamini Mkulu atasikia hili namsihi achukue hii fursa kama chanzo kipya cha mapato ya serikali na kuleta nafuu kwa wapigakura wake kupitia kupunguza kodi za maduka mitaani ambayo mitaji inakata maduka yanafungwa kila siku kodi kubwa , mapato ya mafuta yatumike kufidia punguzo la kodi za maduka mitaani na kuwaletea raia nafuu ya maisha na hapo atawafunga mdomo Bwana Nape na Prof Mukandala ambao wanasema Mkulu hafuati ilani ya Chama inayomtaka kujali maendeleo ya watu kwanza na si miundombinu!!

Nashauri Mkulu tunaemkubali sana aunde kamati ya kudumu ya huu uwekezaji mpya wa mafuta, Mkuu wa Majeshi mstaafu awe Mwenyekiti , katibu awe Bashe ila asaidiwe na Zitto atakaempa mawazo mbadala na kinzani ( watu hawa wawili ni geniuses kwa mawazo yangu)

Naishauri serikali sasa iamue inunue na kuuza mafuta yenyewe kwenye vituo vyake nchini na ichukue tenda za mafuta nje ya nchi tutaona matunda yake muda mfupi tu kuna hela sana huko kwenye mafuta ndo maana mabeberu hawaachii na serikali wakipata faida tupunguziwe kodi za biashara za maduka yetu mitaani, muda wa mabeberu kuiba bongo umeisha!!

Inaitwa state capitalism, na inawezekana tu kama nchi ina utawala wa sheria au Rais mbabe na jasiri ambae huwanyoosha mafisadi na wazembe bila ajizi, najua hiki ninachosema nimekisomea tena nje si hapa elimu ya kukariri , tatizo letu bongo ni kukosa watu sahihi tu kusimamia miradi, uwekezaji huu unawezekana in one day, kupanga ni kuchagua! hata ukuta wa Mererani wapinzani walibeza ila kwa nguvu ya Magu leo yametolewa mawe ya ajabu!
 
Back
Top Bottom