Serikali yaanza rasmi Biashara ya kuuza mafuta nchini

Serikali yaanza rasmi Biashara ya kuuza mafuta nchini

Hiyo hatua ni nzuri.Huwenda mafuta ikawa sio ghali sana
Kwani kuna mtu anafanya biashara ya kusambaza umeme na maji pamoja na kukusanya kodi? Mbona havina afueni? Jiengeze mkuu.

Mfumo wa dunia wa sasa hivi unalenga serikali kutokujihusiaha na biashara bali ni kukusanya kodi tu zitokanazi na hizo biashara, sisi ndio tunaelekea the opposite direction. Nini kifuatacho? Kuuza nafaka, vipodozi na mitumba? Be careful what you wish for mkuu!
 
Vichwa vyetu vimegubukwa na siasa kuliko uhalisia, tunato mifano mibgi iliyotuzunguka ila tunachowaza ni siasa na negative thinking tu!

BP - British Petroleum
TOTAL - Wafaransa
AGIP - Wajerumani

Aidha hofu ya wafanya biashara ya mafuta inatoka wapi mbona tuna TTCL na VODACOM, TiGO, AIRTEL, ZANTEL, HALOTEL, SMART, nao wanaendelea na biashara zao tena far much better kuliko hao TTCL?

TBC wanafanya biashara lakini hawamshiki mkono ITV, AZAM TV, CLAUDS TV, WASAFI TV wala ETV, tena ukiangalia ufanisi pamoja na TBC kuwa na facilities zote na man power kubwa yenye kuongozwa na Dr. Ayubu Chacha Ryoba mmbobezi katika tasnia lakini hawafanyi vyema kama AZAM TV hofu yenu ni ipi wakulungwa.

Mifano ni mingi sana naomba tusitushane. Serikali iendelee kufungua vituo vya mafuta na Oilcom, PUMA, GAPCO, wataendelea kufanya kazi.
Na hili la siri-kali kuwakamata wakurugenzi wa mashirika shindani (competitors) na kuwarundika ndani limekaaje??!
 
Wananchi kupiga si ndo vizuri!
Kwani mkuu hujui kama CCM ni wachawiii? Wanataka kila mtu avae ndara na atembee kwa miguu huku tunarushiana vumbi huku wachache wao wanatembelea V8 na wanawaachia wengine wakiendelea kuwaabudu. Ujamaa ni dini ya Paganism. Mkuu wa nchi hugeuja kuwa Mungu!
 
View attachment 1472096

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amezindua rasmi biashara ya kuuza na kusambaza mafuta nchini kwa kufungua kituo cha kwanza kuuza mafuta ya Petroli na Dizeli cha Serikali kitakachosimamiwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) kupitia Kampuni yake Tanzu ya Mafuta ( TANCOIL). Aidha Dkt. Kalemani alisema kuwa kuzinduliwa na kufunguliwa kwa biashara hiyo ni kutimiza azma na nia njema ya Serikali ya kuboresha shirika lake la TPDC,kuwapatia na kuwasogezea karibu wananchi wake huduma ya kupata mafuta yenye viwango vya ubora unaotakiwa, bei nafuu, na yatakayopatikana kwa wingi muda wote.

Dkt. Kalemani alifanya Uzinduzi huo pamoja na kufungua kituo hicho wilayani Musoma, mkoani Mara Juni 6, 2020, wakati wa ziara yake ya kikazi katika Mkoa huo, akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Zena Said pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Wizara hiyo na Taasisi zilizochini yake. Alisema baada ya kuanza rasmi kwa biashara hiyo, TPDC kupitia TANCOIL itashirikiana na Halmashauri zote nchini kuhakikisha inafanikisha azma ya Serikali ya kufungua na kuweka vituo vya kuuza na kusambaza mafuta katika kila halmashauri nchini pamoja na miundombinu ya kuhifadhi na kusafirisha mafuta.

Dkt. Kalemani aliwaeleza watanzania kuwa TPDC na TANOIL watashiriki katika biashara ya uagizaji na usambazaji mafuta kama zinavyofanya kampuni zingine za mafuta nchini ili kuongeza ushindani na kutanua wigo wa kampuni za kizalendo kushiriki katika biashara ya mafuta, ambayo kwa sasa inafanywa na makampuni kutoka nje ya nchi tu. Alisema kuwa serikali kupitia TPDC itajenga vituo 100 kwa kipindi cha miaka 5 ijayo, tayari baadhi ya Halmashauri zimeanza kutenga maeneo yatakayojengwa vituo hivyo: Aidha itahakikisha kuwa nusu ya mafuta yote yanayoingizwa nchini yanasimamiwa TPDC.
Naomba bei zake plz
 
Waanzishe na kufufua mabasi ya usafirishaji ya mikoa kama Kauru, kaumu, kauta, kaudo na kadhalika maana hawa wafanya biashara wanapiga sana ela
Ongeza
RTC
National Milling
Kabimita
Mwadeco
Mudeco
Tardeco
nk
 
Tunajenga taifa hodhi la ajabu sana. Kupanga ni kuchagua, vituo vya mafuta ni pety buss kwa sasa wapo wajasiliamali wengi wadogo na wa kati. Endapo lipo swala la usalama bora serikali ingejipanga kuagiza bulk pekee.
We acha swaga zako . Wahisani wako waliohimiza kuua makampuni nchini mwaka wana Ma biashara makubwa kabisa makampuniyanayomilikiwa na serikali yameoteshwa mizizi. Hakuna tatizo kama makampuni yetu yakakamata share maana ni petty co zetu hazina uwezo wa kushika uchumi kisawasawa
 
Na hili la siri-kali kuwakamata wakurugenzi wa mashirika shindani (competitors) na kuwarundika ndani limekaaje??!
Taarifa yenyewe uliisikia? Au umeamua kurunga ya kwako Mkuu!

Ni utaratibu wa kawaida kila Julai 1 ndio mwaka mpya wa bajeti. Na huambatana na kupanda kwa gharama ya vitu pendekezwa kwenye bajeti.

Hivyo ni kawaida sana kwa wafanya biashara kuficha bidhaa kwa ajili ya kujipatia SUPER NORMAL PROFIT sasa Serikali imewastukia na Kosa lenyewe wamekiri na kwa mujibu wa sheria za EWURA kosa Hilo faini take ni Milioni 10.

Karibu tena kijana
 
Serikali na kufanya biashara! Wacha tuone.
Wakiondoa urasmu wanaweza kufanikiwa.

Mfano wa urasmu ni kama ifuatavyo:

Unaandika imprest kwa ajili ya ela ya kupalilia magugu kwenye shamba la umma la mahindi la ekari 100 . Ela hiyo unakuja kuipata baada ya miezi miwili... Majani magugu yameisha meza mahindi !!! Na bado wanakuja( wakuu) kukulaumu kuwa huwezi kazi. Wakati huo huo hawataki kukupa ela yote ya kugharamia mradi huo wa mahindi toka kuandaa shamba mpaka kuvuna. Wanakupa ela kwa awamu awamu.

Biashara kama hizi zinazojali muda hazitaki urasmu wa namna yeyote kwenye uendeshaji wake. Serikali uondoe urasimu huu ambao unalazimika fomu ya kuomba ela isainiwe na watu kibao kabla ya kuidhinisha ela hiyo na hivyo kuchelewesha upatikanaji wa ela kwa wakati.
 
Serikali inakwenda kutengeneza hasara nyingine mbaya kabisa. Hii biashara usimamizi wake ni umafia mtupu.
 
Sioni vipi sekta binafsi inaweza shindana na serikali. Yale yale ya FastJet kujirudia.. but all in all kwetu walaji wa mwisho inaweza kuwa nafuu... let's wait and see
Mbona TTCL wamekwama? Na bank ya Posta je, is It any better? Huu ni Upuuzi tu wa Kutamani kila senti inayopita mbele yao, tayari Magu alishaua biashara ya Korosho
 
Mbona TTCL wamekwama? Na bank ya Posta je, is It any better? Huu ni Upuuzi tu wa Kutamani kila senti inayopita mbele yao, tayari Magu alishaua biashara ya Korosho
Mkuu serikali haishindwi jambo...serikali iliitengeneza NMB vivyo hivyo serikali itaweka magari yote ya serikali kujaza mafuta station za TPDC hapo ndo itakuwa imeshinda katika hii biashara na station nyingine zitakufa tu
 
Ifike hatua serikali iachie sekta binafsi kuendesha baadhi ya maeneo,sio kila sehemu inataka ishindane kwa sababu fikilia kama kituo kikiishiwa mafuta na michakato ya serikali kuandikia barua mpaka zisainiwe maofsini na wakurugenzi,sheria za manunuzi n.k kwa upande wangu naona kuna vituo vitakaa takribani siku 2 bila mafuta huku vikisubiri mchakato wa manunuzi.
 
Back
Top Bottom