Serikali yaanza rasmi Biashara ya kuuza mafuta nchini

Serikali yaanza rasmi Biashara ya kuuza mafuta nchini

Hiyo ni kampuni imeazishwa itafanya kazi kama kampuni nyingine zinavyofanya kazi.Mbona serikali inamiliki 50% kwenye PUMA Energy hakuna shida kama kuna usimamizi mzuri tuu.Na ikwa inalipa kodi na kutoa gawio kama wengine ni jambo zuri.Kutaleta ushindani kama wengine
 
Halafu utakuta kampuni hii inaendeshwa kwa hasara Kama zilivyo kampuni zingine za serikali. Na hivyo, kutegemea Ruzuku toka serikalini kuweza kujiendesha.
 
Angalia na upande wa pili kiuchumi, ambao ndio wa msingi zaidi na manufaa kwa wananchi na maendeleo yao. Ushindani kwa upatikanaji na bei wa hiyo nishati muhimu ni jambo la kheri kuliko hiyo dhana yako ya kufikirika ikiongozwa na mtazamo hasi.
Anayejua tofauti za nauli Kati ya ATC na precision Air anisaidie mie ni mgeni hapa.
 
Maanake taasisi na mashirika yote ya serikali yatalazimishwa kununua mafuta Kutoka sheli zinazomilikiwa na serikali, Naliona anguko la sekta binafsi katika biashara hii.
 
Serikali na kufanya biashara!!Wacha tuone.
Kwenye biashara muhimu na nyeti kama umeme na nishati ya mafuta ni hatari ukategemea private companies kwa asilimia 100 na hasa kama kampuni hizo ni za nchi zingine. Tulishuhudia tulichokipata pale TANESCO na ATCL tulipowapa kampuni za Africa ya kusini na kadhalika. Tumeshuhudia licha ya bei ya mafuta ya petroli na dizeli kuteremka kwenye soko la dunia kwa sababu ya coronavirus kutoka USD 60 kwa pipa hadi USD 15 kwa pipa, sisi pamoja na EWURA yetu bei ya mafuta haya yalipungua kwa Tsh zisizozidi 100 tu kwa lita. Hii ni kwa sababu ya unyonyaji wa makampuni ya nje ya uagizaji na usambazaji wa mafuta haya hususani BP, Total, Camel etc. Sasa tutakuwa na TANOIL yetu wenyewe. Hatutaki kuchezewa chezewa tena.
 
Anayejua tofauti za nauli Kati ya ATC na precision Air anisaidie mie ni mgeni hapa.
Bei ya nauli ya precision air kutoka Dar hadi Mwanza kabla ya kufufuliwa kwa ATC ilifikia shilingi laki 8 kwenda tu. Baada ya kufufuka kwa ATCL nauli hiyo iliteremka hadi laki 2 tu au chini yake ili kuweza kushindana na bombadier za ATCL!
 
Huku wamiliki/shareholders wa vituo vingi ni hawahawa watendaji wa serikari! Wacha wawape mpenyo wajanja.
 
Bei ya nauli ya precision air kutoka Dar hadi Mwanza kabla ya kufufuliwa kwa ATC ilifikia shilingi laki 8 kwenda tu. Baada ya kufufuka kwa ATCL nauli hiyo iliteremka hadi laki 2 tu au chini yake ili kuweza kushindana na bombadier za ATCL!
Umesahau fastjet ilikuwa sh. Ngapi?
 
Sioni vipi sekta binafsi inaweza shindana na serikali. Yale yale ya FastJet kujirudia.. but all in all kwetu walaji wa mwisho inaweza kuwa nafuu... let's wait and see
Ni swala la muda tu,,wataua private sector then waenze kutupiga bei WANAOTAKA make watakua Hawana mshimdani
 
Umesahau fastjet ilikuwa sh. Ngapi?
Bei ya fast jet ilikuwa hivyo hivyo. Ilitokea Kenya kuja kushindana na precision air. Walitoa discount uki book mapema lakini mara nyingi discount hizo ulikuwa huwezi kuzipata maana mara nyingi utaambiwa discount hizo ziko kuanzia miezi 6 ijayo!
 
Sioni vipi sekta binafsi inaweza shindana na serikali. Yale yale ya FastJet kujirudia.. but all in all kwetu walaji wa mwisho inaweza kuwa nafuu... let's wait and see

Hakuna unafuu wowote utakaopata mkubwa...

Biashara ya nishati ya umeme 100% inaendeshwa na serikali, kuna unafuu wowote? Kuna ubora wowote wa huduma hiyo?

Jibu ni HAKUNA...!!

Kama ndivyo, huko ndiyo kushindwa kwenyewe hivyo kwa serikali kusimamia mambo...

Serikali inapaswa kuijengea mazingira wenzeshi sekta binafsi (private sector) kunawiri na yeye ijikite zaidi ktk kutoa huduma na si kufanya biashara...

Tukienda hivi tunaweza kurudi kulekule enzi za miaka 1985 kurudi nyuma...

Enzi za RTC, maduka ya kijiji au mtaa, foleni kununua sukari nk...

Sina hakika kama ulikuwa upo umezaliwa nyakati hizo. Kama ulikuwepo, basi kumbe wewe ni MHENGA pia...
 
Hata hvyo walichelewa sana kwenye hiyo biashara, sekta hii ya mafuta sio biashara ya kuyaachia makampuni ya nje tu coz lazma ujue athari ya mafuta iwapo yakikosekana au yakipanda bei mnavyojua kulalamika.
Ewuera kazi yao ni nini? Unajua kua wanafanya bulk procurement?
 
Sioni vipi sekta binafsi inaweza shindana na serikali. Yale yale ya FastJet kujirudia.. but all in all kwetu walaji wa mwisho inaweza kuwa nafuu... let's wait and see
Kama ambavyo kwenye Nauli za Usafiri wa Ndege wa ndani hakuna unafuu wowote...

Itakua the same kwa Mafutaa.

Kama vile Taasisi za Serikali zilivyokosa Ueledi, Mfano Dawasco, Tanesco n.k.
Ndo itavyokua pia kwa hiyo Taasisi ya Mafuta.
 
Bei ya fast jet ilikuwa hivyo hivyo. Ilitokea Kenya kuja kushindana na precision air. Walitoa discount uki book mapema lakini mara nyingi discount hizo ulikuwa huwezi kuzipata maana mara nyingi utaambiwa discount hizo ziko kuanzia miezi 6 ijayo!

FastJet haikuwa kampuni ya Kenya wala haikutokea Kenya.

Image https://centreforaviation.com › reports
Low-cost airlines start to penetrate African international market, led by fastjet | CAPA

22 Oct 2013 · It is the first of several planned international routes for fastjet from Tanzania and other potential new bases throughout Africa. Incredibly there
 
Mafuta sio biashara kama biashara nyingine.

Unapozungumzia mafuta unazungumzia national security ya nchi.

Mataifa yenye kuzalisha mafuta utakuta National Oil Companies (NOC) zao zina shiriki kwenye value chain zote kuanzia kwenye kutafuta mpaka retail and petrochemical industries too. Na nchi nyingi tu state companies zinauza retail ata kama awachimbi mafuta.

Na nchi zisizo shiriki basi zinashirikiana kimkakati na kampuni binafsi mfano hakuna mtu anaweza chimba mafuta North Sea upande wa UK zaidi ya Shell, ukichezea maslahi ya makampuni ya marekani USA hayo yanayoitwa private popote duniani subiri fujo za serikali yao. Ukienda India karibu makampuni yote ya mafuta shareholder ni serikali.

Kwa nchi kama Tanzania TPDC ushiriki wake kwenye energy security ni mdogo sana it’s about time waanze kufanya investment storage yenyewe ya nchi nzima sidhani kama inamudu mwezi wakati ushauri wa ‘International Energy Agency’ kila nchi inatakiwa walau iwe na uwezo wa kuweka akiba ya miezi mitatu.

Nani atawekeza kwenye hizo infrastructure zaidi ya TPDC na kama unajukumu hilo ni bora pia uuze mafuta upate kipato faida uwekeze kwenye infrastructure za mkakati.

Bado kuna swala la military strategies na mafuta.

In short biashara na umuhimu wa mafuta ulimwengu wa leo ni swala la kimkakati na ukikosea it could be very costly government have been toppled kwa sababu ya mafuta.

Upuuzi ni kusema TPDC ndio itakayokuwa inaagiza nusu ya mafuta yanayoingia nchini wao pekee au wakianza sabotage zingine za sector kama ilivyo adha kisa kukurupuka bila ya business plan.
 
Serikali na kufanya biashara!!Wacha tuone.
Daah!
Naona kama serikali inajibebesha majukumu mazito sana ambayo ilipswa kuyaacha yawe chini ya taasisi binafsi.

Labda wanaogopa kukosa udhibiti ikitokea migomo ya wauzaji mafuta kama kile kipindi cha Kikwete. Inaweza kuwa mikakati ya usalama wa nchi, ingawa bado hii sababu haina uzito.

Kama usalama wa nchi basi wao wangejikita kununua na kuweka hifadhi ya mafuta ghafi kama Marekani na nchi zingine zilizo endelea. Ukitokea mgomo au mfumuko wa bei ya mafuta inaachia mafuta yake ya akiba kuziba pengo.

Hivi vituo vya TANOIL ni kutengezeza mtambo wa upigaji na wa kuzalisha watuhumiwa wa uhujumu uchumi tu.
 
Back
Top Bottom