Hapana.mimi naona ni jambo zuri.
Maana faida itaenda hazina..
waache kutegemea kodi.
Wawe na vyanzo vya mapato..
Unadhani ni kitu gani kitatokea kwa uchumi wa Tanzania kutokana na uwezo wetu wa kuhifadhi mafuta iwapo Iran ikifanikiwa kuzuia meli yoyote kukatiza strait of Hormuz kwa muda wa miezi mitatu tu?vyanzo vya mapato kwa serikali vipo takribani vitatu na vipo kihalali kabisa I.e kodi,mikopo na misaada(grants).Serikali inapojiingiza directly kwenye business ni jambo ambalo halina afya kwa upande mmoja lakini nikiri kuwa faida ni kiduchu kwa last consumer.Serikali iweke mipango na mifumo mizuri ya kusimamia na kutengeneza mazingira mazuri kwa sekta binafsi ya ufanyaji biashara
About time, ila bado viwanda kama Tanganyika Packers, Textiles, madini, vya kilimo n.k. Tutafika tu...View attachment 1472096
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amezindua rasmi biashara ya kuuza na kusambaza mafuta nchini kwa kufungua kituo cha kwanza kuuza mafuta ya Petroli na Dizeli cha Serikali kitakachosimamiwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) kupitia Kampuni yake Tanzu ya Mafuta ( TANCOIL). Aidha Dkt. Kalemani alisema kuwa kuzinduliwa na kufunguliwa kwa biashara hiyo ni kutimiza azma na nia njema ya Serikali ya kuboresha shirika lake la TPDC,kuwapatia na kuwasogezea karibu wananchi wake huduma ya kupata mafuta yenye viwango vya ubora unaotakiwa, bei nafuu, na yatakayopatikana kwa wingi muda wote.
Dkt. Kalemani alifanya Uzinduzi huo pamoja na kufungua kituo hicho wilayani Musoma, mkoani Mara Juni 6, 2020, wakati wa ziara yake ya kikazi katika Mkoa huo, akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Zena Said pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Wizara hiyo na Taasisi zilizochini yake. Alisema baada ya kuanza rasmi kwa biashara hiyo, TPDC kupitia TANCOIL itashirikiana na Halmashauri zote nchini kuhakikisha inafanikisha azma ya Serikali ya kufungua na kuweka vituo vya kuuza na kusambaza mafuta katika kila halmashauri nchini pamoja na miundombinu ya kuhifadhi na kusafirisha mafuta.
Dkt. Kalemani aliwaeleza watanzania kuwa TPDC na TANOIL watashiriki katika biashara ya uagizaji na usambazaji mafuta kama zinavyofanya kampuni zingine za mafuta nchini ili kuongeza ushindani na kutanua wigo wa kampuni za kizalendo kushiriki katika biashara ya mafuta, ambayo kwa sasa inafanywa na makampuni kutoka nje ya nchi tu. Alisema kuwa serikali kupitia TPDC itajenga vituo 100 kwa kipindi cha miaka 5 ijayo, tayari baadhi ya Halmashauri zimeanza kutenga maeneo yatakayojengwa vituo hivyo: Aidha itahakikisha kuwa nusu ya mafuta yote yanayoingizwa nchini yanasimamiwa TPDC.
Kwenye biashara muhimu na nyeti kama umeme na nishati ya mafuta ni hatari ukategemea private companies kwa asilimia 100 na hasa kama kampuni hizo ni za nchi zingine. Tulishuhudia tulichokipata pale TANESCO na ATCL tulipowapa kampuni za Africa ya kusini na kadhalika. Tumeshuhudia licha ya bei ya mafuta ya petroli na dizeli kuteremka kwenye soko la dunia kwa sababu ya coronavirus kutoka USD 60 kwa pipa hadi USD 15 kwa pipa, sisi pamoja na EWURA yetu bei ya mafuta haya yalipungua kwa Tsh zisizozidi 100 tu kwa lita. Hii ni kwa sababu ya unyonyaji wa makampuni ya nje ya uagizaji na usambazaji wa mafuta haya hususani BP, Total, Camel etc. Sasa tutakuwa na TANOIL yetu wenyewe. Hatutaki kuchezewa chezewa tena.
Wasisahau kufufua kampuni ya mabasi KAMATA nchi nzima,,watu wanapiga hela sana hii sekta,,serikali inaachia pesa nyingi tu..[emoji58][emoji58]
Sioni vipi sekta binafsi inaweza shindana na serikali. Yale yale ya FastJet kujirudia.. but all in all kwetu walaji wa mwisho inaweza kuwa nafuu... let's wait and see
Hapana.mimi naona ni jambo zuri.
Maana faida itaenda hazina..
waache kutegemea kodi.
Wawe na vyanzo vya mapato..
Huna gari wewe ndio maana .........unapata wap ujasiri wa kuongea hakati huna gariTunajenga taifa hodhi la ajabu sana. Kupanga ni kuchagua, vituo vya mafuta ni pety buss kwa sasa wapo wajasiliamali wengi wadogo na wa kati. Endapo lipo swala la usalama bora serikali ingejipanga kuagiza bulk pekee.
Elimu yako please?
vyanzo vya mapato kwa serikali vipo takribani vitatu na vipo kihalali kabisa I.e kodi,mikopo na misaada(grants).Serikali inapojiingiza directly kwenye business ni jambo ambalo halina afya kwa upande mmoja lakini nikiri kuwa faida ni kiduchu kwa last consumer.Serikali iweke mipango na mifumo mizuri ya kusimamia na kutengeneza mazingira mazuri kwa sekta binafsi ya ufanyaji biashara
Ni ujinga serikali kujiingiza kwenye vibiashara