Serikali yaanza kuhujumu Mameya Dar es Salaam

Serikali yaanza kuhujumu Mameya Dar es Salaam

Nilifikiri awamu ya tano haitaendekeza siasa uchwara, Rais wetu alisema atakuwa raisi wa watu na vyama vyote. Kwa hiyo inawezekana hajui kinachoendelea huku chini. Katika mambo yanayoweza kuturudisha nyuma kiuchumi mojawapo ni kuendekeza siasa uchwara.. Tujaribu kuangalia Zanzibar na siasa zao.. Hapa kazi tu, maana yake hatuna longo longo za siasa...so sad
Rais angekuwa haendekezi siasa uchwara asingesema wapinzani ni watoto wa jirani (uzinduzi wa mtambo Kinyerezi II).

Kwa kauli ile Rais ndo kawafundisha Hawa wasaidizi wake wawaone wapinzani kama watoto wa jirani na kuwabagua.Siasa hizi zimeasisiwa na JPM
 
Hii ni aibu hasa kwa Simbachawene ambaye kesha onyesha dhahiri chuki zake kwa viongozi hao.
Lakini wanachoshindwa kujua ni kuwa ukimchukia Meya wa Dar umewachukia wananchi wa Dar. Waangalie Kule Arusha, walionyesha chuki ya wazi kabisa kwa Lema kilichofuata ni hata ule uhai mdogo wa ccm uliokuwepo wakaumalizia kabisa.
Hizi ni siasa za kishamba kabisa na kama bwana mkubwa anajua na kunyamaza ajue anajimaliza. Akikosa support ndani ya mji mkuu ndio kunalizika kwake, hao wakina Simbachawene na Makonda watanponza, hiyo Dar asijekuta anazomewa ikawa taabu bure!
 
Mameya nanyie muwe mnajiongeza, kila saa kulalamika tu!!

Kwanza wekeni mikakati yenu, kwani mnatambua vikwazo vilivyopo mbele yenu. Kwanza fanyeni haya:

1. Muwe wazi kwa wahisani wenu, weelezeni changamoto mnazo pitia, kwani CCM hawajazoea kushindwa ila sasa wameshindwa na wataendelea kushindwa!!

2. Technology ipo kwa sasa. Kwani ni lazima ww uende South Africa ndio hela ije Bongo? Huwezi kufanya Video Conference? Au hamjui ngeli kama mkulu?
Hamna official Email? Hamna formal communication systems with your donors? Huwezi tuma muakilishi kama kweli una nia ya msaada? Huwezi wasiliana na Ubalozi wa Tz kwa niaba na kumtaarifu donor wako?

2. Fukuzeni walinzi wote na PS wote ofisini kwenu au muwahamishie Ofisi za Wana CCM. Hawa ni waongo si mchezo, kila umbeya wanao, hawapitwi na kitu. Ajirini wenu wapya hasa wa Red-bridged.

3. Fanyeni kazi na media, tengeni hela za kuwahonga. Hawa nao kwa rushwa hawajambo!!
Tufuteni hujuma hizo na ni nani alie nyuma yake na video clip au voice clip, samabazeni kwa muda wa mwaka 1 , watahaibika na kukosa pa kujificha. Ila maneno bila ushahidi ni sawa na bure. YOU MUST SPEND MONEY! Nakumbuka zile Clip za Masaburi za kuandamana kuwa wanamtaka Dr. Slaa zimechangia sn yy kudharaulika na shindwa pia kiurahisi sn.

4. Siyo kila kitu uwe na kibali bhana inapo shindikana, kwani ulikuwa tiyari na tiketi na huduma zote ungehudhuria kama ww na si Meya!! Mf. Rais Mugabe alihudhuria Mazishi ya Papa kama mkatoliki na si Rais na hakukamatwa!! Sasa ww ni mwanasiasa Kibali cha nn? Ww nenda kama ww, wakizikataa hela Jenga kitega uchumi, ajiri vijana!!

Mm ni mtanzania kwenda Kenya hadi Magufuli afahamu?

Ushauri muwe munaomba mapema kabla ya kutukosesha hela!!
Umewaeleza vema Mameya wa upinzani wanapaswa kufahamu watafanyiwa figisu figisu za kila aina....... hiyo safari ya SA ilitakiwa uende ukapandie ndege Lusaka Zambia tambueni kwamba ni mapambano kwa kwenda mbele hakuna mtu atawavua umeya kienyeji siku nyingine msilete habari ya kulia lia
 
Meya unaposema uchaguzi umeisha mbona Wenzio Dodoma wanaendekeza siasa? au nyinyi pekee yenu mnajua vigisuvigisu?
 
Mameya nanyie muwe mnajiongeza, kila saa kulalamika tu!!

Kwanza wekeni mikakati yenu, kwani mnatambua vikwazo vilivyopo mbele yenu. Kwanza fanyeni haya:

1. Muwe wazi kwa wahisani wenu, weelezeni changamoto mnazo pitia, kwani CCM hawajazoea kushindwa ila sasa wameshindwa na wataendelea kushindwa!!

2. Technology ipo kwa sasa. Kwani ni lazima ww uende South Africa ndio hela ije Bongo? Huwezi kufanya Video Conference? Au hamjui ngeli kama mkulu?
Hamna official Email? Hamna formal communication systems with your donors? Huwezi tuma muakilishi kama kweli una nia ya msaada? Huwezi wasiliana na Ubalozi wa Tz kwa niaba na kumtaarifu donor wako?

2. Fukuzeni walinzi wote na PS wote ofisini kwenu au muwahamishie Ofisi za Wana CCM. Hawa ni waongo si mchezo, kila umbeya wanao, hawapitwi na kitu. Ajirini wenu wapya hasa wa Red-bridged.

3. Fanyeni kazi na media, tengeni hela za kuwahonga. Hawa nao kwa rushwa hawajambo!!
Tufuteni hujuma hizo na ni nani alie nyuma yake na video clip au voice clip, samabazeni kwa muda wa mwaka 1 , watahaibika na kukosa pa kujificha. Ila maneno bila ushahidi ni sawa na bure. YOU MUST SPEND MONEY! Nakumbuka zile Clip za Masaburi za kuandamana kuwa wanamtaka Dr. Slaa zimechangia sn yy kudharaulika na shindwa pia kiurahisi sn.

4. Siyo kila kitu uwe na kibali bhana inapo shindikana, kwani ulikuwa tiyari na tiketi na huduma zote ungehudhuria kama ww na si Meya!! Mf. Rais Mugabe alihudhuria Mazishi ya Papa kama mkatoliki na si Rais na hakukamatwa!! Sasa ww ni mwanasiasa Kibali cha nn? Ww nenda kama ww, wakizikataa hela Jenga kitega uchumi, ajiri vijana!!

Mm ni mtanzania kwenda Kenya hadi Magufuli afahamu?

Ushauri muwe munaomba mapema kabla ya kutukosesha hela!!
Umewaeleza vema Mameya wa upinzani wanapaswa kufahamu watafanyiwa figisu figisu za kila aina....... hiyo safari ya SA ilitakiwa uende ukapandie ndege Lusaka Zambia tambueni kwamba ni mapambano kwa kwenda mbele hakuna mtu atawavua umeya kienyeji siku nyingine msilete habari ya kulia lia
 
Hiyo sasa ni hiari ya muajiri wake kama anaona inafaa au haifai. BTW serikali hii ilijitanabisha kuwa haihitaji misaada.
Lakini ile ya China ilipokelewa kwa mikono miwili na yajuzi ya Marekani double standard
 
Mbunge wao amesema bungeni kwamba huu unaoitwa kubana matumizi itafika wakati wakati watanyanganywa magari wapewe baiskeli na ikulu ipangishwe rais akapange Mbagala.
Sijui ni nani aliyewaambia hawa watu nyumba zinazokula chakula duni kwa kisingizio cha kubana matumizi ndizo zinazojenga.
Uhalisia ni kwamba ndizo zinazodidimia na hata kufikia kiwango cha ubumbuazi wa kifikra. Hapo ndiko tunakoendea kama taifa ikiwa hatutajirekebisha ama hatutaacha kuweka hatma ya taifa juu ya kichwa cha mtu mmoja.
 
Inasikitisha mpaka unafikia kuwa meya kwa tiketi ya ukawa ulikuwa huijui ccm, pole sana
 
Lakini ile ya China ilipokelewa kwa mikono miwili na yajuzi ya Marekani double standard
Hizo wanaleta wenyewe ila hazifuatwi, wanajipendekeza wenyewe kuahidi. Hata za jamaa wangezileta nadhani kusingekuwa na tatizo.

Lakini mkuu shida ninayo ona hapa ni kuleta kibali late ilhali tarehe ya kusafiri imeandikwa kwenye form husika. Ni afadhali wangekataa kabisa kuliko uhuni waliomfanyia Meya
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SERIKALI YAANZA KUHUJUMU MAMEYA DSM

Habari za mchana huu ndugu waandishi wa habari na wananchi wote ndani ya Manispaa ya Kinondoni, awali ya yote nimshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutujalia pumzi na uhai mpaka leo hii, alikadhalika niwe miongoni mwa wengi tunaowatakia heri ndugu zetu Waislamu, katika mwezi huu Mtukufu wa tiba, mwenyezi Mungu awajalie heri na kuzisikia funga ziwe zenye Baraka kwao na jamii kwa ujumla.

Baada ya kutoa utangulizi huo, ndugu zangu waandishi wa habari na wananchi wa Kinondoni, sio kawaida yangu kuongea habari zinazohusu Serikali Kuu, kwa kuwa ninaamini kuwa Maendeleo ya Wananchi wa Mkoa huu wa Dar es salaam na Wilaya ya Kinondoni, hayawezi kuletwa kwa ubinafsi wa viongozi, bali ushirikiano mwema ya sisi tuliopewa dhamana ya kuziongoza Halmashauri kutoka vyama vinavyounda UKAWA, na CCM wanaounda Serikali Kuu. Jambo hili hufanya tuwe kimya na wavumilivu mara nyingi sana, ingawa bado kuna mahusiano ya kutia shaka kila kukicha.

Ila leo ndugu zetu waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla, tumeamua kuandika na kufikisha ujumbe huu kwenu, ili mjue yalipofikia kama viongozi na Serikali Kuu na mabaya yanayoendelea na ya kusikitisha sana.

Na kusema huku, tutafanya viongozi wakuu wa nchi kama walikuwa hawajui wajue au walitoa baraka hizi, basi sawa watusikie masikitiko yetu haya, kwa kuwa tulikuwa na imani nao sana na bado tutaendelea kuwa na imani nao kama Serikali juu ya kutatua changamoto na matatizo ya Wananchi.

Hali ya kimahusiano kati ya Mameya wanaotokana na UKAWA na Serikali Kuu si mazuri hata kidogo, viongozi tumeamua tuhabarishe umma wa Watanzania kuwa kuna hujuma za waziwazi zinazofanywa na wenzetu juu ya shughuli za Mameya wa Kinondoni, Ilala na Jiji la Dar es salaam.

Si mara ya kwanza hii kwa sisi Mameya kuhisi kuhujumiwa na baadhi ya viongozi serikalini ambao kimsingi, sisi tuliamini uchaguzi umeshapita na kwamba kila mmoja wetu atampa mwenzake heshima inayostahili juu ya ajenda za Maendeleo, ndiyo maana kama nilivyo sema hapo awali, tumekuwa kimya juu ya vikwazo vidogo vidogo ambavyo tulihisi ni hujuma lakini tukaamua kuwa kimya na wavumilivu lakini tunatambua kuwa ipo mikakati ovu mingi dhidi yetu, ya kutukwamisha tusifanikiwe kuleta Maendeleo ndani ya Mkoa wetu na Wilaya zetu, hata tulipo amua kuvumilia uchokozi wa wawaziwazi wa kejeli za kutishia kunyang'anya Mameya magari na vinginevyo, kutoka kwa mtu tunaye muheshimu kama Waziri wa TAMISEMI ofisi ya Rais, akidai wakurugenzi watupore magari tena mbele ya vyombo vya habari.

Ila sasa hujuma zimefika mahali pabaya kiasi kwamba kutukwamisha kupata misaada ya Maendeleo kutoka kwa nchi rafiki na Halmashauri zilizopo Dar es salaam.

Binafsi Manispaa ya Kinondoni nilishawahi kunyimwa ruhusa nisisafiri kwenda nchini Afrika ya Kusini nilipokuwa nimealikwa na wahisani waliotaka kunifadhili kutengeneza mto Mlalakuwa, uliokuwa utengenezwe kingo zake kuanzia Goba,Makongo juu mpaka Kata ya Kawe kuelekea baharini, wafadhili hao ni ICLEI-local government sustainability, mradi ambao ulikuwa unafanyika nchi nyingi za Afrika.

Mbali nakuwa wafadhili walikubali kulipia usafiri,malazi na gharama zote za kongamano lililokuwa lifanyike huko Afrika Kusini, nchi zote zilifika katika kongamano la CIP AIRR, lakini uwakilishi wetu ulikosekana kwa kisingizio cha ruhusa kutopatikana, madhara yake Manispaa ya Kinondoni ikaondolewa kwenye programu ya kufadhiliwa huku nchi kama Ghana,Kenya,Zambia na nyinginezo zikifadhiliwa. Baada ya mkutano kuisha nchini Afrika Kusini, Katibu Mkuu kiongozi akaniandikia kibali cha kusafiri, baada ya kongamano kuisha na kukosa kiasi cha tshs Bilioni 1.3.

Kubwa lilofanya kuwatarifu nyinyi na umma juu ya hujuma hizi ni kitendo cha juzi alfajiri. Tukiwa tayari uwanja wa ndege kuanza safari ya mualiko wa kwenda nchini uturuki, ulio andaliwa na kufadhiliwa na ubalozi wa uturuki nchini Tanzania kwa ajili ya kukamilisha maongezi yaliyokwisha anza hapa Dar es salaam juu ya kusaidia kutatua chngamoto za ajira za vijana kwa miradi endelevu; ikiwemo mpango wa ujenzi wa chuo cha ufundi stadi kwa udhamini wa ubalozi wa uturuki,kupitia wafadhili wake.

Ubalozi wa Uturuki ulikuwa umedhamini safari ya Mameya kwenda Uturuki kukutana na wadau na wafadhili wa miradi mbalimbali ikiwemo ikiwemo Chuo Cha Ufundi ndani ya Manispaa ya Kinondoni, Ubalozi huo ulikuwa umeshatoa kibali cha kusafiri (Visa) na kugharamia fedha za usafiri, malazi, chakula na gharama zingine zote, ambapo matayarisho tu yali gharimu kiasi cha dola za kimarekani 42,000/=,sawa na shillingi millioni 88,kwa mameya wote wanne na mtendaji mmoja mmoja kutoka kila Halmashauri.

Safari pamoja na mkutano vilitakiwa kuanza tarehe 16 june mpaka 19 june 2016,huku wafadhili na wadau wetu wa maendeleo wakiandaa mialiko na wawekezaji na wafadhili kutoka sehemu mbali mbali za uturuki,kuja makao makuu ya nvhi hiyo,jiji la instanbul ulitarajiwa lakini Serikali imevunja Safari hiyo.

Kwa kufanya hivi Serikali imezikosesha Manispaa zetu fursa za Maendeleo ikiwemo Chuo hicho cha ufundi.

*Msimamo* wetu kwenye hili suala ni kutaka kujua:

• Je huo ndio msimamo rasmi wa viongozi wote wa serikali,?

• Tungependa kusikia Tamko kutoka kwa Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kama maagizo haya ya kubana fedha na matumizi ya serikali yanahusianaje na safari za kufadhiliwa na nchi wahisani?

• Je hakuna namna ya kushirikiana na nchi rafiki kutupatia miradi ya Maendeleo?

Mwisho nimalizie kwa kusema sisi bado tuna imani ya kwamba hujuma hizi Mheshimiwa Rais hazifahamu ila isipokuwa baadhi ya viongozi wa serkali wanajaribu kuweka tafsiri tofauti ya sera ya kuzuia matumizi mabaya ya fedha kwenye safari za nje ya nchi.

Pamoja na kutumia vibaya agizo la Mheshimiwa Rais kuruhusu vibali vya viongozi katika mamlaka mbalimbali za serikali, Sisi tuna amini kuwa agizo la kuomba kibali maalumu ikulu halituhusu sisi (kama viongozi tusio watendaji), wala kutumia bajeti za serikali au halmashauri zetu kwenda kuonana na wadau wamaendeleo.

IMETOLEWA NA MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA KINONDONI.

BONIFACE JACOB.
IJUMAA 17/06/2016
 
wewe ukisubili ruhusa itakula kwako,kama pesa yote ya safali watatoa wao siku nyingine,we nenda tu maana hawato kuvua umeya
Tiketi sio ya serikali, pesa ya malazi sio ya serikali, viza unayo unaomba kibali cha nini wakati wewe si mwajiriwa wa serikali we ni kutoa taarifa tu ya safari, panda ndege leta maendeleo lawama badae.
 
Kama haya maelezo ni ya kweli, na kama kweli kuna hujuma anayefanya hizo hujuma ajue anawahujumu wananchi waliokuchagueni na ataadhibiwa kwenye sanduku la Kura 2020 na pia ataadhibiwa na mwenyezi mungu maana sauti ya wengi ni sauti ya mungu.
 
Wananchi Gani unaosema wewe hawa wanaorukaruka Majipu yanatumbuliwa lkn Sukari Kilo elf6
Yaani basi tu. Wakati mwingine najuta kuzaliwa kwenye nchi yenye watu maprimitive kama hii Najisikia km am in a wrong place! Mh rais anasema kila siku tusibaguane kumbe ni maneno tu?
 
Huyu asilalamike kutafuta kick. Kwa anatekeleza sera za CCM au za CHADEMA-UKAWA?

Maana walisema watafanya bila serikali kwa kushika manispaa tu. Kama watategemea serikali waandike maumivu.
 
Mkuu kwa watumishi wa umma..tena hawa wa ngazi za juu...pale airport bila kibali hawakuruhusu kusafiri. Wapo waliozuiliwa hata kwa safari binafsi ila wameogopa kusema wazi..nyumba zao zisije zikazingirwa na polisi.
Kwani mkuu lazima wapandie ndege Dar? Si wanaweza kwenda hata kupandia Nairobi? Basi kama wanazuiliwa hata kwenda nchi jirani tutakuwa na shida na uongozi wetu huu!!
 
Back
Top Bottom