Serikali yaanza kuhujumu Mameya Dar es Salaam

Serikali yaanza kuhujumu Mameya Dar es Salaam

Usimbane sana na wewe ungezama kidogo. Serikali imenizuia, Ilipaswa nicommunicate hizi changes kwa mfadhili mapema na kumpa hii option ya teleconference kama inawezekana maana kama mtu ameamua kukusaidia na ukamueleza uhalisia na ikibidi ukampa contact za uhakika kujilidhisha, Nio hiyohiyo ya kutaka niudhulie anaweza kuihamishia kwenye kuongeza option ya Teleconference. Ndio maana jamaa anataka kujua huyu meya alistruggle vipi kutafuta alternative au alikata tamaa na kusubili kutoa tamko. Lazima atueleze na initiative zake alizofanya na ikibidi ushahidi wa maandishi/emails/barua

Kumbuka kulikua na nchi nyingi zinahitaji huo msaada..sio Tanzania tu. Sasa mfadhili amesema ana 1.3B za kuipatia kinondoni...kamwambia meya aje tena kwa gharama za huyo mfadhili ili waweke mambo sawa na wasign mikataba. Meya anamwambia eti "sitaweza kuja kwasababu ikuku haijaniruhusu...hebu nenda mahali utafute teleconference"...hivi hata kama mfadhili ni wewe si utaona ni upuuzi? Nchi gani ambayo inahitaji hizo hela itafanya hivyo? Ndio maana mfadhili kaona hela zake awape zimbabwe na nchi zingine ambazo ziko proactive. Yani hii ban ya kusafiri itatucost sana mkuu
 
Kuna kitu sijaelewa,amri yakutosafiri inawagusa namna gani?nilidhani ni watumishi wa serekali tu na haiwahusu wanasiasa kama diwani na wabunge.

Mkuu hii amri kwakweli inabidi ikulu waiweke vizuri. Airport pale wamezuiliwa watu wengi wa kisiasa...wanaogopa tu kusema wazi wazi maana siku hizi ukionekana unakosoa...sirro anakufuata
 
Huu uchama utazidi kuendelea kuididimiza hii nchi! Kama Raisi alihusika kwenye Hujuma hii kuwakosesha wananchi maendeleo kwa makusudi basi nae atakua klz wa aina yake. Ila siamini kama alihusika. Siasa za uchama wasubiri uchaguzi kwengine sahivi tunataka maendeleo. Tumbua watu kama hao kwenye serikali yako Magufuli watakuharibia sana kwamanufaa ya matumbo yao.
 
Nimepandwa na hasira sana. Sijui nisemeje!Hebu waambieni wananchi kws sauti kubwa ili ijulikane hii serikali haijitambui. Yunajikosedha pesa hivihivi kwa sababu za kijinga. Hivi kweli Magufuli anaruhusu upuuzi huu? Ofisi ya rais inahusuka kuhujumu maendeleo ya wananchi? Mbona aibu hii?
Wananchi Gani unaosema wewe hawa wanaorukaruka Majipu yanatumbuliwa lkn Sukari Kilo elf6
 
Mwenyekiti wa chama alikiri hadharani Ukawa mmeiumiza ccm kwenye uchaguzi uliopita kwa Mara ya kwanza nilishuhudia mgombea urais anapiga push up jukwaani, awaache tu mje mumsumbue tu 2020
 
Magufuli anaendekeza sera za hovyo hovyo! Hata kule Mwanza kafuta UMISETA kwa wanafunzi kwa kisingizio cha madawati! Mawazo ya kimasikini kabisa!! Magufuli hafai kuwa kiongozi mkuu wa nchi! Hana dira wala malengo.
Mizuka ni mingi sana nchi hii
 
Akisema kitu tarajia kinyume chake
Kila kitu kina baraka kutoka juu! Sio hujuma za siri, ni mpango mahususi kufifisha wapinzani. Hii nchi ina viongozi wa ajabu mno! Inasikitisha mno kuwa raisi wetu alikiri kuwa atakuwa ni wawatz wote ila haya yanatokea! Kama ikulu ndo inatoa kibali, basi hata hili atakua alilijua.
Serikali iwe na huruma kwa watu wake!

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Mlipoambiwa hakuna safari mlifikiri linamuhusu nani?
 
Usimbane sana na wewe ungezama kidogo. Serikali imenizuia, Ilipaswa nicommunicate hizi changes kwa mfadhili mapema na kumpa hii option ya teleconference kama inawezekana maana kama mtu ameamua kukusaidia na ukamueleza uhalisia na ikibidi ukampa contact za uhakika kujilidhisha, Nio hiyohiyo ya kutaka niudhulie anaweza kuihamishia kwenye kuongeza option ya Teleconference. Ndio maana jamaa anataka kujua huyu meya alistruggle vipi kutafuta alternative au alikata tamaa na kusubili kutoa tamko. Lazima atueleze na initiative zake alizofanya na ikibidi ushahidi wa maandishi/emails/barua
Nashukuru mkuu. Naona watu wanachemka tu. Hawataki kufikiri
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SERIKALI YAANZA KUHUJUMU MAMEYA DSM

Habari za mchana ndugu waandishi wa habari na wananchi wote ndani ya Manispaa ya Kinondoni, awali ya yote nimshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutujalia pumzi na uhai mpaka leo hii, alikadhalika niwe miongoni mwa wengi tunaowatakia heri ndugu zetu Waislamu, katika mwezi huu Mtukufu wa tiba, mwenyezi Mungu awajalie heri na kuzisikia funga ziwe zenye Baraka kwao na jamii kwa ujumla.

Baada ya kutoa utangulizi huo, ndugu zangu waandishi wa habari na wananchi wa Kinondoni, sio kawaida yangu kuongea habari zinazohusu Serikali Kuu, kwa kuwa ninaamini kuwa Maendeleo ya Wananchi wa Mkoa huu wa Dar es salaam na Wilaya ya Kinondoni, hayawezi kuletwa kwa ubinafsi wa viongozi, bali ushirikiano mwema ya sisi tuliopewa dhamana ya kuziongoza Halmashauri kutoka vyama vinavyounda UKAWA, na CCM wanaounda Serikali Kuu. Jambo hili hufanya tuwe kimya na wavumilivu mara nyingi sana, ingawa bado kuna mahusiano ya kutia shaka kila kukicha.

Ila leo ndugu zetu waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla, tumeamua kuandika na kufikisha ujumbe huu kwenu, ili mjue yalipofikia kama viongozi na Serikali Kuu na mabaya yanayoendelea na ya kusikitisha sana.

Na kusema huku, tutafanya viongozi wakuu wa nchi kama walikuwa hawajui wajue au walitoa baraka hizi, basi sawa watusikie masikitiko yetu haya, kwa kuwa tulikuwa na imani nao sana na bado tutaendelea kuwa na imani nao kama Serikali juu ya kutatua changamoto na matatizo ya Wananchi.

Hali ya kimahusiano kati ya Mameya wanaotokana na UKAWA na Serikali Kuu si mazuri hata kidogo, viongozi tumeamua tuhabarishe umma wa Watanzania kuwa kuna hujuma za waziwazi zinazofanywa na wenzetu juu ya shughuli za Mameya wa Kinondoni, Ilala na Jiji la Dar es salaam.

Si mara ya kwanza hii kwa sisi Mameya kuhisi kuhujumiwa na baadhi ya viongozi serikalini ambao kimsingi, sisi tuliamini uchaguzi umeshapita na kwamba kila mmoja wetu atampa mwenzake heshima inayostahili juu ya ajenda za Maendeleo, ndiyo maana kama nilivyo sema hapo awali, tumekuwa kimya juu ya vikwazo vidogo vidogo ambavyo tulihisi ni hujuma lakini tukaamua kuwa kimya na wavumilivu lakini tunatambua kuwa ipo mikakati ovu mingi dhidi yetu, ya kutukwamisha tusifanikiwe kuleta Maendeleo ndani ya Mkoa wetu na Wilaya zetu, hata tulipo amua kuvumilia uchokozi wa wawaziwazi wa kejeli za kutishia kunyang'anya Mameya magari na vinginevyo, kutoka kwa mtu tunaye muheshimu kama Waziri wa TAMISEMI ofisi ya Rais, akidai wakurugenzi watupore magari tena mbele ya vyombo vya habari.

Ila sasa hujuma zimefika mahali pabaya kiasi kwamba kutukwamisha kupata misaada ya Maendeleo kutoka kwa nchi rafiki na Halmashauri zilizopo Dar es salaam.

Binafsi Manispaa ya Kinondoni nilishawahi kunyimwa ruhusa nisisafiri kwenda nchini Afrika ya Kusini nilipokuwa nimealikwa na wahisani waliotaka kunifadhili kutengeneza mto Mlalakuwa, uliokuwa utengenezwe kingo zake kuanzia Goba,Makongo juu mpaka Kata ya Kawe kuelekea baharini, wafadhili hao ni ICLEI-local government sustainability, mradi ambao ulikuwa unafanyika nchi nyingi za Afrika.

Mbali nakuwa wafadhili walikubali kulipia usafiri,malazi na gharama zote za kongamano lililokuwa lifanyike huko Afrika Kusini, nchi zote zilifika katika kongamano la CIP AIRR, lakini uwakilishi wetu ulikosekana kwa kisingizio cha ruhusa kutopatikana, madhara yake Manispaa ya Kinondoni ikaondolewa kwenye programu ya kufadhiliwa huku nchi kama Ghana,Kenya,Zambia na nyinginezo zikifadhiliwa. Baada ya mkutano kuisha nchini Afrika Kusini, Katibu Mkuu kiongozi akaniandikia kibali cha kusafiri, baada ya kongamano kuisha na kukosa kiasi cha tshs Bilioni 1.3.

Pamoja na hayo, Ubalozi wa Uturuki ulikuwa umedhamini safari ya Mameya kwenda Uturuki kukutana na wadau na wafadhili wa miradi mbalimbali ikiwemo ikiwemo Chuo Cha Ufundi ndani ya Manispaa ya Kinondoni, Ubalozi huo ulikuwa umeshatoa kibali cha kusafiri (Visa) lakini Serikali imevunja Safari hiyo.

Kwa kufanya hivi Serikali imezikosesha Manispaa zetu fursa za Maendeleo ikiwemo Chuo hicho cha Ufundi.

IMETOLEWA NA MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA KINONDONI:

BONIFACE JACOB.
IJUMAA 17/06/2016
Kama Rais anajua na kufumbia macho huu upuuzi
Nimekata tamaa
 
Wakuu msinikamie sana. Kwa maelezo ya Meya ni wazi kuwa kafanya jitihada za kutosha kuona ni jinsi gani anaweza kuhudhuria huko alikoalikwa lakini serikali imewazuia kwa namna yoyote. Kama wafadhili walidhamiria kusaidia hawawezi kutumia njia nyingine? Kama kina Meya waliweza kuwashawishi wafadhili hadi wakafikia hatua ya kuwatumia nauli, kwani hawawezi kutumia njia nyingine kuwashawishi na hela zikafika sehemu lengwa? Pia tusiimbe sana wafadhili tukasahau nguvukazi zetu wenyewe. Huyo Rais mwenyewe keshasema nchi hii inaweza kujiendesha. Upinzani uhakikishe wanapambana kuhakikisha ukusanyaji wa mapato kwenye halmashauri zao unarudi kwao na si kwenda TRA. Watu wakililia safari na wafadhili wakasahau wanaporwa hela huku nyuma itakuwa ni tatizo. Msinielewe vibaya. Tunapanuana tu mawazo
 
Kumbuka kulikua na nchi nyingi zinahitaji huo msaada..sio Tanzania tu. Sasa mfadhili amesema ana 1.3B za kuipatia kinondoni...kamwambia meya aje tena kwa gharama za huyo mfadhili ili waweke mambo sawa na wasign mikataba. Meya anamwambia eti "sitaweza kuja kwasababu ikuku haijaniruhusu...hebu nenda mahali utafute teleconference"...hivi hata kama mfadhili ni wewe si utaona ni upuuzi? Nchi gani ambayo inahitaji hizo hela itafanya hivyo? Ndio maana mfadhili kaona hela zake awape zimbabwe na nchi zingine ambazo ziko proactive. Yani hii ban ya kusafiri itatucost sana mkuu
Nimeifuatilia japo kwa juujuu ishu sio tu kupata hizo fdha zinazotolewa na mfadhili (European Union’s Horizon 2020 Research and Innovation Programme), pia kuna knowledge exchange maana mnakutana watu wa mataifa na majiji mbalimbali,
Sasa inaonyesha watu waliotakiwa kuhudhulia ni Mameya wa afrika, watu wa serikali za mitaa, na watu wengine wakiwemo taasisi na wanataaruma wa mambo ya maji,mafuriko etc.
Pia mkutano huo sio wa mwisho inaonekana itaendelea kuwepo, Anapaswa kuwa makini maana next time mameya wa majiji kama mwanza wanaweza kuomba na wao kupewa kipaumbele au wa manispaa nyingine ikawa kama ishu ya wabunge wale wa mambo ya ukimwi kwenda marekani.

Lakini ni makosa kufanya maamuzi ya kulaumu upande mmoja bila kujua kwa nini hakupewa kibali/kutoka kwa wahusika. pili ni kweli kulikuwa na huo msaada. Kufanya maamuzi kutoka kwa source mmoja ya mlalamikaji pia sio maamuzi yakiweredi mkuu
 
Meya naye aache ushamba, kwani angeenda bila kibali angefukuzwa kazi? Kibali ni utaratibu wa juzi tu unaowahusu waajiriwa wa serikali
Usidhani huyo meya analalama bure...ngoja nikuelimishe ni kwamba akienda nje ya nchi anapewa posho na Halmashauri yake 'per DM' iko palepale labda ambacho hawampi ni nauli...

Hao mameya wamekosa posho nono za kwenda nje ya nchi ndio maana wanalialia...Halmashauri kwasasa mkakati wake ni kujenga madarasa mazuri na kukamilisha ujenzi wa madawati na sio kulipa watu posho...
 
Duh... Hizi Thread ni za kutufanya kupata chuki...
 
Poleni sana Makamanda na wananchi wa Manispaa zinazoongozwa na UKAWA.tuunganishe nguvu kupinga udharimu huu
 
Kwan mameya mna serikali yenu tofauti na hii ya jamhuri?
 
Back
Top Bottom