Serikali yaanza kuhujumu Mameya Dar es Salaam

Serikali yaanza kuhujumu Mameya Dar es Salaam

Ndio siasa zetu meya acha kulalamika, kila upande ukifanya kitu hakipati sapoti Kutoka upande mwingine,ccm ikifanya kizuri mnaponda na hamkisapoti inafikia kipindi mnataka mpaka raisi hashindwe, ili mradi mpate kuongea ktk majukwaa yenu, ukija upande wa ccm nao hivyo hivyo hawasapoti upande wa upinzani, ndio serikali yetu, yaani huu chizi, tunauendekeza mpaka mtu ana mtukana rais mnaona sawa mpaka nyinyi chadema mnachangishana kampa ela ya kulipa faini, kwa hiyo mbwana meya asilalamike serikali hii NI YAKUONYESHANA NA KUTUNISHIANA MISULI NA SI YA KUSHIRIKIANA KATI YA UPINZANI NA SERIKALI.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SERIKALI YAANZA KUHUJUMU MAMEYA DSM

Habari za mchana huu ndugu waandishi wa habari na wananchi wote ndani ya Manispaa ya Kinondoni, awali ya yote nimshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutujalia pumzi na uhai mpaka leo hii, alikadhalika niwe miongoni mwa wengi tunaowatakia heri ndugu zetu Waislamu, katika mwezi huu Mtukufu wa tiba, mwenyezi Mungu awajalie heri na kuzisikia funga ziwe zenye Baraka kwao na jamii kwa ujumla.

Baada ya kutoa utangulizi huo, ndugu zangu waandishi wa habari na wananchi wa Kinondoni, sio kawaida yangu kuongea habari zinazohusu Serikali Kuu, kwa kuwa ninaamini kuwa Maendeleo ya Wananchi wa Mkoa huu wa Dar es salaam na Wilaya ya Kinondoni, hayawezi kuletwa kwa ubinafsi wa viongozi, bali ushirikiano mwema ya sisi tuliopewa dhamana ya kuziongoza Halmashauri kutoka vyama vinavyounda UKAWA, na CCM wanaounda Serikali Kuu. Jambo hili hufanya tuwe kimya na wavumilivu mara nyingi sana, ingawa bado kuna mahusiano ya kutia shaka kila kukicha.

Ila leo ndugu zetu waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla, tumeamua kuandika na kufikisha ujumbe huu kwenu, ili mjue yalipofikia kama viongozi na Serikali Kuu na mabaya yanayoendelea na ya kusikitisha sana.

Na kusema huku, tutafanya viongozi wakuu wa nchi kama walikuwa hawajui wajue au walitoa baraka hizi, basi sawa watusikie masikitiko yetu haya, kwa kuwa tulikuwa na imani nao sana na bado tutaendelea kuwa na imani nao kama Serikali juu ya kutatua changamoto na matatizo ya Wananchi.

Hali ya kimahusiano kati ya Mameya wanaotokana na UKAWA na Serikali Kuu si mazuri hata kidogo, viongozi tumeamua tuhabarishe umma wa Watanzania kuwa kuna hujuma za waziwazi zinazofanywa na wenzetu juu ya shughuli za Mameya wa Kinondoni, Ilala na Jiji la Dar es salaam.

Si mara ya kwanza hii kwa sisi Mameya kuhisi kuhujumiwa na baadhi ya viongozi serikalini ambao kimsingi, sisi tuliamini uchaguzi umeshapita na kwamba kila mmoja wetu atampa mwenzake heshima inayostahili juu ya ajenda za Maendeleo, ndiyo maana kama nilivyo sema hapo awali, tumekuwa kimya juu ya vikwazo vidogo vidogo ambavyo tulihisi ni hujuma lakini tukaamua kuwa kimya na wavumilivu lakini tunatambua kuwa ipo mikakati ovu mingi dhidi yetu, ya kutukwamisha tusifanikiwe kuleta Maendeleo ndani ya Mkoa wetu na Wilaya zetu, hata tulipo amua kuvumilia uchokozi wa wawaziwazi wa kejeli za kutishia kunyang'anya Mameya magari na vinginevyo, kutoka kwa mtu tunaye muheshimu kama Waziri wa TAMISEMI ofisi ya Rais, akidai wakurugenzi watupore magari tena mbele ya vyombo vya habari.

Ila sasa hujuma zimefika mahali pabaya kiasi kwamba kutukwamisha kupata misaada ya Maendeleo kutoka kwa nchi rafiki na Halmashauri zilizopo Dar es salaam.

Binafsi Manispaa ya Kinondoni nilishawahi kunyimwa ruhusa nisisafiri kwenda nchini Afrika ya Kusini nilipokuwa nimealikwa na wahisani waliotaka kunifadhili kutengeneza mto Mlalakuwa, uliokuwa utengenezwe kingo zake kuanzia Goba,Makongo juu mpaka Kata ya Kawe kuelekea baharini, wafadhili hao ni ICLEI-local government sustainability, mradi ambao ulikuwa unafanyika nchi nyingi za Afrika.

Mbali nakuwa wafadhili walikubali kulipia usafiri,malazi na gharama zote za kongamano lililokuwa lifanyike huko Afrika Kusini, nchi zote zilifika katika kongamano la CIP AIRR, lakini uwakilishi wetu ulikosekana kwa kisingizio cha ruhusa kutopatikana, madhara yake Manispaa ya Kinondoni ikaondolewa kwenye programu ya kufadhiliwa huku nchi kama Ghana,Kenya,Zambia na nyinginezo zikifadhiliwa. Baada ya mkutano kuisha nchini Afrika Kusini, Katibu Mkuu kiongozi akaniandikia kibali cha kusafiri, baada ya kongamano kuisha na kukosa kiasi cha tshs Bilioni 1.3.

Kubwa lilofanya kuwatarifu nyinyi na umma juu ya hujuma hizi ni kitendo cha juzi alfajiri. Tukiwa tayari uwanja wa ndege kuanza safari ya mualiko wa kwenda nchini uturuki, ulio andaliwa na kufadhiliwa na ubalozi wa uturuki nchini Tanzania kwa ajili ya kukamilisha maongezi yaliyokwisha anza hapa Dar es salaam juu ya kusaidia kutatua chngamoto za ajira za vijana kwa miradi endelevu; ikiwemo mpango wa ujenzi wa chuo cha ufundi stadi kwa udhamini wa ubalozi wa uturuki,kupitia wafadhili wake.

Ubalozi wa Uturuki ulikuwa umedhamini safari ya Mameya kwenda Uturuki kukutana na wadau na wafadhili wa miradi mbalimbali ikiwemo ikiwemo Chuo Cha Ufundi ndani ya Manispaa ya Kinondoni, Ubalozi huo ulikuwa umeshatoa kibali cha kusafiri (Visa) na kugharamia fedha za usafiri, malazi, chakula na gharama zingine zote, ambapo matayarisho tu yali gharimu kiasi cha dola za kimarekani 42,000/=,sawa na shillingi millioni 88,kwa mameya wote wanne na mtendaji mmoja mmoja kutoka kila Halmashauri.

Safari pamoja na mkutano vilitakiwa kuanza tarehe 16 june mpaka 19 june 2016,huku wafadhili na wadau wetu wa maendeleo wakiandaa mialiko na wawekezaji na wafadhili kutoka sehemu mbali mbali za uturuki,kuja makao makuu ya nvhi hiyo,jiji la instanbul ulitarajiwa lakini Serikali imevunja Safari hiyo.

Kwa kufanya hivi Serikali imezikosesha Manispaa zetu fursa za Maendeleo ikiwemo Chuo hicho cha ufundi.

*Msimamo* wetu kwenye hili suala ni kutaka kujua:

• Je huo ndio msimamo rasmi wa viongozi wote wa serikali,?

• Tungependa kusikia Tamko kutoka kwa Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kama maagizo haya ya kubana fedha na matumizi ya serikali yanahusianaje na safari za kufadhiliwa na nchi wahisani?

• Je hakuna namna ya kushirikiana na nchi rafiki kutupatia miradi ya Maendeleo?

Mwisho nimalizie kwa kusema sisi bado tuna imani ya kwamba hujuma hizi Mheshimiwa Rais hazifahamu ila isipokuwa baadhi ya viongozi wa serkali wanajaribu kuweka tafsiri tofauti ya sera ya kuzuia matumizi mabaya ya fedha kwenye safari za nje ya nchi.

Pamoja na kutumia vibaya agizo la Mheshimiwa Rais kuruhusu vibali vya viongozi katika mamlaka mbalimbali za serikali, Sisi tuna amini kuwa agizo la kuomba kibali maalumu ikulu halituhusu sisi (kama viongozi tusio watendaji), wala kutumia bajeti za serikali au halmashauri zetu kwenda kuonana na wadau wamaendeleo.

IMETOLEWA NA MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA KINONDONI.

BONIFACE JACOB.
IJUMAA 17/06/2016
Hayo ni madhara ya kuleta mambo ya kisiasa ndani ya kazi.inatakiwa wote muwe kitu kimoja ili maendeleo yapatikane kwa manufaa ya wananchi wote.
 
KWANZA TAARIFA YAKO IMENIUMIZA SANA MOYO WANGU KWANI INATUHUSU SISI WANANCHI.Mhe. kwa hili hebu tupate uthibitisho kwa kutafuta appoint wewe pamoja na Viongozi wenzako kufika Ikilu na kumueleza Rais hujuma hii na majibu yake ndiyo yatawapa mwanga kuwa ni wale wale au ni hujuma za vingozi wa ngazi za chini japo kuwa tamko la kuzuia safari za nje yeye Rais ndiye aliye litoa kuwa ni lazima patolewe kibali au ruhusa na sii kuwazuia kwenda nje ya nchi hasa tena kwa manufa ya Taifa.

Na hakika hao wanao fanya hizi hujuma Mungu kawalaani kwa kuwanyima maarifa kwani hawawakomoi ninyi viongozi bali wanatukomoa sisi wananchi kwa kukosa huduma za msingi kwa kusaidiwa na Wahisani ambapo nchi yetu ulishindwa kuwekewa misingi ya kujitegemea pamoja na kuwa na Rasimali zote na kubarikiwa na Mungu kuwa na asali na maziwa lakini viongozi walishindwa na wanashindwa kuzitumia badala yake ni siasa za kipuuzi tu kuziendeleza.

Hakika endapo Viongozi wetu hawato badilika kuna uwezekano mkubwa kwenda kulitumbukiza Taifa ktk Majanga makubwa sana na wao pia hawatokuwa salama na familia zao...na hata kwa Mungu pia hawatojificha au kutumia vyeo vyao na Pesa zao kujinusuru.Taifa hili ni letu sote na si la watu flani hasa wenye upeo mdogo wa kufikiri tu, au chama flani NEVER...Na kama ni kweli Mungu azidi kuwalaani na kuzidi kuwanyima akili na maarifa na awape adhabu stahiki kwa kutunyima na kuwashindwa kutupatia huduma za msingi na maendeleo hadi leo hii...MUNGU AWAPE ADHABU YAKE SAWASAWA NA MATENDO YAO.
 
Hii inch ni ya hovyo sana....kama wamegharamiwa na ubaloz kwann wanyimwe vibali?
 
Anyway, mi ni ukawa damu lakini kwa hoja hizo sidhani kama inafaa kulalama hivi. Tumieni namna nyingine hata ikiwezekana teleconference. Siku hizi teknolojia ni pana. Kumbuka anayempiga chura teke anamuongezea mwendo
Mkuu usiwapangie watu wanaokupa ufadhili tena mpaka na nauli,eti wawe na teleconference!!maana ya kukulipia wewe nauli uende kwenye mkutano ni nini?
 
wewe ukisubili ruhusa itakula kwako,kama pesa yote ya safali watatoa wao siku nyingine,we nenda tu maana hawato kuvua umeya

Unaomba ruhusa kama unatumia fedha za serikali kuu na sio kama unajifadhili mwenyewe kutumia njia zako!! Usitegemee huruma toka kwa haya magamba; kamanda uko vitani tumia mbinu za msituni kufikisha malengo!!
 
Sasa huyu Meya hatokani na chama cha kijani, halafu matumizi ya safari yake hayakuwa yana lipwa na serikali. Kwani alitakiwa kuomba ruhusa Ikulu au alitakiwa kuomba ruhusa Chadema?
Mimi naona kama alijichanganya maana yy japo yuko kiutendaji serikalini bali ki utawala hatawaliwi na serikali ya Ccm.
 
Wasianze kutafuta huruma kutoka kwa wananchi,wanatakiwa watimize ahadi zao.

Huyo jamaa aliitisha press conference akidai Kinondoni haihitaji pesa alizoomba RC Meck Sadiq kwa rais sababu makusanyo ya kodi yanajitoshereza baadae tena akajitokeza tena kudai DC Makonda anamuingilia majukumu yake.

In fact jamaa kila siku analalamika kwenye media tu as if hiyo ndiyo kazi yake.

Kwa hiyo jiji bado linanuka sababu wamenyimwa vibali vya kufuata vifagio Istanbul?

Kama hawawezi kustahimili hujuma za CCM si wang'atuke badala ya kuendelea kujilizaliza.
 
Mkuu usiwapangie watu wanaokupa ufadhili tena mpaka na nauli,eti wawe na teleconference!!maana ya kukulipia wewe nauli uende kwenye mkutano ni nini?
Kwani kawapangia au hali halisi imejionyesha? Alipaswa atoe taarifa hiyo kwa hao wafadhili aonyeshe na jitihada alizofanya na mkwamo aliopata na kisha awaombe mbadala ili tu aweze kupata huo ufadhili. Kulia tu haitoshi
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SERIKALI YAANZA KUHUJUMU MAMEYA DSM

Habari za mchana ndugu waandishi wa habari na wananchi wote ndani ya Manispaa ya Kinondoni, awali ya yote nimshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutujalia pumzi na uhai mpaka leo hii, alikadhalika niwe miongoni mwa wengi tunaowatakia heri ndugu zetu Waislamu, katika mwezi huu Mtukufu wa tiba, mwenyezi Mungu awajalie heri na kuzisikia funga ziwe zenye Baraka kwao na jamii kwa ujumla.

Baada ya kutoa utangulizi huo, ndugu zangu waandishi wa habari na wananchi wa Kinondoni, sio kawaida yangu kuongea habari zinazohusu Serikali Kuu, kwa kuwa ninaamini kuwa Maendeleo ya Wananchi wa Mkoa huu wa Dar es salaam na Wilaya ya Kinondoni, hayawezi kuletwa kwa ubinafsi wa viongozi, bali ushirikiano mwema ya sisi tuliopewa dhamana ya kuziongoza Halmashauri kutoka vyama vinavyounda UKAWA, na CCM wanaounda Serikali Kuu. Jambo hili hufanya tuwe kimya na wavumilivu mara nyingi sana, ingawa bado kuna mahusiano ya kutia shaka kila kukicha.

Ila leo ndugu zetu waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla, tumeamua kuandika na kufikisha ujumbe huu kwenu, ili mjue yalipofikia kama viongozi na Serikali Kuu na mabaya yanayoendelea na ya kusikitisha sana.

Na kusema huku, tutafanya viongozi wakuu wa nchi kama walikuwa hawajui wajue au walitoa baraka hizi, basi sawa watusikie masikitiko yetu haya, kwa kuwa tulikuwa na imani nao sana na bado tutaendelea kuwa na imani nao kama Serikali juu ya kutatua changamoto na matatizo ya Wananchi.

Hali ya kimahusiano kati ya Mameya wanaotokana na UKAWA na Serikali Kuu si mazuri hata kidogo, viongozi tumeamua tuhabarishe umma wa Watanzania kuwa kuna hujuma za waziwazi zinazofanywa na wenzetu juu ya shughuli za Mameya wa Kinondoni, Ilala na Jiji la Dar es salaam.

Si mara ya kwanza hii kwa sisi Mameya kuhisi kuhujumiwa na baadhi ya viongozi serikalini ambao kimsingi, sisi tuliamini uchaguzi umeshapita na kwamba kila mmoja wetu atampa mwenzake heshima inayostahili juu ya ajenda za Maendeleo, ndiyo maana kama nilivyo sema hapo awali, tumekuwa kimya juu ya vikwazo vidogo vidogo ambavyo tulihisi ni hujuma lakini tukaamua kuwa kimya na wavumilivu lakini tunatambua kuwa ipo mikakati ovu mingi dhidi yetu, ya kutukwamisha tusifanikiwe kuleta Maendeleo ndani ya Mkoa wetu na Wilaya zetu, hata tulipo amua kuvumilia uchokozi wa wawaziwazi wa kejeli za kutishia kunyang'anya Mameya magari na vinginevyo, kutoka kwa mtu tunaye muheshimu kama Waziri wa TAMISEMI ofisi ya Rais, akidai wakurugenzi watupore magari tena mbele ya vyombo vya habari.

Ila sasa hujuma zimefika mahali pabaya kiasi kwamba kutukwamisha kupata misaada ya Maendeleo kutoka kwa nchi rafiki na Halmashauri zilizopo Dar es salaam.

Binafsi Manispaa ya Kinondoni nilishawahi kunyimwa ruhusa nisisafiri kwenda nchini Afrika ya Kusini nilipokuwa nimealikwa na wahisani waliotaka kunifadhili kutengeneza mto Mlalakuwa, uliokuwa utengenezwe kingo zake kuanzia Goba,Makongo juu mpaka Kata ya Kawe kuelekea baharini, wafadhili hao ni ICLEI-local government sustainability, mradi ambao ulikuwa unafanyika nchi nyingi za Afrika.

Mbali nakuwa wafadhili walikubali kulipia usafiri,malazi na gharama zote za kongamano lililokuwa lifanyike huko Afrika Kusini, nchi zote zilifika katika kongamano la CIP AIRR, lakini uwakilishi wetu ulikosekana kwa kisingizio cha ruhusa kutopatikana, madhara yake Manispaa ya Kinondoni ikaondolewa kwenye programu ya kufadhiliwa huku nchi kama Ghana,Kenya,Zambia na nyinginezo zikifadhiliwa. Baada ya mkutano kuisha nchini Afrika Kusini, Katibu Mkuu kiongozi akaniandikia kibali cha kusafiri, baada ya kongamano kuisha na kukosa kiasi cha tshs Bilioni 1.3.

Pamoja na hayo, Ubalozi wa Uturuki ulikuwa umedhamini safari ya Mameya kwenda Uturuki kukutana na wadau na wafadhili wa miradi mbalimbali ikiwemo ikiwemo Chuo Cha Ufundi ndani ya Manispaa ya Kinondoni, Ubalozi huo ulikuwa umeshatoa kibali cha kusafiri (Visa) lakini Serikali imevunja Safari hiyo.

Kwa kufanya hivi Serikali imezikosesha Manispaa zetu fursa za Maendeleo ikiwemo Chuo hicho cha Ufundi.

IMETOLEWA NA MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA KINONDONI:

BONIFACE JACOB.
IJUMAA 17/06/2016

Kwa nini hakuomba kibali kwa fisadi Lowasa si ndiyo Raisi wa mioyo yenu?`
 
Mameya nanyie muwe mnajiongeza, kila saa kulalamika tu!!

Kwanza wekeni mikakati yenu, kwani mnatambua vikwazo vilivyopo mbele yenu. Kwanza fanyeni haya:

1. Muwe wazi kwa wahisani wenu, weelezeni changamoto mnazo pitia, kwani CCM hawajazoea kushindwa ila sasa wameshindwa na wataendelea kushindwa!!

2. Technology ipo kwa sasa. Kwani ni lazima ww uende South Africa ndio hela ije Bongo? Huwezi kufanya Video Conference? Au hamjui ngeli kama mkulu?
Hamna official Email? Hamna formal communication systems with your donors? Huwezi tuma muakilishi kama kweli una nia ya msaada? Huwezi wasiliana na Ubalozi wa Tz kwa niaba na kumtaarifu donor wako?

2. Fukuzeni walinzi wote na PS wote ofisini kwenu au muwahamishie Ofisi za Wana CCM. Hawa ni waongo si mchezo, kila umbeya wanao, hawapitwi na kitu. Ajirini wenu wapya hasa wa Red-bridged.

3. Fanyeni kazi na media, tengeni hela za kuwahonga. Hawa nao kwa rushwa hawajambo!!
Tufuteni hujuma hizo na ni nani alie nyuma yake na video clip au voice clip, samabazeni kwa muda wa mwaka 1 , watahaibika na kukosa pa kujificha. Ila maneno bila ushahidi ni sawa na bure. YOU MUST SPEND MONEY! Nakumbuka zile Clip za Masaburi za kuandamana kuwa wanamtaka Dr. Slaa zimechangia sn yy kudharaulika na shindwa pia kiurahisi sn.

4. Siyo kila kitu uwe na kibali bhana inapo shindikana, kwani ulikuwa tiyari na tiketi na huduma zote ungehudhuria kama ww na si Meya!! Mf. Rais Mugabe alihudhuria Mazishi ya Papa kama mkatoliki na si Rais na hakukamatwa!! Sasa ww ni mwanasiasa Kibali cha nn? Ww nenda kama ww, wakizikataa hela Jenga kitega uchumi, ajiri vijana!!

Mm ni mtanzania kwenda Kenya hadi Magufuli afahamu?

Ushauri muwe munaomba mapema kabla ya kutukosesha hela!!
Umetoa ushauri mzuri lakini kwa nini CCM yenye umri wa miaka yote hii bado iwe na watu wasiojua kuishi na wengine kiasi hicho? Yaani imefika hatua Meya aishi kama yuko Serengeti na wanyama wasio na ufahamu!

Tatizo la CCM ni kuendelea kuwatumia watu wenye ufahamu mdogo ktk mambo ya ki-Dunia. Unaweza ukakuta Mkiti wa chama wa Wilaya, aliye na elimu ya darasa la chini kabisa kwa cheo chake, anatoa amri kwa OCD, kwa mkuruigenzi au hata kwa waiziri ili atekeleze mambo yasiyo na maana yoyote ile.

Waziri wa TAMISEMI ana elimu gani jamani maana sasa CV za web ya Bunge siziamini.
 
Naskia japo sina uhakika kuwa Simba cha Wenyewe ni Lawyer, alie achiriwa na UCCM!
 
Naskia japo sina uhakika kuwa Simba cha Wenyewe ni Lawyer, alie achiriwa na UCCM!
Dah! Alisoma chuo gani? Elimu yaweza kuwa hina uhusiano na utendaji wake lakini nimekuwa nikiamini kwamba mtu aliyezoea kufanya mambo yake kwa forgery ni vigumu sana atumie mbinu nyingine hata kama yuko kwenye kazi zinazohitaji uaminifu. Nitasikitika sana kama hata yeye atakuwa na elimu inayoitwa na JF kuwa ni ya HAPA NA PALE.

Bado ana umri wa kurudi shule ya maana.
 
,,,kip fighting makamanda na cha msing n kuwa mnatoa update kama iv ili wananch wajue kinachoendelea,,,,,mi wala sishangai mana aliyekuwa msemaj wa chama cha mwendokasi Nape aliwahig kusema akiwa Kigoma kuwa majimbo yote yaliyo chin ya upinzan wasahau maendeleo///,,,,,,,hawa jamaa n wabaguz xana ila ukiwasikia utadhan malaika
 
Back
Top Bottom