Serikali yaanza kuhujumu Mameya Dar es Salaam

Anyway, mi ni ukawa damu lakini kwa hoja hizo sidhani kama inafaa kulalama hivi. Tumieni namna nyingine hata ikiwezekana teleconference. Siku hizi teknolojia ni pana. Kumbuka anayempiga chura teke anamuongezea mwendo
Hahaaa..Mkuu umetimiza matumizi ya Ibara ya 18 katika katiba yetu....huna Logic
 
Nilifikiri awamu ya tano haitaendekeza siasa uchwara, Rais wetu alisema atakuwa raisi wa watu na vyama vyote. Kwa hiyo inawezekana hajui kinachoendelea huku chini. Katika mambo yanayoweza kuturudisha nyuma kiuchumi mojawapo ni kuendekeza siasa uchwara.. Tujaribu kuangalia Zanzibar na siasa zao.. Hapa kazi tu, maana yake hatuna longo longo za siasa...so sad
Magufuli hahusiki na ujinga huo hata kidogo, katika hili nitamtetea kwa nguvu zote. Huyo 'Area commissioner' wake ni 'project' ya kundi fulani ndani ya chama ambalo linaloa amini mafanikio ya chama yamo ndani ya ujinga na umasikini wa watu, hivyo watu wakielimika na kupiga hatua wanahisi hawatakua na ajenda wala influence.
Mkuu akimchunguza huyo dogo, naamini atakayoyagundua atamuondoa mbele ya vyombo vya habari tena kwenye mkutano wa hadhara.
 
Aisee nilikuwa mbioni kuanzisha uzi kuhusu ukimya wenu haswa katika masuala ya miradi ya maendeleo mfano UDA.Nashukuru kwa taarifa nimepata jibu la hoja yangu.
Ushauri
Pelekeni mashtaka yenu kwa wanamchi ili wajue nin kinaendelea msisubir mpaka ukaribie uchaguzi.
 
Meya naye aache ushamba, kwani angeenda bila kibali angefukuzwa kazi? Kibali ni utaratibu wa juzi tu unaowahusu waajiriwa wa serikali
 
Hakuna nchi iliyowahi kuendelea kwa utaratibu huu.
Hoja ya serikali ni kupunguza gharama (CUTCOST) na hiyo miradi kama kweli ilikuwa ni kwa ajili ya kuisaidia serikali na wananchi.
Sio sawa,
 
Nilifikiri awamu ya tano haitaendekeza siasa uchwara, Rais wetu alisema atakuwa raisi wa watu na vyama vyote. Kwa hiyo inawezekana hajui kinachoendelea huku chini. Katika mambo yanayoweza kuturudisha nyuma kiuchumi mojawapo ni kuendekeza siasa uchwara.. Tujaribu kuangalia Zanzibar na siasa zao.. Hapa kazi tu, maana yake hatuna longo longo za siasa...so sad

Kila kitu kina baraka kutoka juu! Sio hujuma za siri, ni mpango mahususi kufifisha wapinzani. Hii nchi ina viongozi wa ajabu mno! Inasikitisha mno kuwa raisi wetu alikiri kuwa atakuwa ni wawatz wote ila haya yanatokea! Kama ikulu ndo inatoa kibali, basi hata hili atakua alilijua.
Serikali iwe na huruma kwa watu wake!

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Hayo Hata marehemu Kabwe aliyafanya mwanza.. akamdanganya hadi pinda aigawe Halmashauri mara2. ahasante kwa kutujuza
 
Anyway, mi ni ukawa damu lakini kwa hoja hizo sidhani kama inafaa kulalama hivi. Tumieni namna nyingine hata ikiwezekana teleconference. Siku hizi teknolojia ni pana. Kumbuka anayempiga chura teke anamuongezea mwendo

Matatizo ya kufikiri kimasaburi haya!

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Mameya nanyie muwe mnajiongeza, kila saa kulalamika tu!!

Kwanza wekeni mikakati yenu, kwani mnatambua vikwazo vilivyopo mbele yenu. Kwanza fanyeni haya:

1. Muwe wazi kwa wahisani wenu, weelezeni changamoto mnazo pitia, kwani CCM hawajazoea kushindwa ila sasa wameshindwa na wataendelea kushindwa!!

2. Technology ipo kwa sasa. Kwani ni lazima ww uende South Africa ndio hela ije Bongo? Huwezi kufanya Video Conference? Au hamjui ngeli kama mkulu?
Hamna official Email? Hamna formal communication systems with your donors? Huwezi tuma muakilishi kama kweli una nia ya msaada? Huwezi wasiliana na Ubalozi wa Tz kwa niaba na kumtaarifu donor wako?

2. Fukuzeni walinzi wote na PS wote ofisini kwenu au muwahamishie Ofisi za Wana CCM. Hawa ni waongo si mchezo, kila umbeya wanao, hawapitwi na kitu. Ajirini wenu wapya hasa wa Red-bridged.

3. Fanyeni kazi na media, tengeni hela za kuwahonga. Hawa nao kwa rushwa hawajambo!!
Tufuteni hujuma hizo na ni nani alie nyuma yake na video clip au voice clip, samabazeni kwa muda wa mwaka 1 , watahaibika na kukosa pa kujificha. Ila maneno bila ushahidi ni sawa na bure. YOU MUST SPEND MONEY! Nakumbuka zile Clip za Masaburi za kuandamana kuwa wanamtaka Dr. Slaa zimechangia sn yy kudharaulika na shindwa pia kiurahisi sn.

4. Siyo kila kitu uwe na kibali bhana inapo shindikana, kwani ulikuwa tiyari na tiketi na huduma zote ungehudhuria kama ww na si Meya!! Mf. Rais Mugabe alihudhuria Mazishi ya Papa kama mkatoliki na si Rais na hakukamatwa!! Sasa ww ni mwanasiasa Kibali cha nn? Ww nenda kama ww, wakizikataa hela Jenga kitega uchumi, ajiri vijana!!

Mm ni mtanzania kwenda Kenya hadi Magufuli afahamu?

Ushauri muwe munaomba mapema kabla ya kutukosesha hela!!
uko sahihi ingekuwa na uzito sana kama angeenda airport na kwenye media tumuone anazuiwa kisa serikali haitaki akawaletee free BIL1.3 ya wananchi. Sasa kulalamikia kwenye offisi hata hatua huchukui napo sio sawa. Japo kama kweli wamezuiwa kwa sababu hizohizo sio sawa.
 
Najiuliza, huo msaada wa Nje ulikuwa na masharti ya kumwona kiongozi wa UKAWA ndipo itolewe? Jaribu kutumia Skype ili tupate hizo fedha.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SERIKALI YAANZA KUHUJUMU MAMEYA DSM

Habari za mchana ndugu waandishi wa habari na wananchi wote ndani ya Manispaa ya Kinondoni, awali ya yote nimshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutujalia pumzi na uhai mpaka leo hii, alikadhalika niwe miongoni mwa wengi tunaowatakia heri ndugu zetu Waislamu, katika mwezi huu Mtukufu wa tiba, mwenyezi Mungu awajalie heri na kuzisikia funga ziwe zenye Baraka kwao na jamii kwa ujumla.

Baada ya kutoa utangulizi huo, ndugu zangu waandishi wa habari na wananchi wa Kinondoni, sio kawaida yangu kuongea habari zinazohusu Serikali Kuu, kwa kuwa ninaamini kuwa Maendeleo ya Wananchi wa Mkoa huu wa Dar es salaam na Wilaya ya Kinondoni, hayawezi kuletwa kwa ubinafsi wa viongozi, bali ushirikiano mwema ya sisi tuliopewa dhamana ya kuziongoza Halmashauri kutoka vyama vinavyounda UKAWA, na CCM wanaounda Serikali Kuu. Jambo hili hufanya tuwe kimya na wavumilivu mara nyingi sana, ingawa bado kuna mahusiano ya kutia shaka kila kukicha.

Ila leo ndugu zetu waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla, tumeamua kuandika na kufikisha ujumbe huu kwenu, ili mjue yalipofikia kama viongozi na Serikali Kuu na mabaya yanayoendelea na ya kusikitisha sana.

Na kusema huku, tutafanya viongozi wakuu wa nchi kama walikuwa hawajui wajue au walitoa baraka hizi, basi sawa watusikie masikitiko yetu haya, kwa kuwa tulikuwa na imani nao sana na bado tutaendelea kuwa na imani nao kama Serikali juu ya kutatua changamoto na matatizo ya Wananchi.

Hali ya kimahusiano kati ya Mameya wanaotokana na UKAWA na Serikali Kuu si mazuri hata kidogo, viongozi tumeamua tuhabarishe umma wa Watanzania kuwa kuna hujuma za waziwazi zinazofanywa na wenzetu juu ya shughuli za Mameya wa Kinondoni, Ilala na Jiji la Dar es salaam.

Si mara ya kwanza hii kwa sisi Mameya kuhisi kuhujumiwa na baadhi ya viongozi serikalini ambao kimsingi, sisi tuliamini uchaguzi umeshapita na kwamba kila mmoja wetu atampa mwenzake heshima inayostahili juu ya ajenda za Maendeleo, ndiyo maana kama nilivyo sema hapo awali, tumekuwa kimya juu ya vikwazo vidogo vidogo ambavyo tulihisi ni hujuma lakini tukaamua kuwa kimya na wavumilivu lakini tunatambua kuwa ipo mikakati ovu mingi dhidi yetu, ya kutukwamisha tusifanikiwe kuleta Maendeleo ndani ya Mkoa wetu na Wilaya zetu, hata tulipo amua kuvumilia uchokozi wa wawaziwazi wa kejeli za kutishia kunyang'anya Mameya magari na vinginevyo, kutoka kwa mtu tunaye muheshimu kama Waziri wa TAMISEMI ofisi ya Rais, akidai wakurugenzi watupore magari tena mbele ya vyombo vya habari.

Ila sasa hujuma zimefika mahali pabaya kiasi kwamba kutukwamisha kupata misaada ya Maendeleo kutoka kwa nchi rafiki na Halmashauri zilizopo Dar es salaam.

Binafsi Manispaa ya Kinondoni nilishawahi kunyimwa ruhusa nisisafiri kwenda nchini Afrika ya Kusini nilipokuwa nimealikwa na wahisani waliotaka kunifadhili kutengeneza mto Mlalakuwa, uliokuwa utengenezwe kingo zake kuanzia Goba,Makongo juu mpaka Kata ya Kawe kuelekea baharini, wafadhili hao ni ICLEI-local government sustainability, mradi ambao ulikuwa unafanyika nchi nyingi za Afrika.

Mbali nakuwa wafadhili walikubali kulipia usafiri,malazi na gharama zote za kongamano lililokuwa lifanyike huko Afrika Kusini, nchi zote zilifika katika kongamano la CIP AIRR, lakini uwakilishi wetu ulikosekana kwa kisingizio cha ruhusa kutopatikana, madhara yake Manispaa ya Kinondoni ikaondolewa kwenye programu ya kufadhiliwa huku nchi kama Ghana,Kenya,Zambia na nyinginezo zikifadhiliwa. Baada ya mkutano kuisha nchini Afrika Kusini, Katibu Mkuu kiongozi akaniandikia kibali cha kusafiri, baada ya kongamano kuisha na kukosa kiasi cha tshs Bilioni 1.3.

Pamoja na hayo, Ubalozi wa Uturuki ulikuwa umedhamini safari ya Mameya kwenda Uturuki kukutana na wadau na wafadhili wa miradi mbalimbali ikiwemo ikiwemo Chuo Cha Ufundi ndani ya Manispaa ya Kinondoni, Ubalozi huo ulikuwa umeshatoa kibali cha kusafiri (Visa) lakini Serikali imevunja Safari hiyo.

Kwa kufanya hivi Serikali imezikosesha Manispaa zetu fursa za Maendeleo ikiwemo Chuo hicho cha Ufundi.

IMETOLEWA NA MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA KINONDONI:

BONIFACE JACOB.
IJUMAA 17/06/2016
Huu si mkoa tajiri!
Labda nafasi hiyo wakipewa Mwanza wanaruhusiwa!
 
Hadi ukiona anaongea uyu meya jua kavumilia sana na kama kweli wahusika wanafanya figisu figisu wabadilike
 
meya ni speaker wa baraza la madiwani tu. tatizo wanaingilia kazi za utendaji kama huyo wa kinondoni utadhani ndio mkurugenzi wa wilaya. mameya wa ukawa hawaelewi kazi yao wanadhani wao ndio serikali kwenye maeneo yao kumbe serikali ya magufuli ya ccm ndio inaongoza nchi.
 
Wewe unajua unachokiongea kweli
 
meya ni speaker wa baraza la madiwani tu. tatizo wanaingilia kazi za utendaji kama huyo wa kinondoni utadhani ndio mkurugenzi wa wilaya. mameya wa ukawa hawaelewi kazi yao wanadhani wao ndio serikali kwenye maeneo yao kumbe serikali ya magufuli ya ccm ndio inaongoza nchi.
Kwa hiyo hapo Meya wa K'ndoni kaingilia kazi gani ya CCM?
Tunaendelea kujuwa kuwa adui yetu ni CCM...na sisi kumchagua JPM haimaanishi tuliipenda sana CCM ila tulipata "imani" na record ya JPM,sasa kama anafikiri tutamsifia kwa kila kitu wakati watu tunataka mabadiliko basi 2020 utakuwa ni mwaka mgumu kwa uchaguzi zaidi ya 2015

Halafu mtu anatoka hadharani anasema "Niombeeni,Mimi ni Rais wa chadema,CUF,CCM na wale wasio na chama"...
Tumegundua "siri" ya umasikini wa nchi hii ni chama tawala,wanataka tuendelee kuwa masikini ili wapate mtaji wao wa kisiasa....Huyu mkuu wa kaya ni kisirani sana,aache siasa atuleteee maendeleo!!Kweli CCM ni ile ile
 
Tatizo kila mwanasiasa anajiona ni bora zaidi ya mwingine...hata ushauri wanapeana kwa kuitana majina ya ajabu ajabu unategemea nini?mtaungana!...tatizo ninyi wanasiasa mnazani wananchi mambugila kila siku...leo uniite sina akili,mwege au nyumbu alafu kesho unakuja kutaka ushirikiano kweli...kueni bana pendaneni shaurianeni kama watu wazima wenye uchungu na wananchi wenu...kila mmoja akijali tumbo la chama mtaishia kila siku kulalama na kuhitaji huruma ya wananchi
 
Meya naye aache ushamba, kwani angeenda bila kibali angefukuzwa kazi? Kibali ni utaratibu wa juzi tu unaowahusu waajiriwa wa serikali
Meya alitakiwa aambatane na baadhi ya waajiriwa pale Manispaa.. Hao sasa ndo wasingeweza kwenda bila ya kibali toka Ikulu.. Angeenda mwenyewe Meya sidhani kama ingeleta picha nzuri huko kwa wafadhili na kusababisha kuonekana longolongo..

Meya yuko sawa kuwahabarisha wananchi maana vita wanayopigwa ni kubwa sana.. Kuhamisha makusanyo ya kodi ya majengo toka kwa manispaa, ni moja ya hujuma ambayo viongozi wa upinzani kwenye manispaa wamefanyiwa..
 
Back
Top Bottom