Serikali yaagizwa kulipa Tsh. Bil 21.8 baada ya kupandisha bei elekezi ya Pamba

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Fedha hizo ni hasara iliyotokana na kushuka kwa bei ya kilo ya Pamba kwenye soko dunia mwaka 2019 kisha Serikali ikatangaza bei ibaki Tsh. 1,200 kutoka Tsh. 900 na kwamba Serikali itafidia hasara yote.

Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), imesema Serikali iwajibike kulipa deni hilo kwa wanunuzi kwa sababu kuna kampuni zilinunua Pamba kwa bei hiyo na kupata hasara.

========================

Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), imeagiza Serikali kulipa deni la Sh21.8 bilioni la wanunuzi wa pamba lililotokana na kununua zao hilo kwa bei ya juu kuliko bei ya soko la dunia mwaka 2019. Mwaka 2019, Serikali ilipanga bei elekezi ya pamba kuwa ni Sh1,200 kwa kilo, lakini baada ya msimu kuanza bei iliporomoka katika soko la dunia, hivyo ilibidi zao hilo kununuliwa kwa Sh900.

Hata hivyo, Juni 2019 akiwa wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga alitangaza kuwa bei itakuwa ni hiyo hiyo ya Sh1,200 kwa kilo na kwamba Serikali itafidia hasara.

Akizungumza baada ya kupokea na kuchambua taarifa ya Msajili wa Hazina kuhusu uwekezaji katika Bodi ya Pamba, Mwenyekiti wa PIC, Jerry Silaa alisema mwaka 2019, Serikali ilitoa bei elekezi ya kununua pamba iliyokuwa juu zaidi ya bei katika soko la dunia.

Alisema kuna kampuni zilinunua pamba kwa bei hiyo elekezi na kupata hasara, hivyo kuna deni la Sh21.8 bilioni. Silaa, ambaye pia ni mbunge wa Ukonga, alisema wanunuzi hao wasingeinunua pamba hiyo ingebaki kwa mkulima kwa kuwa ni zao la kibiashara lingewaingizia hasara kubwa.

“Serikali sasa ifike mwisho iweze kutatua hili, ilipe deni hili la Sh21.8 bilioni kwa wale wanunuzi walionunua pamba kwa bei elekezi ambayo Serikali iliweka na kwa makubaliano waliyokuwa wamewekeana ili sasa wanunuzi waweze kushiriki kwenye ukuaji wa zao la pamba,” alisema Silaa.

Kwa upande wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) ambayo walikutana nayo juzi, Silaa alisema kamati hiyo iliona kuna mlolongo mrefu kati ya mnunuzi wa nje ya nchi, mawakala wa ununuzi na mkulima. Alisema bei ya mwisho ambayo wakala anaitoa katika mnada anaweka tofauti na bei ambayo mnunuzi kutoka nje angenunua moja kwa moja kupitia mnada.

“Kunaonekana kuwa kuna pesa hapa katikati ingeweza kumnufaisha mkulima, lakini haipati kutokana na kuwa na mlolongo wa mawakala,” alisema.

MWANANCHI
 
Kwa nini hawakudai zamani?
Kwani waziri wa fedha alikuwa nani? Makamu wa rais ba waziri mkuu walikuwa akina nani.

Walimshauri nini rais?

Kama wapo washitakiwe kwa uhujumu uchumi na kushindwa kumshauri vizuri rais.
 
Back
Top Bottom