Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,024
- 1,616
Habari Wakuu, baada ya Bodi ya Sukari Nchini kutangaza bei elekezi ya Sukari, kuwa 2,700 hadi 3,200, kwa Kilogramu 1, siku 6 baadaye bado Wananchi wana sintofahamu nyingi sana
Mimi binafsi nina Maswali kadhaa ambayo natamani yapate Majibu kutoka katika Wizara husika
1. Bei elekezi inaanza lini? Baada ya tamko la Waziri au baada ya zile Tani 100,000 zilizoagizwa kuingizwa sokoni? Maana hadi sasa bei bado ni changamoto kila mtu ana bei yake
2. Mtu akiuziwa Sukari Kilo 4,000 anaripoti wapi? Maana Waziri aliishia tuu kusema Wafanyabiashara wasiotiii tamko watakuwa wamevunja Sheria. Mamlaka inapaswa kuweka wazi hili na pia hatua ziwe zina uhalisia. Maana ukimwambia tuu mtu 'ukikuta bei tofauti ripoti' ana ripoti wapi? Nilitarajia tamko liseme watu waripoti kwa Viongozi wa Mtaa au wapige namba fulani kwa utatuzi wa haraka
3. Halafu Serikali inasubiri nini kuweka Kikosi kazi cha kupita mtaani na kukamata WafanyaBiashara wanaokiuka Tamko la Waziri? Kwa sababu kutoa tamko bila Ufuatiliaji ni sawa na kuwaachia maamuzi wafanyabiashara, kwamba waamue wanafuata Tamko au laa.
Nawasilisha!