Billal Saadat

Senior Member
Nov 30, 2022
169
356
1679662963818.png

Tanzania yatoa msaada wa Dola za Marekani 1,000,000 kwa Uturuki kufuatia madhara ambayo nchi hiyo inepata kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea mwezi Februari mwaka huu.

Hii ni mara ya pili Tanzania kufanya hivyo baada ya majuzi kuwasaidia marafiki zetu wa Malawi waliokumbwa na Kimbunga kilichosababisha maafa.

Tanzania inarejea enzi za Mwalimu Nyerere ilipokuwa mstari wa mbele kulikomboa Bara la Afrika.
 
Mahela yanamwagika tu.

Halafu unakuta ni ile mikopo ya juzi tuliyopewa.

Tunajifanya matajiri kumbe tumekopa.

Na wao wanapokea tu.

Tuwaambieni wazikatae maana sisi tunahitaji zaidi kuliko wao.

Ni sawa na mzazi kutoa mchango wa harusi ya mtoto wa jirani kwa kupenda sifa wakati wanae wanalala njaa..
 
Mahela yanamwagika tu.

Halafu unakuta ni ile mikopo ya juzi tuliyopewa...

Tanzania iliongoza mapambano ya Ukombozi wa nchi kusini mwa Bara la Afrika tulikuwa na utajiri gani?

Tanzania haijatoa msaada kwa ajili ya sifa, Uturuki ni mshirika wa karibu kwa Tanzania kibiashara.

Ni sehemu ya ushirika wa kidiplomasia. Tanzania si kisiwa.
 
Ipitishwe sheria duniani, kuwa kiongozi wa nchi masikini, ni lazima upitie SWAT ya akili kwa muda usiopungua mwaka.

Tanzania hii hii? Kenya tu hapo wamepigwa na ukame, hata mahindi tu tunayolima wenyewe tulishindwa kuwapa! Malawi, Msumbiji, Madagascar, kila leo wanapigwa na majanga asili, tumewahi kufanya lolote kwa kiwango hicho?

Samahani, nimeenda mbali huko nje ya mipaka, kumbe kuna wamasai wametimuliwa kwenye makazi yao huko, ambako pia walikuwa wakinywa maji na mifugo...nakumbuka niliona picha ya madarasa ya udongo jimboni kwa NAPE

Hata baada ya kutawala miaka 60, hakuna hata mkoa mmoja wanaoweza sema wameujenga ukakamilika kwa huduma zote muhimu, HAKUNA.

Bilioni 2.3 kama msaada kwa european country?
 
Ipitishwe sheria duniani, kuwa kiongozi wa nchi masikini, ni lazima upitie SWAT ya akili kwa muda usiopungua mwaka...

Kwa Spidi hii ya Samia, 2025 Tanzania haitakamatika kiuchumi Afrika.
 
Mahela yanamwagika tu.

Halafu unakuta ni ile mikopo ya juzi tuliyopewa.

Tunajifanya matajiri kumbe tumekopa.

Na wao wanapokea tu.

Tuwaambieni wazikatae maana sisi tunahitaji zaidi kuliko wao.

Ni sawa na mzazi kutoa mchango wa harusi ya mtoto wa jirani kwa kupenda sifa wakati wanae wanalala njaa..
Hawa wanajenga reli yetu.

Ninapata shida sana kulaumu hili.
 
Back
Top Bottom