kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,000
- 17,909
Kuna watu wana makasiriko hadi mambo kama haya!! Sasa kuna ubaya gani kwa nchi kusaidia wahanga wa tetemeko? Hivi tumekuwa wabinafsi kiasi gani? Tunasahau kuwa majanga ya asili hayana mwenyewe na hayazuiliki kirahisi.
Tunasahau kuwa leo kwao kesho kwetu, tusipojitoa kwa kidogo chetu siku yatatukumba ni nani atatukimbilia? Famasiala nini? Usiombe yakukute.
Mtu analeta hoja za kijinga eti tunatoa msaada wakati vitu vimepanda bei, hizo bilioni 2.3 ndo zinawahenyesha na kuwatoa watu mapovu hivi? Bilioni 2.3 zinaweza vipi kupunguza bei ya unga au vitu kupanda kama sio roho mbaya tu?
Tumezoea kupewapewa tu, na sisi siku moja tukijitoa sio mbaya!! Tatizo bongo wengi hawajui diplomasia ya kiuchumi, Samia sio hayati mwendazake yule ambaye hela za tetemeko rambirambi alikula yeye na genge lake bila aibu. Alikuwa rais wa hovyo sana na hakuwa na hata na chembe ya aibu usoni na moyoni mwake.
Tujikumbushe : "Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewaomba wakazi wa Kagera walioathirika na tetemeko kufanya jitihada za kujijengea nyumba zao wenyewe kwani michango iliyochangwa na wadau imeelekezwa kwenye taasisi za serikali. Mkuu wa Mkoa amedai kuwa jumla ya fedha zilizochangwa ni zaidi ya Bilioni 5.4 na kusema kuwa zimeelekezwa katika kukarabati miundombinu ya taasisi za Serikali na kuwataka wananchi wanaosubiri msaada wa serikali kusubiri mchango itakayotolewa na wadau walioahidi kuwasaidia waathirika moja kwa moja."
Uturuki wametusaidia mangapi nchi yetu tokea uhuru? Yaani tatizo ni hiko kibilioni 2.5 ndo tunang'aka kiasi hiki angetoa bilioni 100 jee??
Kuna watu hawafurahii utawala na mageuzi aliyoyafanya Rais Samia hususan maridhiano na kurudisha maridhiano na demokrasia iliyokuwa imeporwa na dikteta katili wa awamu ya tano. Hawa Sukumagang ndio wanaopinga kila kitu. Mimi naona kama wamenunishwa na maridhiano kati ya Chadema na Mama, basi wahame nchi.
Tunasahau kuwa leo kwao kesho kwetu, tusipojitoa kwa kidogo chetu siku yatatukumba ni nani atatukimbilia? Famasiala nini? Usiombe yakukute.
Mtu analeta hoja za kijinga eti tunatoa msaada wakati vitu vimepanda bei, hizo bilioni 2.3 ndo zinawahenyesha na kuwatoa watu mapovu hivi? Bilioni 2.3 zinaweza vipi kupunguza bei ya unga au vitu kupanda kama sio roho mbaya tu?
Tumezoea kupewapewa tu, na sisi siku moja tukijitoa sio mbaya!! Tatizo bongo wengi hawajui diplomasia ya kiuchumi, Samia sio hayati mwendazake yule ambaye hela za tetemeko rambirambi alikula yeye na genge lake bila aibu. Alikuwa rais wa hovyo sana na hakuwa na hata na chembe ya aibu usoni na moyoni mwake.
Serikali: Fedha za Maafa ya Tetemeko Kagera zimeelekezwa kwenye Taasisi za Umma
Wakuu, Kuna habari picha ambayo inasambaa mitandaoni (hususani Whatsapp) yenye maneno kuwa.. "Serikali imewaomba wakazi wa Kagera walioathirika na tetemeko kujijengea wenyewe kwani michango iliyochangwa na wadau imeelekezwa kwenye taasisi za serikali." Picha hiyo ni ya kutoka ukurasa wa...
www.jamiiforums.com