Serikali ya Rais Samia kutoa mbolea ya ruzuku mpaka 2025

kalacha mateo

Senior Member
Sep 27, 2021
118
237
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dk Stephan Ngailo amesema serikali itatoa mbolea kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2022/2023 hadi 2024/2025 ili kuwapunguzia wakulima gharama za kilimo.

Serikali imeanza maandalizi ya kutoa ruzuku ya mbolea kwa msimu wa kilimo mwaka 2023/2024 ili ifikapo Julai Mosi, mwaka huu iwe imesambazwa kwa mawakala. Aidha, imewataka wakulima ambao bado hawajasiliwa kwenye daftari na mfumo wa wakulima wahakikishe wanasajiliwa na kutoa taarifa sahihi ili kuwarahisishia kupata mbolea kwa wakati.

Pamoja na hayo serikali imeanza kutatua changamoto zilizojitokeza kwa msimu wa 2022/2023 ikiwemo mbolea kuchelewa kufika kwa mbolea. Katika msimu huu mbolea zitasambazwa kwenye vyama vya ushirika pamoja na kuongeza mawakala haswa pembezoni mwa nchi lakini kutoa maghala bure kwa kampuni ambazo zimesajiliwa kusambaza mbolea.

89586592.jpg
 
Back
Top Bottom