Serikali ya Madalali na Vishoka Pamoja na Sera za Kuuza Nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya Madalali na Vishoka Pamoja na Sera za Kuuza Nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by VoiceOfReason, Oct 20, 2011.

 1. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Hakuna pesa za elimu ya bure na afya ya bure…(ni kweli kwa sasa na kwa mtindo huu hizi pesa hazitapatikana, tutaendelea kuwa omba omba mpaka miaka 1000 baada ya uhuru..!!)


  Kwa kauli ya Waziri Mkuu mwenyenye Mh. Pinda alisema inachukua 10% tu ya watu kulisha nchi nzima.. (nakubaliana nae 100%) kilimo cha sasa ni efficient sana na kwa kutumia machinery taasisi kama moja au mbili tu zinaweza kulisha nchi nzima na kupata surplus ya kuweza kuuza.

  Cha ajabu kinachotokea sasa hiyo 10% itakayolisha nchi tunataka iwe wageni kutoka nje ambao tunawapa ardhi bora kwa kisingizio kwamba watamsaidia mkulima mdogo wakati ukweli ni kwamba mkulima mdogo atakufa, hawa watu wanajali faida tu hata kodi watatumia loopholes kuzikwepa na watahakikisha wanacheza na supply ili demand ibakie kubwa na kusababisha bei zisishuke sana.

  Swali langu ni kwamba hivi Serikali haiwezi kuhakikisha kwamba hao10% watakaolisha nchi wasiwe ni state ili kuhakikisha kwamba wanachojali sio profit bali ni service kama (afya na elimu ya bure na kuacha kutembeza bakuli kuwa omba omba) ? Sababu wanachofanya sasa ni kazi ya uuzaji na kuwa madalali. Hivi hii ndio kazi ya serikali kutafuta wawekezaji ?, kwanini wenyewe washindwe kuwekeza..?

  Don’t get me wrong sikatai uwekezaji ila kwanini baada ya kuzalisha kwa wingi na kwa bei nafuu wawekezaji wasiitwe waje kujenga viwanda vya food processing ili ajira ziongezeke… (lakini means of production iwe state owned for the benefit of the people) how much does it cost au how hard is it mpaka serikali ishindwe..?

  Please tell me why the government can not do this…, na kama ni kweli serikali ipo pale kuzunguka kila mahali na kubembeleza watu waje wajichotee sehemu zetu zenye rutuba wakati kuna mazao yanaoza vijijini kwa kukosa wanunuzi.

  Na kama serikali imeshindwa kuwekeza yenyewe labda ipo kwenye kazi ambayo sio yake na wapishe wengine wajaribu na wenyewe waingie kuwa taasisi ya biashara..
   
 2. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Unajua kusema kweli hili bara la Afrika sijui lina laana au lilipaswa kutengwa kabisa na the rest of humanity. Karibu kila nchi utakayokwenda sehemu kubwa ya viongozi wana tabia hizihizi za kuweka maslahi yao na rafiki zao mbele halafu nchi wanaitupilia mbali.

  Ninaamini kuwa hayo mawazo yako wapo watu wengi tu ambao huwa wanaishauri serikali lakini kwa vile maendeleo ya nchi na wananchi siyo agenda yao basi tunazidi kuliwa.

  Lakini nadhani sisi nao ni wa kulaumiwa kwa sababu tunaiogopa serikali na hatuko tayari kuchukua hatua stahiki ambazo nchi zingine watu wanachukua. Tunaogopa machafuko na serikali kwa kujua hili inacheka tu kwa kwenda mbele huku ikiifilisi nchi.

  Uwezo wa kubadili mambo na kusimamia nchi wanao ila hawana nia hiyo. Jiulize nchi kama Korea Kusini, Malaysia, Singapore au Indonesia

  zimetupitaje kimaendeleo wakati miaka ya mwanzoni mwa uhuru tulikuwa karibu sawa tu. Patriotism haipo kabisa ndiyo maana leo tuko hoi kiasi hiki, ni hatari mno.
   
 3. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Kumbuka Wakuu sisemi kwamba hawa jamaa wasije ila ni vizuri hizi mega farms zikawa mikononi mwa state inayowajali wananchi na sio mifuko yao au profit zao..; angalia hii article ya UK iliyotokea June, uone ni nini kinaweza kutokea na jinsi hizi industrial farms uwezo wake ulivyo:-

  Kwahiyo wakuu ninachosema mimi sio kwamba tusiende huko bali keki hio isimilikiwe na wawekezaji bali serikali iwekeze kwa niaba ya wananchi na kutoa service kwa kila mwananchi.
   
 4. T

  Topical JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Unajua nyie hamjui wapebari na sera..

  mimi sioni unachokataa na kukubali hapo hapo (unataka wawekezaji unakataa sijui nini? hueleweki
   
 5. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Wawekezaji wa Kitanzani ni wasanii watupu. Metl amepewa shamba la katani, hakuna la maana analofanya.
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Oct 20, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hapa mkuu wangu unatupaka mafuta ya mgongo.. Ukweli ni kwamba wawekezaji ktk kilimo hawatakiwi kutoka nje -WASIJE kabisa ila uwekezaji utoke ndani, binafsi sikubaliani na siasa za kwamba wananchi hawawezi ati hawana mtaji wa kutosha na uhuni mwingineo kama walivyofanya wakoloni walipoivamia Afrika...

  Kilimo tunakiweza na waafrika tumejaliwa ujuzi wa kilimo na tunapenda kulima. Huku kuna mashamba mengi sana na ukweli ni kwamba wafanyakazi ktk mashamba hayo ndio wanatoka Africa, Jamaica na South Amerika... Nenda ktk website ya Canada utaona kitengo cha visa kwa watu wanaotafuta kazi za ukulima mashambani, kuna watu kutoka Kongo na Burundi wamejaa hapa wakilima ktk mashamba ya hapa why?.

  Leo sisi tunaagiza wawekezaji kisha wananchi wenyewe ndio wanakuwa wakulima waajiriwa mnategemea wakatoka vipi?
   
 7. M

  Makupa JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hata mbowe ni kama dalali tu mnakumbuka yale malori
   
 8. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mkuu ni rahisi sana ardhi yetu na vyanzo vingi vya maji ni goldmine.., (ambayo badala ya kuwagawia private sectors) inaweza ikasimamiwa na serikali (au vyama vya ushirika) kwa niaba ya wananchi wote ili faida yote 100% iwe kwa faida ya wananchi wote.. Kuliko kitakachotokea kwa kuwapa hawa so called wawekezaje (foreigners) na sijui utawabana wapi sababu hata kodi wataziepuka kwa loopholes nyingi tu..

  Kilimo cha kisasa sio rocket science kusema kwamba serikali itashindwa ukizingatia SUA inatema watu kila leo (hata wanaposhindwa wanaweza kuleta so called experts in short contracts)

  Wawekezaji waachi waje wajenge viwanda na ku-compete na malighafi zinazozalishwa..., It simple mkuu badala ya kugawa ngombe wako wa maziwa uzia watu maziwa...!!!
   
 9. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #9
  Oct 20, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Na Serikali ya Tanzania ni ya kisanii, angalia tatizo la Umeme na Maji bado hatujagusia Afya, Ajira, Barabara mbovu na Ufisadi uliyokithiri unaoongozwa na Lifisadi Papa Kikwete kwenye Nchi yetu
   
 10. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #10
  Oct 20, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mkuu mimi siongelei ngozi ya mtu tu bali naongelea ubepari in general kwa jambo kubwa kama hili kuwepo kwenye mikono ya wachache.., kwanini jambo kama hili apewe mtu mmoja na sio taasisi ambayo itakuwa pale kwa niaba ya umma, ndio mpaka sasa vyama vya ushirika vimekuwa na ufisadi ila kwanini visiangaliwe kwa usimamizi zaidi.., na kuhakikisha vikakuwa productive ?
   
 11. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #11
  Oct 20, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mkuu ni kweli usemayo lakini huoni kwamba with machinery hata manpower itapungua sababu kazi nyingi kuanzia kulima, kupanda na kuvuna itakuwa ni mashine lakini tukifanya hizo kosa na hizi mashine zikawa ni za watu kutoka nje watanzania tutabakia kuwa walinzi wa haya mashamba...!, na competition itakuwa kubwa hata wale wenye mashamba madogo watakufa kifo cha kawaida.., vilevile profit kubwa itapelekwa kwa hawa watu kwao na huenda hata viwanda vya processing vyote vikawa nchini kwao...

  Kwahiyo mkuu nakubaliana na wewe kabisa kwenye hii goldmine asiguse kabisa mtu aliye nje kuja hapa labda wakitaka sana wapewe sehemu kame ambazo hazilimiki wala hazina maji na ukame mkubwa in the middle of nowhere lakini sehemu nzuri nzuri zote ziwe kwa manufaa ya jamii (100%)
   
 12. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #12
  Oct 20, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,249
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Imekaa vema sana mkuu!
   
 13. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #13
  Oct 20, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Sijui unataka kuzungumza nini VoR, hapa nadhani unazungumzia Zama za Siasa ni Kilimo.
  Unazungumzia Kilimo, ktk zama kama hizi za Ufisadi na Wizi kila mahali, Mkulima wa Pamba mwaka huu anatangaziwa kuwa bei ya Pamba msimu ujao itakuwa Tsh 1,200/=, anahamasika anaenda kulima Pamba, akivuna akienda Sokoni anaambiwa NO, bei ni Tsh 800/=, Huu ni Ubakaji wa Nguvu za Mkulima.
  Hizi ni Zama za Wanasiasa kukutana KEMPINSKI na kupitisha neno Kilimo Kwanza, a shopping list of CCM( Ilani)
   
 14. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #14
  Oct 20, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,367
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  Pinda na wapambe wako humu JF: Mambo uloandika nakuhakikishia wewd ni Pinda ama wapambe wako, lakini na nyie chukueni hii, ikiwauma lets meet kesho then, mzalendo ni yule alie tayari kuipoteza nafsi yake kwa ajili ya Watanzania wenzake maskini, kwanza wewe unatumia jina kwa lugha za kigeni which to me seeen as unaficha wewe ni nani hasa, pili ulichokiandika kinataka akili ya pili kuelewa maana ya ujumbe wako na tatu usiendeleee kuleta upupu JF kwani siku tukikuumbua hutakuwa na wa kulia nae.
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Oct 20, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kwanza mimi skubaliani na swala hili la kupunguza idadi ya wakulima hadi kufikia 10%.. Niliwahi kulizungumzia hili nyuma na nitaendelea kulizungumzia leo.

  Kila nchi ina watu na mazingira tofauti, kilimo kwa nchi za Ulaya sio suluhisho wala uti wa mgongo wa uchumi wao, hivyo hatuwezi kuiga Ulaya ikiwa sisi WATU na mazingira yetu ni tofauti kabisa. Zipo sababu kubwa zilizowalazimu wazungu kuwa na mashamba makubwa na idadi ndogo ya wakulima.. Nikiwa na maana wao karibu wote walikuwa wakulima kama sisi lakini mageuzi yao kiuchumi yalitokana na kufufuka kwa viwanda na huduma.. Technologia ndiyo iliyozaa ajira nyinginezo kiasi kwamba wakulima waliacha kilimo na kwenda kufanya kazi wakipata mshahara ama niseme pato kubwa kuliko kilimo cha mwaka mzima..

  Hivyo taratibu wananchi waliacha kilimo na kujiingiza katika ajira nyingine zilizozalishwa na sii kwamba Ukulima wenyewe ulipatiwa ufumbuzi wa kutafuta asilimia 10 ya wakulima..Hivyo kwa kila mkulima aliyeondoka Mkulima aliyebakia alichukua eneo kubwa zaidi na kuzalsiha zaidi ili kukidhi mahitaji ya wale waliokimbilia mijini na matokeo yake ndio leo tuna wakulima wachache zaidi ya miaka 100 iliyopita lakini mageuzi haytakutokana na kubadilisha namna ya ukulima.

  Sisi kwa upande wetu tunataka kubadilisha Ukulima kwa kutumia mikakati hewa ambayo inawaondoa wananchi ktk Ukulima pasipo kuwapamkazi nyingine isipokuwa Utumwa ktk kilimo hicho hicho..Kama tunataka mageuzi ya kilimo basi tuanze na kujenga viwanda, jamani wakati wa Nyertere tulikuwa na kiwanda cha Baiskeli leo hii na madai ya kuendelea kiwanda hicho na vingine vingi vimekufa sasa hao waajiriwa wake unategemea wanafanya nini?... wengi wao kwa kukosa ajira mijini wamerudi ktk Kilimo! - Unaiona tofauti hapo?. Sasa leo hii ukiwaondoa tena katika kilimo wakati hawa watu wamepoteza ajira zao mijini wakarudi mashambani ambako serikali inawanyang'anya tena mashamba unafikiri haya ni maamuzi mazuri ya kiuchumi?.

  Mageuzi ya Uchumi siku zote hutokana na mikakati inayowezeshwa na sio kulazimishwa, gradualy vitu hivi vitabadilika ikiwa serikali itaweka policies na mikakati ktk uwekezaji wa miundombinu itakayo wezesha ukuaji wa viwanda na huduma mbalimbali..Kinachofanyika Tanzania leo ni Udikteta mbaya sana kuliko hata uile wa Nyerere kwa sababu at least Nyerere alikuwa na mrengo, dira na imani ya kwamba tukiweza Ukulima ulikuwa uti wa mgongo wa uchumi wetu na alijaribu kwa kila hali kuhakikisha wananchi wanabakia vijijini wakati viwanda vikijengwa badala ya kila mtu kukimbilia mijini ambako ajira zilikuwa bado zilkizalishwa taratibu ktk ujenzi wa viwanda na mashirika ya Umma..

  Leo tunafanya maamuzi kwa kuogopa umaskini na njaa ya kukimu matatizo yetu kama mwananchi wa India ambaye yuko radhi kuuza ini au figo zake ili apate mtaji wa kuuza Kacholi na chai.
   
 16. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #16
  Oct 20, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nina wasiwasi tu kwamba lazima wajukuu wetu watafika mahali pa kufukua makaburi yetu ili waangalie kama tulikuwa binadamu halisia
   
 17. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #17
  Oct 20, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mkuu nadhani tupo on the same boat mimi siongelei kupunguza for the sake ya kupunguza.., pia siongelei kwamba hii issue itokee overnight.., hapana. Ninachosema mazao kama nafaka ambayo yanaweza yakawa produced efficiently using heavy machinery yafanywe hivyo (na sio na private sectors wala muwekezaji bali na state/vyama vya ushirika...) na profit yake hii yote iende kwenye services na welfare za wananchi (na pia hii itafanya chakula kishuke sana bei).., kwahiyo utaona na heavy production power ya hizi mashine individuals watakuwa hawana faida sana na kulima hizi nafaka swali linakuja watafanya nini..? majibu ni kama ifuatavyo:-
  • Kwa kuwa na viwanda au food processing industries wanaweza kupata ajira
  • Nafaka ndio itakuwa sio profitable kulima lakini kuna mazao ambayo ni valueable per hectare, mfano mboga, viungo maua, uyoga n.k. hawa wakulima au hobbyist wanaweza part time na efficiently wakalima haya mazao ambayo wakiuza yatawapatia faida huku wana uhakika kwamba mashamba ya ushirika/state yanawaletea chakula cha uhakika na faida inayopatikana inawasomesha na kuwatibu watoto wao na ndugu zao (yaani mzazi anao uhakika kwamba akizaa tu mtoto wake atafika university bila kuja na kudai ada wala usumbufu wowote
  • Pia serikali inaweza ikasimamia mashamba makubwa ya mifugo ambayo yatahakikisha kuna nyama ya kutosha, maziwa pamoja na kusindika nyama (beef) n.k. hii itapunguza ila adha ya sasa kila mtu anataka mifugo mingi na kugombania sehemu ya malisho.., sababu as a community tutajua kwamba tuna uhakika wa nyama ya bei nafuu.
  Kwahiyo mkuu mimi point yangu ya 10% ni kwamba ile efficiency kama taasisi kama mbili au serikali inaweza ikalima mwaka mzima na kulisha watu wote (kwa nafaka) kwanini wananchi wengine wasiconcentrate kwenye kulima vitu vingine ambavyo wanaweza kuvifanya effectively.

  Ila what is happening now kwa kweli inatisha sana tena sana tunauza nchi yetu wenyewe mchana kweupe na viongozi wetu wanatuuza sisi na wajukuu zetu bila kutupa option.., Itakuja kufika wakati mtu elimu hauna, pa kulima hauna wala kazi ya kufanya haipo (unakuwa mtumwa kwenye nchi yako mwenyewe).., tunapoenda yaani hata wizo utakuwa ni career ujambazi utaongezeka, chuki, umasikini na matabaka makubwa sana..., kama baba yako ni masikini leo basi hadi kitukuu kitakuwa masikini...

  Kweli we need to rethink before its too late
   
 18. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #18
  Oct 20, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mkuu nimesema hivi sababu yanayotokea sasa ni madogo huko tunakokwenda panatisha zaidi sababu sasa hata unayo ardhi ya kupanda uyoga na mchicha ukashindia ubuyu wewe na familia yako.., huko tuendako itakuwa ni shughuli kubwa tukiuza hata means ya kutulisha itabidi tutegee debe la mahindi kwa hisani ya muwekezaji.., hata wale big four wanaotulisha sasa kwa jembe la mkono watapotea.., na hawa jamaa ndio watapanga bei wakuuzie mahindi kwa bei gani..., na wewe hata pesa ya kununua mahindi utakosa sababu hakuna ajira na wote hatuwezi kupiga debe kwenye daladala au kufagia ofisi za boss..


  Mkuu we acha tu..., wakati kuna option ya pili badala ya huyo jamaa mmoja au wachache kuwategemea hiki kitega uchumi kingekuwa chetu wote na kuhakikisha watu wanapata keki yao kwa uzuri zaidi na sio kwa hisani ya watu wachache

  Sasa hivi tupo 40m just imagine tukifikia kwenye 60m (hakuna ajira na nchi yote inamilikiwa na wachache...) patakuwa HAPATOSHI
   
 19. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #19
  Oct 20, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Hossam
  Senior Member [​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG]


  Join Date : 2nd September 2011
  Posts : 95
  Rep Power : 21

  ...Hizi CRAP nyingine jamani. wewe umejiunga humu Juzi, hujui hata Rules and Regulations za humu JF, leo unajipa U-Kiranja Koko humu.
  hebu nionyeshe nilipomfagilia huyo Pinda wako hapo, tatizo la kufikiri kwa kutumia Masa.......
   
 20. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #20
  Oct 20, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mkuu VoR, ndio maana nasema unazungumzia History, Mwalimu alianzisha Siasa ni Kilimo, na hii ilifanyika kwa Vitendo, Mwalimu mwenyewe akiongoza, enzi hizo Wanasiasa walipaswa wawe na Mashamba ya Mfano, ndio kipindi ambacho Wananchi(Wakulima) walihamasika na Kilimo, Vyama vya Ushirika vilianzishwa na kusimamiwa.
  Sasa hivi nadhani ni kwa sababu Serikali inakosa Vipaumbele, Serikali haiwekezi vya kutosha say ktk Kilimo, badala yake wanakuja na kauli Mbiu, kila Kukicha. Hao Wawekezaji wanaokuja nao kwa sababu ya mikataba ya kifisadi wanayoingia na Watendaji Serikalini, basi wanakuwa Miungu Watu, mwekezaji anauziwa Shamba lilikuwa linatumika kwa kilimo cha Mpunga, yeye anakuja analima mbogamboga.
  Siku hao Wakulima wa the Big four watakapogoma kulima, hali itakuwa tete zaidi, yatatukuta ya Somalia
   
Loading...