Serikali ya Madalali na Vishoka Pamoja na Sera za Kuuza Nchi

Mkuu nadhani tupo on the same boat mimi siongelei kupunguza for the sake ya kupunguza.., pia siongelei kwamba hii issue itokee overnight.., hapana. Ninachosema mazao kama nafaka ambayo yanaweza yakawa produced efficiently using heavy machinery yafanywe hivyo (na sio na private sectors wala muwekezaji bali na state/vyama vya ushirika...) na profit yake hii yote iende kwenye services na welfare za wananchi (na pia hii itafanya chakula kishuke sana bei).., kwahiyo utaona na heavy production power ya hizi mashine individuals watakuwa hawana faida sana na kulima hizi nafaka swali linakuja watafanya nini..? majibu ni kama ifuatavyo:-
  • Kwa kuwa na viwanda au food processing industries wanaweza kupata ajira
  • Nafaka ndio itakuwa sio profitable kulima lakini kuna mazao ambayo ni valueable per hectare, mfano mboga, viungo maua, uyoga n.k. hawa wakulima au hobbyist wanaweza part time na efficiently wakalima haya mazao ambayo wakiuza yatawapatia faida huku wana uhakika kwamba mashamba ya ushirika/state yanawaletea chakula cha uhakika na faida inayopatikana inawasomesha na kuwatibu watoto wao na ndugu zao (yaani mzazi anao uhakika kwamba akizaa tu mtoto wake atafika university bila kuja na kudai ada wala usumbufu wowote
  • Pia serikali inaweza ikasimamia mashamba makubwa ya mifugo ambayo yatahakikisha kuna nyama ya kutosha, maziwa pamoja na kusindika nyama (beef) n.k. hii itapunguza ila adha ya sasa kila mtu anataka mifugo mingi na kugombania sehemu ya malisho.., sababu as a community tutajua kwamba tuna uhakika wa nyama ya bei nafuu.
Kwahiyo mkuu mimi point yangu ya 10% ni kwamba ile efficiency kama taasisi kama mbili au serikali inaweza ikalima mwaka mzima na kulisha watu wote (kwa nafaka) kwanini wananchi wengine wasiconcentrate kwenye kulima vitu vingine ambavyo wanaweza kuvifanya effectively.

Ila what is happening now kwa kweli inatisha sana tena sana tunauza nchi yetu wenyewe mchana kweupe na viongozi wetu wanatuuza sisi na wajukuu zetu bila kutupa option.., Itakuja kufika wakati mtu elimu hauna, pa kulima hauna wala kazi ya kufanya haipo (unakuwa mtumwa kwenye nchi yako mwenyewe).., tunapoenda yaani hata wizo utakuwa ni career ujambazi utaongezeka, chuki, umasikini na matabaka makubwa sana..., kama baba yako ni masikini leo basi hadi kitukuu kitakuwa masikini...

Kweli we need to rethink before its too late
Yes tupo msitari mmoja isipokuwa mimi nakataa kulazimisha kitu ili tuonekane tunafanya kama Ulaya.. Hii ndio nisichokubaliana nacho kwa sababu hata ukitazama heavy equipment wazungu wamezitumia sio kwa sababu walitaka kuwaondoa wakulima wadogo wadogo isipokuwa demand ya mazao yao iliongezeka kiasi kwamba jembe la mkono lisingeweza kutosheleza demand ya mazao yao...Hivyo utaalam wa kuunda heavy equipment ukachukua nafasi kwa sababu jembe la mkono halikuweza tena kutosheleza na ardhi ikatakiwa kubwa zaidi ili kuweza kuzalisha kiwango kinachotakiwa - Necessity was the mother of invention!

Tofauti na wao, sisi tunachogombea hapa ni ARDHI, hakuna mkulima wala mchuuzi mwenye nia ya kuongeza uzalsihaji hilo ndio ukweli, kinachofanyika leo ni udalali wa ardhi na viongozi wetu ndio macho yanawatoka..Serikali imeshindwa kutazama demand ya chakula badala yake wanatazama demand ya ardhi kuwa ndio biashara.. Kweli ni busara zaidi kuweka kilimo mikononi mwa serikali au wananchi wakafungua mashamba makubwa kwa sababu ndivyo alivyofikiria Nyerere kuhakikisha ardhi inabakia mikononi mwa wananchi (serikali), tunazalisha kulingana na mahitaji ili kukuza uchumi wetu lakini wazungu kama tabia yao ama kutokana na kushuka kwa uchumi wao miaka hiyo wakapunguza mahitaji ya mali za nje ikiwa ni pamoja na mazao yetu. Tulianguka lakini ukitazama kulikuwa na goals tumeweka na kuthamini ardhi na Uhuru wetu..

Binafsi ningependa kujua sababu hasa kwa nini kilimo kinakosa soko ndani ingawa demand ya vyakula imeongezeka kwanza kabla ya kuchukua hatua zaidi. Lazima kuna tatizo la kisera ambalo linawakwaza wananchi wakulima kujipanua ama kuweka nguvu zao ktk kilimo, ufugaji na uvuvi. Hii habari ya Kilimo kwanza ni policy mbovu ambazo zimetungwa na wanansiasa badala ya kupitia kwa mkulima. Halafu pia tukumbuke tu kwamba thamani ya shilingi inazidi kuporomoka vibaya sana wakati hali ya maisha inapanda kwa kasi muathirika mkubwa ni mkulima wa leo ambaye atanunua mahitaji yake kwa thaminisho la dollar.

Kwa hiyo vitu vyote vinakwenda sambamba, ili kuwawezesha wakulima tunatakiwa kuanzisha viwanda ndani nchini kulingana na mahitaji yaliyopo, tufiirie kujitegemea wenyewe. Necessity ipo! toka Ukulima hadi viwanda soko lipo kwa nini bado tunaagiza mali kutoka China, India na kadhalika wakati soko lipo ndani na hakuna sababu ya kimazingira, utaalam ama uwezo kuanzisha viwanda hivi bali tunataka kupanua kilimo, kupunguza ajira za wananchi wasiopungua asimilia 70 wakati hakuna viwanda wala ajira sehemu nyinginezo ni kujiongezea matatizo zaidi. leo hii nasikia zaidi ya asilimia 50 ya graduates wa University zetu hukosa ajira, hivi unafikiri hawa vijana wanafanya nini leo?
 
Yes tupo msitari mmoja isipokuwa mimi nakataa kulazimisha kitu ili tuonekane tunafanya kama Ulaya.. Hii ndio nisichokubaliana nacho kwa sababu hata ukitazama heavy equipment wazungu wamezitumia sio kwa sababu walitaka kuwaondoa wakulima wadogo wadogo isipokuwa demand ya mazao yao iliongezeka kiasi kwamba jembe la mkono lisingeweza kutosheleza demand ya mazao yao...Hivyo utaalam wa kuunda heavy equipment ukachukua nafasi kwa sababu jembe la mkono halikuweza tena kutosheleza na ardhi ikatakiwa kubwa zaidi ili kuweza kuzalisha kiwango kinachotakiwa - Necessity was the mother of invention!

Ndio mkuu ila kama opportunity ya serikali kuweza kuzalisha zaidi na kuweza kulisha east and central africa au africa kwa ujumla basi ichukue opportunity hii (ila hii haewezi kufanyika mpaka miundo mbinu pia iwe bora), kuongeza value ya mazao n.k.; na wafanye haraka na kuanza kufanya hivyo, point yangu ni kwamba hizi story za kwamba serikali haina pesa inakopa wala elimu bora au afya ya bure haiwezekani inabidi ziishe kwa kupata stream nyingine of income (tena kama nilivyosema kwenye hizi big farms serikali ingeconcetrate kwenye nafaka) na kuwashauri wakulima kwenye smaller farms wawe na kilimo cha mboga na viungo na other more valuable plants per hectare (ingawa kwanza wahikikishe wanawatengeneza miundombinu na uwezekano wa kumwagilia)
 
Serikali ya ccm na Deals za kutengeneza millions:

Huyu muhindi anapanga dili na Nape Nnauye, kama kawaida watachota hela serikalini.

ijay Kumar > Nape Nnauye Hi nape,

It is long since I heard from you. How are you? I came twice during the early part of this year.

Can I have your reachable Mobile number and mail Id? I have an interesting project on green energy which, if implemented, will definitely provide basic needs of millions.
I shall discuss in detail once I can contact you

Tuesday at 19:28 near Bangalore, India
 
Serikali ya ccm na Deals za kutengeneza millions:

Huyu muhindi anapanga dili na Nape Nnauye, kama kawaida watachota hela serikalini.

Vijay Kumar > Nape Nnauye Hi nape,

Hii heading yako mtoa mada imenifurahisha kweli,ingawa sijaweza connect vishoka na madalali hawa wa kitaa na jinsi serikali yetu ilivyo. Sijawahi kupata bahati ya ku operate kwenye ulimwengu wa madalali na vishoka
 
Tupo pamoja sana tu mkuu wangu. Kumbuka kile ulichokianzisha - Serikali ya Madalali na Vishoka pamoja na Sera za kuuza Nchi.. That's my concern
Sasa kwa nini tuwaamini watu hawa? Hawa ni Mafisadi ambao ARDHI kwao ni mtaji mpya wa utajiri na sio kilimo. Nataka ufahamu ya kwamba neno Kilimo halipo akilini mwao tusifanye makosa kama tulivyouza viwanda na nyumba za serikali..Leo hii wabunge wote ni matajiri pale walipo na kwa kila jimbo ukiuliza au kutazama matajiri ni kina nani basi Wabunge ni kati ya matajiri na wote wana ardhi kubwa wamenunua kwa kodi zetu. Leo hii ardhi ni mali yao kwa uchaguzi wako wa mwakilishi..

Kwa hiyo mkuu wangu CCM lazima itoke kwanza.. hakuna kitakachofanyika zaidi ya kumalizia uthiri ulobakia..Tazama WATU na MAZINGIRA kufikia maamuzi ya busara kwani leo hii kila mtu anataka ardhi na thamani ya ardhi imepanda juu kupita kiasi. Viongozi wengi wameshikilia ardhi wakidai ni wakulima wakati shamba hilo wamelikodisha kwa wananchi au wakulima wadogo wadogo wakisubiri wakati muafaka wa kuuza ardhi hiyo - Hii ndio hali halisi ya watu na mazingira tuliyopo.

Kama tutapata kiongozi au mtawala mwenye Uzalendo kama wa Nyerere mbona kila kitu kinawezekana na rahisi kabisa isipokuwa sasa hivi mkuu wangu tusijidanganye kwa kuwapa hawa watu mamlaka ya kupitisha mikakati yoyote ya maendeleo kupitia Ardhi yetu kwa sababu kote huko wameisha maliza kuuza imebakia ardhi tu na kilimo kinatumika kama sababu tu. Waogope viongozi hawa kama Ukoma na waswahili wanasema la kuvunda halina ubani - CCM kwisha kazi wamevunda ni madalali, vishoka na sera zao za kuuza nchi.
 
Ni kweli mkuu ila ninachokihofia huenda ikawa too late by then.., ndio maana ningependa nchi iwe na upinzani wa kweli na mkali ili waweze kuangaliana na kuchungana.., ila nadhani njia bora kabisa ni kwa wananchi kupata elimu na kuelewa kwamba kinachofanyika sasa sio sahihi na kuna njia mbadala ambayo ni bora zaidi.
 
[h=2]Wananchi 3, Polisi 3 Wauawa katika mauaji ya ardhi Dodoma[/h]

Baada ya hilo hapo kutokea leo..., nadhani Serikali isipotumia busara more of the same (au worse) itaendelea sana kutokea.. hususan population inavyozidi kuongezeka
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Do not ignore History,in Europe by 17th century LAND was of commercial value,power and dominance.Hiki ndo kinachoendelea na kutokea sasa.
 
Serikali ya ccm na Deals za kutengeneza millions:

Huyu muhindi anapanga dili na Nape Nnauye, kama kawaida watachota hela serikalini.

ijay Kumar > Nape Nnauye Hi nape,

It is long since I heard from you. How are you? I came twice during the early part of this year.

Can I have your reachable Mobile number and mail Id? I have an interesting project on green energy which, if implemented, will definitely provide basic needs of millions.
I shall discuss in detail once I can contact you

Tuesday at 19:28 near Bangalore, India

Mkuu unaweza kufafanua kwenye hii issue....?
 
Unajua kusema kweli hili bara la Afrika sijui lina laana au lilipaswa kutengwa kabisa na the rest of humanity. Karibu kila nchi utakayokwenda sehemu kubwa ya viongozi wana tabia hizihizi za kuweka maslahi yao na rafiki zao mbele halafu nchi wanaitupilia mbali.

Ninaamini kuwa hayo mawazo yako wapo watu wengi tu ambao huwa wanaishauri serikali lakini kwa vile maendeleo ya nchi na wananchi siyo agenda yao basi tunazidi kuliwa.

Lakini nadhani sisi nao ni wa kulaumiwa kwa sababu tunaiogopa serikali na hatuko tayari kuchukua hatua stahiki ambazo nchi zingine watu wanachukua. Tunaogopa machafuko na serikali kwa kujua hili inacheka tu kwa kwenda mbele huku ikiifilisi nchi.

Uwezo wa kubadili mambo na kusimamia nchi wanao ila hawana nia hiyo. Jiulize nchi kama Korea Kusini, Malaysia, Singapore au Indonesia

zimetupitaje kimaendeleo wakati miaka ya mwanzoni mwa uhuru tulikuwa karibu sawa tu. Patriotism haipo kabisa ndiyo maana leo tuko hoi kiasi hiki, ni hatari mno.

Tabia za viongozi zile zile ,mapolisi zile zile , wananchi zile zile wachache sana wana change wengi mh .
 
Baada ya hilo hapo kutokea leo..., nadhani Serikali isipotumia busara more of the same (au worse) itaendelea sana kutokea.. hususan population inavyozidi kuongezeka

Mkuu Serikali hii haina busara, maana wamepata nafasi chungu nzima za kutumia busara baada ya vilio vya Wananchi katika kona mbali mbali za nchi yetu lakini hakuna mabadiliko yoyote ili kubadilisha mwelekeo baada ya kusikia vilio hivyo. Naamini kabisa huko siku za usoni hali ndio itazidi kuwa mbaya katika ugomvi wa kugombea ardhi.
 
Hii heading yako mtoa mada imenifurahisha kweli,ingawa sijaweza connect vishoka na madalali hawa wa kitaa na jinsi serikali yetu ilivyo. Sijawahi kupata bahati ya ku operate kwenye ulimwengu wa madalali na vishoka

Mkuu huoni viongozi wetu wanazunguka kila mahali kunadi nchi (eti wawekezaji) huenda hapo kuna 10% yao..!!

Huoni issue za richmond na dowans..? Huoni issue za kununua magari (mashangingi) wangeweza kununu direct kutoka Kiwandani kwa punguzo ila wanatumia dealers na middle man...?

Huoni wakati wa uchaguzi yale mabango na matangazo yalitengenezwa wapi..? na nani alipewa tender..? na ili-cost kiasi gani na kama kweli wanapenda ajira za bongo kwanini hizo Bango wasipewa watu wa Bongo watengeneze ?

Sasa mkuu wamehamia kwenye ardhi kuuza/kugawa ardhi yetu kwa jina la "wawekezaji" sijui hapo hawa madalali wanapercent ngapi ?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom