ORCA ACE
JF-Expert Member
- Jan 18, 2020
- 1,448
- 1,706
Tuliambiwa hapa kazi tu. Imekuwa kinyume. Serikali hii ya Magufuli inaendelea kukopa pesa kwa matumizi yasiyo sahihi, kuna miradi inaendelea kufanywa bila idhini ya hilo bunge dhaifu la Ndugai. Huyu bwana naye amekuwa kichekesho.
Rais amekimbilia Chato wiki ya 7 bila ya maelezo ya kutosha (Kuna wapo wanaojaza mapovu kuwa rais ana haki ya kukaa popote. Mna matatizo ninyi ebu msome katiba inasema nini? Kuna wengine ni watukanaji ambao wapo kwenye payroll ya Polepole, nawataka hao watumie akili kidogo (kama wanazo) tunapojadili hili kwa maslahi ya nchi yetu.
Magufuli amekosa mikutano miwili ya SADC na EAC kujadili mambo muhimu ya kikanda, hatujui sababu. Magufuli hajawahi kwenda UN hata mara moja kwa kipindi alichokaa madarakani, aliyemwakilisha ni waziri asiye na experience yoyote na mahusiano ya kimataifa. Ni mtu wa ovyo anayejua diplomasia ya mitishamba, hakuna anachojua zaidi ya propaganda za levels za ujima.
Atakayesema kuwa hatujakosa lolote kwenye mikutano miwili ya EAC na SADC atakuwa ana shida kichwani, tena kubwa. Madereva wetu wanazuiwa mipakani kwenye nchi zinazotuzunguka, malori yapo mipakani na bidhaa (perishable) zinaendelea kuharibika na wengine ni wagonjwa hawapati matibabu bali wanarudishwa Tanzania kwenda kulundikwa lundikwa huko Amana au Mloganzila na kwenye makambi yasiyo na huduma.
Kwanini Magufuli anaficha namba za wanaougua? Madhara yake yanaeleweka vizuri. Tumekosa fedha za kukinga uchumi kutokana na madhara ya CORONA na kusaidia kuutokomeza ugonjwa wakati majirani zetu wamepewa. UKWELI NI KITU KIZURI SIKU ZOTE huyo Magufuli hajawahi kuwa mkweli.
Kwanini serikali inawazuia hata wafiwa waongelee huu ugonjwa? Je ni taboo kwa Wasukuma kuongelea ugonjwa? Kuna yanayoshangaza ambayo hayaeleweki. Wakati wa msiba wa Jaji Augustino Ramadhani, tuliwaona marais wastaafu wote pamoja na majaji wakuu/kiongozi wastaafu wa Tanzania/Zanzibar wote wakiwa wamevaa Masks, mbona Magufuli hakuonekana? Ana matatizo gani? Tunapaswa tujue kwa sababu sisi ndiyo tunaolipa mshahara wake.
Haya mambo ya kukwepa kwenda mikutano ya SADC, EAC, UN, AU, DAVOS hayaeleweki. Mwanzoni tuliambiwa anaogopa gharama, hizo gharama ni kubwa kiasi gani mbona Kabudi akienda UN anatumia gharama hizo hizo? Kama hata wakiongezeka walinzi watatu kwenye details yake, gharama zake ni kiasi gani? MAGUFULI USITUDANGANYE.
Tatizo kubwa inawezekana ni lugha ya Kiingereza haiwezi hata kidogo (Hizo theses zake sijui ziliandikwaje?) Haya ndiyo mambo ya undugunaizesheni hapo Mlimani yalivyo) Au ni tatizo la kiafya. Maana hatuelewi hivyo lazima tuhisi sababu. Angekuwa anakwenda halafu anatema yai, tungejua hilo si tatizo. Ila kuongea matusi anajua.
Ni rais wa nchi gani ana-control Bunge? Anawapangia cha kufanya, eti kisa Serikali ndiyo inatoa budget. Hajui hilo ni wajibu wa serikali kikatiba, Serikali kukusanya na kugawa budget siyo tija, hata bunge lingeweza kukusanya mapato, vile vile mahakama ingeweza. Magufuli anatumia mwavuli wa kutoa bajeti kwa mahakama na bunge ili kuwapa maelekezo ya kufanya, mmeona anayoyafanya, hakuna mahakama huru, tume huru, bunge huru (Eti spika anatuambia yeye ndiye mwenye uwezo wa kufukuza na kuwavua ubunge wabunge kwa sababu ndiye aliyewaapisha., ameshasahau na yeye ni mbunge na kama spika ana mipaka ya kazi yake....Atakumbukwa kwenye historia kama spika wa ovyo kutokea nchini kwetu)
LINI NCHI HII KUTAKUWA NA HAKI?
Ndugai anafanya analotaka, yeye kazi yake kubwa ni kumfurahisha Magufuli kwa kupokea maagizo yake. Ina maana Magufuli anamsaidia kufikiri na kuendesha Bunge. Hivi rais haoni aibu kusema kuwa "AMELIAGIZA BUNGE" kama ni wizara ya serikali. Au anavyoliagiza mahakama kumaliza kesi haraka ili awape pesa za kumalizia miradi ya kujenga mahakama.
HIVI MAGUFULI ANAELEWA CONCEPT YA 3-PILLARS?
Kama haelewi kwa nini washauri wake hawamueleweshi? Jaji mkuu naye ni mtu mwingine mwenye tatizo na legelege. Nilimshangaa analivyokuwa anakataa suala la Tundu Lissu lisichunguzwe na wachunguzi huru. Tangu lini Jaji mkuu anahangaika na uchunguzi? Kweli anajua kazi yake?
Kama kungekuwa na tume huru tusingepata hilo tatizo la kuwa na rais anayekimbia kimbia hovyo.
MADINI YA UKWELI, YOU HAVE SPOKEN IT ALL, SAFI SANA, 🙏🙏🙏🙏🙏