Serikali ya CCM mmeamua kutusaliti wananchi, Tunaenda kukumbwa na njaa kubwa hali ni mbaya

muafi

JF-Expert Member
Oct 6, 2015
2,115
4,801
Serikali ya CCM chini ya Rais Samia Imeamua kwa makusudi kutuacha watanzania na kuangali maslai yao.

Hali ni mbaya sana mtaani vyakula bei hazishikiki.

Vyakula vinavushwa mipakani na kwenda nje ya nchi sisi hatupati.

Imefika hatua sasa hivi mabwenyenye wananunua mzigo bado upo shambani wanavuna na kupeleka nje ya nchi, Kilimanjaro kuna njaa lakini mahindi yanapitia hapohapo kwenda Kenya.

Sasa hivi unga wa sembe kilo moja 2000 hii haijawai kutokea kabisa.

Mchele 2400 kilo

Serikali ipo kimya tu wao wana hela za kula.

CCM imeamua kutusaliti, sasa hivi sokoni hatuoni mahindi yanatoka kwenye stock yanawekwa kwenye maroli yanavuka boda.

Tukisema hivi wanaona kama tunatania maana wao hali ya mtaani hawaijui.

Sawa bwana.
 
Tulishauri mwaka huu mavuno ni kidogo wafunge mipaka kwani hata soko la ndani tu linatosha wakashupaza vichwa vyao.

Mavuno yakiwa mengi watu wauze nje ni sawa lakini mwaka wenye mavuno kidogo nao wauze nje kipindi chote hapana,

Burundi kuuza mahindi, maharage, mtama na muhogo ni uhujumu uchumi kwa sasa, Uganda kazuia hakuna kuuza chochote nje isipokua ni ruhusa kununua, na kuingiza ndani,

Rwanda kazuia kabisa hakuna kutoa hata kiazi, wizara ya kilimo ipo ipo tu imekalia siasa, hakuna usalama kama nchi haina chakula cha kutosha na mkumbuke dunia nzima mavuno kwa mwaka ulioisha yalikua hafifu sana, viongozi hawachukui maamuzi simply sababu wao na familia zao njaa haitowakumba.
 
Kwa nini vyakula vinashuswa mipakani na kwenda nje ya nchi na nchi hampati??

Kuna anayewazuia kununua kutoka kwa wafanyabiashara wa mazao na wakulima wanaouza??

Ukienda na pesa zako kwa mkulima wakati huu unataka gunia za mahindi kwa bei anayouza atakukatalia kwa sababu hutoki nje ya nchi?
Serikali ya CCM chini ya Rais Samia Imeamua kwa makusudi kutuacha watanzania na kuangali maslai yao

hali ni mbaya sana mtaani vyakula bei hazishikiki

Vyakula vinavushwa mipakani na kwenda nje ya nchi sisi hatupati

imefika hatua sasaivi mabwenyenye wananunua mzigo bado upo shambani wanavuna na kupeleka nje ya nchi, Kilimanjaro kuna njaa lakini mahindi yanapitia hapohapo kwenda kenya

Sasaivi unga wa sembe kilo moja 2000 hii haijawai kutokea kabisa

mchele 2400 kilo

Serikali ipo kimya tu wao wanahela za kula

CCM imeamua kutusaliti, sasaivi sokoni hatuoni mahindi yanatoka kwenye stock yanawekwa kwenye maroli yanavuka boda


tukisema hivi wanaona kama tunatania maana wao hali ya mtaani hawaijui

Sawa bwana
 
Kwa nini vyakula vinashuswa
mipakani na kwenda nje ya nchi na nchi hampati??
Kuna anayewazuia kununua
kutoka kwa wafanyabiashara
wa mazao na wakulima
wanaouza??
Ukienda na pesa zako kwa
mkulima wakati huu unataka
gunia za mahindi kwa bei
anayouza atakukatalia kwa
sababu hutoki nje ya nchi?
Unaongea na mfanyabiashara au na mlaji anayenunua mchele dukani kwa mangi?
 
Kumbuka kwamba kama wewe unavyofanya biasha upate faida, kilimo nacho ni biashara. Elewa kwamba sasa ni fursa ya mkulima kupata faida. Zingatia mkulima siyo punda wa taifa. Kama unaona vipi acha kupiga soga hapo mjini nenda kajilimie chakula chako.
Mkulima mwenyewe anakuambia hakuna aliyemsaidia wakati analima
So kila mtu apambane na hali yake

Ova
 
Wakati awamu ya nne, mkulima alipewa uhuru wa kuuza anapotaka. Ukawa mwanzo wa mkulima kupata faida. Kila mkulima akavutika kuongeza uzalishaji kwa kuongeza eka anazolima na kuongeza ubora kv mbolea, mbegu bora, kupanda kwa vipimo nk.

Faida katika kilimo ikawavutia waajiriwa kuingia ktk kilimo na baadaye wafanyabiara wakaingia. Hapo kilimo kikawa cha biashara na uzalishaji ukaongezeka maradufu.

Awamu ya tano ikaingia na mwelekeo kama wa mleta mada. Bei ya mazao ya chakula ikaporomoka. Wafanya biashara na waajiriwa wakajichomoa katika kilimo. Wakulima original wakapunguza eka na ubora wa kilimo mwaka hadi mwaka. Uzalishaji wa mazao ya chakula ukaporomoka sana.

Kwa mtu mwenye vision lazima atapenda model ya wamu ya nne. Mimi naipenda na mama anaipenda pia. Sababu inapaisha uzalishaji, mauzo nje ya nchi, mkulima na nchi inafaudika kwa uendelevu.

Kwa ambaye hana vision ataona karibu tu kama mtoa mada. Hilo lilitokea ktk awamu ya tano na kilimo cha mazao ya chakula kikakosa maana. Uzalishaji ukaporomoka vibaya.

Mwendelezo huo ungetufikisha mahali nchi isijitosheleze kwa chakula na kuanza kuagiza toka nje.

Sera ya mama ya kilimo cha chakula ni BORA ashikilie hapohapo.
 
Back
Top Bottom