Hali ni mbaya, waziri Bashe chukua hatua

Dkt Mwijuma

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2023
Posts
205
Reaction score
614
Huu ni mwezi May kuna baadhi ya maeneo yanafanya uvunaji wa mazao tayari, kanda ya ziwa wameshavuna mahindi 80% ya mashamba yao sasa hivi wapo wanaendelea na uvunaji wa mpunga ambao upo 40%

70% ya mazao yanayotumika sana nchini kwetu ni mahindi, mchele na maharage haipiti siku waTanzania 7 kati ya 10 wasitumie moja wapo ya haya mazao, Maeneo yanayolima sana ndio yapo kwenye uvunaji mda huu

Mikoa ya kiuzalishaji kama Ruvuma, Rukwa, Mbeya, Morogoro pia imeanza kuvuna mda huu lakini hatuoni bei ikishuka kwa asilimia kubwa, ikumbukwe nchi yetu inapata mvua vipindi viwili tu kwa mwaka (vuli na masika) vuli hutangulia kuanzia september mpaka disember (maanaake vuli imeshapita) sasa tupo mwishoni mwa mvua za masika mvua hizi zilianza mwezi february na zitaisha rasmi mwishoni mwa mwezi huu

Asilimia kubwa ya wakulima tulokuwa nao nchini wanategemea mvua na hapa tukubaliane kwamba hatutapata tena mda wa kuzalisha mazao mengine mpaka mwishoni mwa mwaka, maanaake mazao haya yaliyopo yanatakiwa yatupeleke mpaka mwaka kesho mwezi kama huu

Kama wakulima wapo wanavuna shambani lakini bei hazishuki na hii inatoa picha kabisa kuwa mazao yaliyopatikana msimu huu bado ni kidogo na bahati mbaya wakulima walokuwa wengi wanauzia mazao shambani maanake tayari wafanyabiashara wa mazao mameshajimilikisha mazao ya msimu huu

Nimepita baadhi ya maeneo haswa kanda ya ziwa mkoani Geita halmashauri ya Geita DC mpunga unavunwa bei ya mchele imepungua lkn sio kwa ukubwa huo huko kg 1 ya mchele wanauza kwa Tsh 2000- Tsh 2500 hii ni bei ya mchele mpya kutoka shamba tuna mwezi mmoja na nusu tu wa uvunaji hali ni mbaya

Hapa serikali inatakiwa izuie moja kwa moja soko la nje, tusijidanganye kuwa tunamsaidia mkulima tutaua watu kwa njaa, kama mwezi may bei ni hii vipi mwezi disember? Soko la ndani bado ni kubwa sana linatosha kuuza mazao ikiruhusiwa mazao kwenda nje trust me mazao hayatashikika

Inawezekana serikali inataka kuvutia watu waingie kwenye kilimo sawa lkn lazima tuwe na mgawanyo wa kazi, watu walime mazao tupate chakula, watu wasome tupate wataalamu, watu wafanye michezo tupate wacheza mpira, riadha ndodi nk

Kuna watu wengine hawawezi kujikita kwenye kilimo ila wanachangia ukuaji wa uchumi wa nchi kwa mambo mengine, hebu tuwawazie vijana wanaojenga majengo (mafundi) wanajitoa sana kuijenga nchi yetu tumeona kilichofanyika Dodoma mji unajengwa kweli kweli, vijana hawa kipato chao kipo pale pale hata mh Rais hajagusia masilahi yao leo hii pale Morogoro ataweza kununua chakula kikipanda bei ikiwa pesa anayolipwa ni ile ile miaka yote

Tusichukulie poa hali itakuwa mbaya sana kuanzia mwezi september mwaka huu
 
N muda wa wakulima kutajirika...vjn wapo mjn wanauza vwembe hawatak kulima...serikali isiingilie swala hili...atakayekufa njaa na afe... BASHE ALISEMA KBS HAWATAINGILIA KAT BEI YA MAZAO..watu tumekuwa tukiwekeza kwenye kilimo lkn outcome miaka yote n ndogo achaaa kila mtu ashinde mechi zake...over
 
  • Je unajua gharama ya kulima heka moja ya mahindi, mpunga, maharage n.k?
  • Je gharama za kilimo zinarudishwa kwa bei ya soko kwa sasa?
  • Kulima si hisani inayofanywa na NGO's ndg; ni uwekezaji.
  • Vijana wawezeshwe kulima ili uzalishaji ukue; na bei uwe inatabirika si kuzipa promo bidhaa za mchina: bodaboda
 
Mpaka mda huu nipo field mkuu nakuhakikishia hakuna mkulima ananufaika na hatua hii kuna watu wapo shambani wananunua mazao kisha wayahifadhi kisha wayauze,

Kufanya kilimo cha ufanisi kikulipe ni lazima uwe na mtaji usiopungua milion 4 ni kijana yupi atatoka mjini akalime kwa mtaji huo?

Siku zote wakulima watakao baki ni hawa hawa tulionao ambao wana mitaji ya laki 5 mpaka milion 1 wanaolima ekari moja mpaka 2 kwa msimu

Najua ww inawezekana hujawahi kufanya kilimo thats why unaongea, mda huo unafanya kilimo kuna vitu vitasimama kwa mtu mwenye mtaji huo wa laki 5 - mil 1 huwezi kuendesha kilimo bila ww kuhusika moja kwa moja

Hii ndio inapelekea kukopa na deni linalipwa moja kwa moja na mazao, hawa wakulima wanaolima ekari 200 na kuendelea ni wachache sana nchi hii

Mitaji hakuna mkuu,, hawa unaowataka watoke mjini warudi wakalime kijijini huenda huko mjini wamejiajiri kwa mtaji wa laki 2 na kitu tu pesa ambayo huwezi kuiweka kwenye kilimo

Lkn ni lazima watu wote waende shamba? Kwanini tusiwe na mgawanyo? Inchi inategemea Uvuvi, Madini, Biashara, Sekta kama Utalii tuna wa walimu, madaktari, wahandisi unataka watu wote walime
 
  • Je unajua gharama ya kulima heka moja ya mahindi, mpunga, maharage n.k?
  • Je gharama za kilimo zinarudishwa kwa bei ya soko kwa sasa?
  • Kulima si hisani inayofanywa na NGO's ndg; ni uwekezaji.
  • Vijana wawezeshwe kulima ili uzalishaji ukue; na bei uwe inatabirika si kuzipa promo bidhaa za mchina: bodaboda
Nakubaliana na wewe mkuu, kiukweli gharama za uzalishaji ni kubwa sana lkn bado bei ya mazao pia ni kubwa sana

Serikari inahaja ya kupunguza ama kuondoa kabisa kodi ya bidhaa za uzalishaji wa kilimo na sana sana ni mbolea, mbegu, na madawa ya kuulia wadudu
 
Mpaka mda huu field mkuu nakuhakikishia hakuna mkulima ananufaika na hatua hii kuna watu wapo shambani wananunua mazao kisha wayahifadhi kisha wayauze,

Kufanya kilimo cha ufanisi kikulipe ni lazima uwe na mtaji usiopungua milion 4 ni kijana yupi atatoka mjini akalime kwa mtaji huo?

Siku zote wakulima watakao baki ni hawa hawa tulionao ambao wana mitaji ya laki 5 mpaka milion 1 wanaolima ekari moja mpaka 2 kwa msimu

Najua ww inawezekana hujawahi kufanya kilimo thats why unaongea, mda huo unafanya kilimo kuna vitu vitasimama kwa mtu mwenye mtaji huo wa laki 5 - mil 1 huwezi kuendesha kilimo bila ww kuhusika moja kwa moja

Hii ndio inapelekea kukopa na deni linalipwa moja kwa moja na mazao, hawa wakulima wanaolima ekari 200 na kuendelea ni wachache sana nchi hii

Mitaji hakuna mkuu,, hawa unaowataka watoke mjini warudi wakalime kijijini huenda huko mjini wamejiajiri kwa mtaji wa laki 2 na kitu tu pesa ambayo huwezi kuiweka kwenhe kilimo

Lkn ni lazima watu wote waende shamba? Kwanini tusiwe na mgawanyo? Inchi inategemea Uvuvi, Madini, Biashara, Sekta kama Utalii tuna wa walimu, madaktari, wahandisi unataka watu wote walime
Swala si kuangalia scale wala una mtaji kiasi gn...vjn wengi hawapendi kaz ngumu na hawana elimu..... Swala la ulanguz lipo nakubali lkn nakuambia wakulima wengi japo hatuna wale wa hectares 200 weng faham znarejea ....mm bnafs nmekuwa nkilima mahnd toka niajiliwe...na nmekuwa nki buy alizet tonnes kazaa kila mwaka ....nenda ndan ndan uko huwez kumwibia sn mkulima ... nowadays hata vjjn unakuta mtu kabak IST,NOAH baada ya kuuza mazao bodaboda sihesabu hz sasa n kama baiskel tuuu.....

Sasa hawa unaosema wana mitaj ya laki mbili hata kumilik bike n ndoto. Kumbuka kuna vjj watu wanalima bila hata mbolea na wanapata...eg njombe, mbeya, songea etc ...mm hiyoo laki 2 npe alafu nkuoneshe mwez wa 6 kipind cha mavuno outcome yake..
 
ilikuaje akawa Waziri huyu, Mtu ana asili ya Somalia ameoa mwenye asili ya Rwanda na anaingia baraza letu la Mawaziri akishikilia wizara uti wa mgongo wa Taifa
Mbona kuna wenye asili ya nchi hii kwa 100% na bado wanapiga dili tu na hawana cha ziada? Tujadili utendaji wake maana asili yake haihusiani na utendaji wake wizarani
 
Swala si kuangalia scale wala una mtaji kiasi gn...vjn wengi hawapendi kaz ngumu na hawana elimu..... Swala la ulanguz lipo nakubali lkn nakuambia wakulima wengi japo hatuna wale wa hectares 200 weng faham znarejea ....mm bnafs nmekuwa nkilima mahnd toka niajiliwe...na nmekuwa nki buy alizet tonnes kazaa kila mwaka ....nenda ndan ndan uko huwez kumwibia sn mkulima ... nowadays hata vjjn unakuta mtu kabak IST,NOAH baada ya kuuza mazao bodaboda sihesabu hz sasa n kama baiskel tuuu.....

Sasa hawa unaosema wana mitaj ya laki mbili hata kumilik bike n ndoto. Kumbuka kuna vjj watu wanalima bila hata mbolea na wanapata...eg njombe, mbeya, songea etc ...mm hiyoo laki 2 npe alafu nkuoneshe mwez wa 6 kipind cha mavuno outcome yake..

Mkuu nadhan ww utakuwa ni motivation speaker unaongea lugha laini sana, hiyo laki 2 ongea na mtu ambaye ana eneo tayari sio huyu ambae hana lazima akodi kutoka kwa mmiliki, watu wanakwepa kufanya vitu vinavyohitaji uwekezaji mkubwa,, kilimo sio kigumu wala kama unavyosema mm naamini ugumu upo kwenye mtaji

Mjini kazi ni ngumu kupita maelezo, mji kama Dar watu wanaamka saa 11 alfajiri na kulala saa 7 usiku mwaka mzima,, niambie ni kijiji gani watu wanaishi hivii? Mtu anapandisha juu ghorofa ya tano kifusi cha mchanga kilichomwagwa na lori (mende), hesabu kilometa anazotembea machinga kwa siku hawa hawashindwi kufanya kilimo bali hawana mitaji

Lkn jambo la msingi na ndio lengo la uzi huu serikali iangalie ni namna gani ya ku-balance bei za mazao bila kuathiri soko (walaji) na pia mkulima,, hatuwezi kulima wote na hata tukilima wote tutamuuzia nani ikiwa kila mtu ana mazao?
Sekta zote zinatakiwa zifanye kazi,, mda huo ww unalima kuna utalii, uchimbaji madini, uvuvi nk
 
Hivi ukiambiwa utaje mikoa inayo lima mpunga utaitaja Geita ?
Mchele huwa unakuwa mwingi na kushuka bei baada ya mikoa ya Tabora,Mbeya na Morogoro kuivisha na mavuno kwenye hii mikoa huwa ni kuanzia mwezi wa 5 .
 
Mimi nadhani, superpowers Kama USA ndo wanatufundisha namna ya kufanya maamuzi, moja ya masharti ya demokrasia Ni kuacha soko lijipangie bei yenyewe, serikali isiingilie, hivyo huenda Bashe Hana kauli hapo.
 
Mbona unalialia kwa hiyo hutaki wakulima tulambe asali kaa kwa kutulia sisi bado tunataka Bei iongezeke kwa taarifa yako hao unao waita wakulima ni wanakijiji , wakulima tupo mjini tunasafirisha mazao yetu unasema wafanya biashara eti?
 
Hakuna cha bei kushuka,kama mnaona rahisi kulima anzeni kulima na nyinyi, mazao yakilimwa kwa wingi yatajishusha bei yanyewe ,Bashe hawezi kunipangia bei ya mpunga/mahindi niliyolima mimi.
Na mwaka huu serikali msifunge mipaka Wacha wakulima tupeleke mazao yetu tutakako.
 
Huu ni mwezi May kuna baadhi ya maeneo yanafanya uvunaji wa mazao tayari, kanda ya ziwa wameshavuna mahindi 80% ya mashamba yao sasa hivi wapo wanaendelea na uvunaji wa mpunga ambao upo 40%

70% ya mazao yanayotumika sana nchini kwetu ni mahindi, mchele na maharage haipiti siku waTanzania 7 kati ya 10 wasitumie moja wapo ya haya mazao, Maeneo yanayolima sana ndio yapo kwenye uvunaji mda huu

Mikoa ya kiuzalishaji kama Ruvuma, Rukwa, Mbeya, Morogoro pia imeanza kuvuna mda huu lakini hatuoni bei ikishuka kwa asilimia kubwa, ikumbukwe nchi yetu inapata mvua vipindi viwili tu kwa mwaka (vuli na masika) vuli hutangulia kuanzia september mpaka disember (maanaake vuli imeshapita) sasa tupo mwishoni mwa mvua za masika mvua hizi zilianza mwezi february na zitaisha rasmi mwishoni mwa mwezi huu

Asilimia kubwa ya wakulima tulokuwa nao nchini wanategemea mvua na hapa tukubaliane kwamba hatutapata tena mda wa kuzalisha mazao mengine mpaka mwishoni mwa mwaka, maanaake mazao haya yaliyopo yanatakiwa yatupeleke mpaka mwaka kesho mwezi kama huu

Kama wakulima wapo wanavuna shambani lakini bei hazishuki na hii inatoa picha kabisa kuwa mazao yaliyopatikana msimu huu bado ni kidogo na bahati mbaya wakulima walokuwa wengi wanauzia mazao shambani maanake tayari wafanyabiashara wa mazao mameshajimilikisha mazao ya msimu huu

Nimepita baadhi ya maeneo haswa kanda ya ziwa mkoani Geita halmashauri ya Geita DC mpunga unavunwa bei ya mchele imepungua lkn sio kwa ukubwa huo huko kg 1 ya mchele wanauza kwa Tsh 2000- Tsh 2500 hii ni bei ya mchele mpya kutoka shamba tuna mwezi mmoja na nusu tu wa uvunaji hali ni mbaya

Hapa serikali inatakiwa izuie moja kwa moja soko la nje, tusijidanganye kuwa tunamsaidia mkulima tutaua watu kwa njaa, kama mwezi may bei ni hii vipi mwezi disember? Soko la ndani bado ni kubwa sana linatosha kuuza mazao ikiruhusiwa mazao kwenda nje trust me mazao hayatashikika

Inawezekana serikali inataka kuvutia watu waingie kwenye kilimo sawa lkn lazima tuwe na mgawanyo wa kazi, watu walime mazao tupate chakula, watu wasome tupate wataalamu, watu wafanye michezo tupate wacheza mpira, riadha ndodi nk

Kuna watu wengine hawawezi kujikita kwenye kilimo ila wanachangia ukuaji wa uchumi wa nchi kwa mambo mengine, hebu tuwawazie vijana wanaojenga majengo (mafundi) wanajitoa sana kuijenga nchi yetu tumeona kilichofanyika Dodoma mji unajengwa kweli kweli, vijana hawa kipato chao kipo pale pale hata mh Rais hajagusia masilahi yao leo hii pale Morogoro ataweza kununua chakula kikipanda bei ikiwa pesa anayolipwa ni ile ile miaka yote

Tusichukulie poa hali itakuwa mbaya sana kuanzia mwezi september mwaka huu
Dkt Mwijuma na wapumbavu wenzio, toka hapa JF nenda ukalime uone mkulima anavyoteseka kuliko kupoteza MBs humu kuandika utumbo.

Mkulima wa Tanzania asipangiwe bei na mtu yeyote!! Unataka bei ziterrmke ili iweje?

Kuanzia mwaka juzi toka Hussein Bashe awe Waziri wa Kilimo alisema muache mkulima amuuzie mtu anayempa bei nzuri!! Nashangaa badala ya kwenda kulima mchangamkie fursa ya bei nzuri instead mnataka kurudisha maisha ya wakulima nyuma.

Wacheni UJINGA
 
Hivi ukiambiwa utaje mikoa inayo lima mpunga utaitaja Geita ?
Mchele huwa unakuwa mwingi na kushuka bei baada ya mikoa ya Tabora,Mbeya na Morogoro kuivisha na mavuno kwenye hii mikoa huwa ni kuanzia mwezi wa 5 .
Kanda ya ziwa mkoa unaoongiza kwa uzalishaji wa mahindi ni Mara wilaya ya Tarime,, Kagera ina hali nzuri sana ila hawajawekeza kwenye kilimo cha mahindi

Ukiachana na hiyo mikoa hakuna mkoa unaizidi Geita,, Geita inapokea mvua vipindi viwili kwa mwaka wakati Geita ina eneo la ukubwa wa zaidi ya ekari 2000 na zote zipo eneo moja kama kuna mtu wa Geita atakuwa anakifahamu kijiji cha Ibanda ambacho kinapaka na Kijiji cha Igaka upande wa Sengerema
 
Dkt Mwijuma na wapumbavu wenzio, toka hapa JF nenda ukalime uone mkulima anavyoteseka kuliko kupoteza MBs humu kuandika utumbo.

Mkulima wa Tanzania asipangiwe bei na mtu yeyote!! Unataka bei ziterrmke ili iweje?

Kuanzia mwaka juzi toka Hussein Bashe awe Waziri wa Kilimo alisema muache mkulima amuuzie mtu anayempa bei nzuri!! Nadhangaa badala ya kwenda kulima mchangamkie fursa ya bei nzuri instead mnataka kurudisha maisha ya wakulima nyuma.

Wacheni UJINGA
Kwanza mimi hakuna sehemu nimemtukana mtu hapa, naamini kwenye kujadili jambo kwa hoja haijalishi mtu kaleta hoja inayokinzana nitajibu kwa hoja na sio kutoa matusi

Pili kilimo ni sehemu ya maisha yangu, naamini kushiriki kilimo sio lazima nikalime hata nikikuletea pembejeo kuzitoa mjini kukusogezea kujijini nitakuwa nimeshiriki kilimo

Lengo la huu uzi sio kumuathiri mkulima kwenye suala la bei no, nilikuwa nawasilisha hoja kuhusu uhaba/uchache wa mavuno msimu huu serikali idhibiti soko mazao yasiuzwe yote kwa haraka soko la nje ilihali soko la ndani bado linauhitaji

Chakula kilichopo hakitoshi kwa humu humu ndani vipi tena kiende nje,, serikali ifunge mipaka kiuzwe hapa pekee

Harafu narudia tena hatuwezi kulima wote mkuu, unataka walimu, madaktari, mapolisi, wavuvi, wahandisi, wafanyabiashara watu wa madini na utalii wote waende shamba?
 
Back
Top Bottom