KERO Serikali, Watu wanazidi kujenga kuzunguka Uwanja wa Mpira wa Ikhanga-Igawilo Mbeya

KERO Serikali, Watu wanazidi kujenga kuzunguka Uwanja wa Mpira wa Ikhanga-Igawilo Mbeya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mel James

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2015
Posts
367
Reaction score
298
Habari ndugu zangu!

Naomba kuwakilisha malalamiko kwa serikali kuangalia upya eneo linalozunguka uwanja wa mpira ambao ni mali ya serikali pia lipo chini ya halmashauri ya jiji la Mbeya.

Uwanja huu ni mkongwe sana jijini Mbeya. Umetumiwa na timu kubwa kama yanga, simba wakija Mbeya kama kambi ya maficho ya mazoezi ya mda mfupi timu hizi zikiwa na mechi kubwa Mbeya.

KIpindi Mbeya City FC, ipo vizuri ilikuwa ndo uwanja wake wa mazoezi. Uwanja ulikuwa ni mkubwa sana na uliwekwa reserve na Jiji Mbeya maana upo sehemu nzuri sana. Cha ajabu nyumba zinazidi kujengwa na zimefikia kabisa uwanja huo kiasi kwamba hata kuweka fence uwanjani hapo ni ngumu kwa sasa.

Sehemu za kusimama mashabiki kote nyumba zinazunguka zikijengwa na serikali ya mtaa inazidi kuuza maeneo hayo ikishirikiana na machifu na mwenyekiti wa mtaa. Tunaomba serikali mfike eneo husika kabla uwanja hujaisha. Wavamizi watolewe wote uwanja hurudi kwa jiji.

Viwanja vya mazoezi ni muhimu sana kwa maeneo ya mjini. Hatuwezi pata vipaji kama hatuna viwanja. Waziri wa michezo tunaomba urudishe uwanja huu.
 
Serikali yako kwenye suala la usimamizi wa mipango miji walishanyoosha mikono juu.
 
Back
Top Bottom