The lost
JF-Expert Member
- Jul 3, 2017
- 2,695
- 8,209
Kulingana na ombwe kubwa la ajira kwa vijana wengi serikali iruhusu mfumo wa ajira kuwa tofauti kidogo. Jana TAMISEMI wametoa takwimu kwa waombaji wa nafasi elfu 6 za ualimu kuwa mpaka jana tarehe 22 ni waombaji zaidi ya elf 87.! Hii ni zaidi ya hatari na ni hatari na huko mbeleni wanasiasa watakuja kuona moto usio wa kawaida. Unafanyaje sampling ya watu elfu 6 kutoka kwa watu elfu 87 wenye sifa sawa? afya watu 2700 waliokamilisha maombi mpaka jana 31000 hii ni hatari kwa usalama wa taifa. Serikali ruhusuni halmashauri ziwaajiri hawa vijana nafasi mbalimbali kama vile utendaji wa kijiji, uafsa maendeleo, wataalamu wa tehama, na kada nyingine wanazoweza kuzimudu.