Serikali ruhusuni wahitimu wa kada ya elimu kuajiriwa sekta nyingine mfano uafisa mtendaji wa kijiji, maafisa maendeleo etc.

THE LOST

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
1,584
2,000
Kulingana na ombwe kubwa la ajira kwa vijana wengi serikali iruhusu mfumo wa ajira kuwa tofauti kidogo. Jana TAMISEMI wametoa takwimu kwa waombaji wa nafasi elfu 6 za ualimu kuwa mpaka jana tarehe 22 ni waombaji zaidi ya elf 87.! Hii ni zaidi ya hatari na ni hatari na huko mbeleni wanasiasa watakuja kuona moto usio wa kawaida. Unafanyaje sampling ya watu elfu 6 kutoka kwa watu elfu 87 wenye sifa sawa? afya watu 2700 waliokamilisha maombi mpaka jana 31000 hii ni hatari kwa usalama wa taifa. Serikali ruhusuni halmashauri ziwaajiri hawa vijana nafasi mbalimbali kama vile utendaji wa kijiji, uafsa maendeleo, wataalamu wa tehama, na kada nyingine wanazoweza kuzimudu.
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
14,753

Bila kufanya ''restructuring'' kubwa kabisa kwenye yenye kuleta maumivu makubwa hasa kwa wanasiasa nchi yetu itazidi kwenda kusikojulikana. Mfumo wetu wa utawala na elimu na namna ya kuwapata viongozi au kuwateua inabidi ibadilishwe kabisa. Siasa na wanasiasa wamejaa kila kona na ndiyo wenye uamuzi na ''utaalam'' wa kila jambo. Mabalozi, wabunge na wateule wengine wanateuliwa kwa kushangaza kila rais anayeingia anaingia na ''timu kula-kula'' yake. Kinachotakiwa ni wanasiasa kupunguzwa kwa idadi na nguvu zao za maamuzi ziwe limited. Hawa waombaji wanaokushangaza hawajuzuka kwa bahati mbaya bali ni matokeo ya mipango mibovu ya kufungua ''vyuo vikuu'' na shule visivyo na sifa ambavyo vilikuwa vinatoa vilaza badala ya wahitimu.
 
Bensonben

Senior Member
Jul 3, 2015
183
500

Daaaaah hivi ni kwann wanaopewa kipaumbele ni walim na watu wa afya pekee yao!! Mbona kila kada ina watu kibao tu mitaani huko hawana ajira!
 
THE LOST

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
1,584
2,000
Daaaaah hivi ni kwann wanaopewa kipaumbele ni walim na watu wa afya pekee yao!! Mbona kila kada ina watu kibao tu mitaani huko hawana ajira!
Mkuu huko wengine wameshajiongeza tofauti na wadogo zetu hawa, sijui sababu ni mitaala yao vyuoni ama nini. Angalia hata wanaoathirika na mfumo wa ajira kwa wingi ni sekta hizi mbili ambazo mwajiri wao mkuu ni serikari tofauti na wahandisi, wajiolojia, wahasibu etc.
 
coolboyjden

JF-Expert Member
Apr 10, 2021
280
500
dah watu ni wengi kweli wanaingia ×15 sio poa
ila naona pia kuna watu hp wameajiriwa na private sector ila kwakua serekali ndio ajira ya uhakika basi lazima waongeze idadi hp ingekua vzuri kutambua idadi kabisa ya wahanga wasio na mbele wala nyuma
serekali ingekaa na hao watu ijue inawaongezeaje ujuzi na misaada mingine yakufanya ili wapate vyakufanya vyenye uhakika na ubunifu ili ajira zikitakangazwa watu wasiwe wengi hvy kwakua watakuwa na imani wanacho kifanya.
kuna watu wanajisifu wamejiajiri alafu ajira ikitoka na yy anakimbizana hko tunakua tumegeuza kijiajiri nisehemu yakuzugia kusubir ajira.
 
road master

JF-Expert Member
Jun 11, 2020
1,825
2,000
Bila kufanya ''restructuring'' kubwa kabisa kwenye yenye kuleta maumivu makubwa hasa kwa wanasiasa nchi yetu itazidi kwenda kusikojulikana. Mfumo wetu wa utawala na elimu na namna ya kuwapata viongozi au kuwateua inabidi ibadilishwe kabisa. Siasa na wanasiasa wamejaa kila kona na ndiyo wenye uamuzi na ''utaalam'' wa kila jambo. Mabalozi, wabunge na wateule wengine wanateuliwa kwa kushangaza kila rais anayeingia anaingia na ''timu kula-kula'' yake. Kinachotakiwa ni wanasiasa kupunguzwa kwa idadi na nguvu zao za maamuzi ziwe limited. Hawa waombaji wanaokushangaza hawajuzuka kwa bahati mbaya bali ni matokeo ya mipango mibovu ya kufungua ''vyuo vikuu'' na shule visivyo na sifa ambavyo vilikuwa vinatoa vilaza badala ya wahitimu.
Kumbuka huko pia kuna watu lukuki wamesomea hizo fani wamejazana mtaani!??
 
kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,619
2,000
Kuna changamoto nyingi sana.

Wakati afya idadi hiyo kubwa wameomba kazi,huku mtaani unakuta kuna watu wameajiri watu wasio na elimu ya afya wala kozi yoyote kwenye maduka ya dawa tena yale makubwa.Wakaguzi wakienda wanaambiwa ni wahasibu.Unakuta famasi moja ina wahasibu feki 6 na mtaalamu mmoja.Wakati mwingine hakuna mtaalamu yoyote ila kuna cheti chake tu.

Kwa elimu najua wengi walio private wameomba hasa baada ya funzo la corona mwaka jana.Taasisi za elimu zilifungwa na kukuta watu wamenyimwa mshahara.Pia dhuluma nyingi huko private na hakuna anayejali.
Naona ipo haja ya kuwepo mjadala mpana juu ya serikali na mamlaka kuhusu suala la ajira
Kulingana na ombwe kubwa la ajira kwa vijana wengi serikali iruhusu mfumo wa ajira kuwa tofauti kidogo. Jana TAMISEMI wametoa takwimu kwa waombaji wa nafasi elfu 6 za ualimu kuwa mpaka jana tarehe 22 ni waombaji zaidi ya elf 87.! Hii ni zaidi ya hatari na ni hatari na huko mbeleni wanasiasa watakuja kuona moto usio wa kawaida. Unafanyaje sampling ya watu elfu 6 kutoka kwa watu elfu 87 wenye sifa sawa? afya watu 2700 waliokamilisha maombi mpaka jana 31000 hii ni hatari kwa usalama wa taifa. Serikali ruhusuni halmashauri ziwaajiri hawa vijana nafasi mbalimbali kama vile utendaji wa kijiji, uafsa maendeleo, wataalamu wa tehama, na kada nyingine wanazoweza kuzimudu.
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
14,753
2,000
Kuna changamoto nyingi sana.

Wakati afya idadi hiyo kubwa wameomba kazi,huku mtaani unakuta kuna watu wameajiri watu wasio na elimu ya afya wala kozi yoyote kwenye maduka ya dawa tena yale makubwa.Wakaguzi wakienda wanaambiwa ni wahasibu.Unakuta famasi moja ina wahasibu feki 6 na mtaalamu mmoja.Wakati mwingine hakuna mtaalamu yoyote ila kuna cheti chake tu.

Kwa elimu najua wengi walio private wameomba hasa baada ya funzo la corona mwaka jana.Taasisi za elimu zilifungwa na kukuta watu wamenyimwa mshahara.Pia dhuluma nyingi huko private na hakuna anayejali.
Naona ipo haja ya kuwepo mjadala mpana juu ya serikali na mamlaka kuhusu suala la ajira
Ni hatari sana hasa hili suala la Pharmacy au Hospital/Maabara kuajiri watu wasio na ujuzi. Usimamizi wa serikali ni mbovu na wa kizembe hivyo unatoa mwanya kwa wamiliki wa Phamarcies na Hospital binafsi kuweka watu wasio na ujuzi kwa sababu wanataka kuwapa ndugu zao ajira au malipo ni kidogo.
 
Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
9,449
2,000
Kama tukitumia akili ya kulalamika basi kila siku kazi iitakuwa nikuwasihi na kuwaomba serikali watusaidie kutatua kero ya ajira ile hali serikali yenyewe inaendeshwa na watu kama wewe na mimi.

Hebu tazama juzi tu akina mama lwakatale walikuwa hapo bungeni, leo hadi akina babu tale na Mwanafa sasa hivi wapo bungeni.

Sasa tukiendelea na huu utaratibu tusubirie akina shilole Joyce kiria, steve nyerere, akina kingwendu na akina swebe ndio wakawe wabunge wetu kutuongelea.

Nachotaka kusema ni kuwa kada ya vijana wa kisasa hatupo serious na maisha yetu. These so called leaders, kama kweli ni leaders then they are leading fools. Sababu only a fool leader will lead fools.

Madhara hatuwezi yaona sasa, but in the next 30 to 40 years from now. Retirement age ikifika. Tutakapokuwa wazee wa miaka 50+ tukiitafuta 60, 70, 80 na 90 kama huo mwili utaruhusu ndipo tutaona gharama ya kucheka na hawa jamaa wanaojiia politicians kwenye shughuli zetu za maendeleo.

Kwasasa tuendelee kuwachekea wakati wanachezea pesa zetu vile wanavyojiskia. Wakati mkilalamika kukosa ajira na vipato, wenzenu kodi inayokusanywa plus misaada wanayopewa kupitia jina la nchi na pia wanapouza na kuweka rehani rasilimali zetu kwa visingizio vya kututafutia maisha bora, tazama wao wanaishi vipi?! Kuanzia wapinzani na chama tawala. Tazama wanavyomumunya pesa zetu kama vile ubuyu wa zanzibar huku wakitufariji kinafiki.

Hebu fuatilia mishahara ya viongozi wote kuanzia rais, mawaziri na manaibu wao, makatibu wizara etc, wabunge, wakuu wa mikoa na wilaya, halafu ujiulize je na wao wanavumilia shida au kuishi kwa matumaini?!

Siku wananchi, especially kada ya wasomi, tutakapoanza kuhoji matumizi ya pesa zetu every single senti inayokusanywa na serikali kuwa inakwenda wapi then it's the day tutaanza kupiga hatua kumaliza mjadala juu ya ajira. Kimya chenu kutohoji ndicho kinachofanya jamaa kuwa na ujasiri wa kukaa kimya na kukaushia issue ya kukosekana ajira.
 
900 Inapendeza zaidi

JF-Expert Member
Nov 19, 2017
3,950
2,000
Kulingana na ombwe kubwa la ajira kwa vijana wengi serikali iruhusu mfumo wa ajira kuwa tofauti kidogo. Jana TAMISEMI wametoa takwimu kwa waombaji wa nafasi elfu 6 za ualimu kuwa mpaka jana tarehe 22 ni waombaji zaidi ya elf 87.! Hii ni zaidi ya hatari na ni hatari na huko mbeleni wanasiasa watakuja kuona moto usio wa kawaida. Unafanyaje sampling ya watu elfu 6 kutoka kwa watu elfu 87 wenye sifa sawa? afya watu 2700 waliokamilisha maombi mpaka jana 31000 hii ni hatari kwa usalama wa taifa. Serikali ruhusuni halmashauri ziwaajiri hawa vijana nafasi mbalimbali kama vile utendaji wa kijiji, uafsa maendeleo, wataalamu wa tehama, na kada nyingine wanazoweza kuzimudu.
walimu wengine hata hawajui kutype barua ya kuomba ajira kutumia pc sasa na TEHAMA wapi na wapi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom