Barua ya wahitimu wa chuo kada ya Ualimu kwa TAMISEMI

kimeumana

Member
May 12, 2020
10
6
AJIRA 5000 ZA WALIMU AMBAZO KIBALI CHAKE KILITOLEWA NA HAYATI DR. JPM ZIMEISHIA WAPIII?swali kwa TAMISEMI chini ya waziri UMMY MWALIMU!

#Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan,

#Katibu mkuu kiongozi muheshimiwa Katanga,

#Waziri Mkuu wa JMT, Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa.

#Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu,

#Waziri wa Elimu prof. Joyce Ndalichako.

#Makatibu na wakurugenzi wakuu wote Waliopo TAMISEMI wizara ya elimu na utumishi kwa WALIMU!

#WALIMU (wahusika na wahanga wakuu)

ITIFAKI IMEZINGATIWA!!!🙏🏾

Nawasalimu kwa jina la JMT!🎤
Na KAZI IENDELEE KAMA KAWAIDA!

Moja kwa moja bila kupoteza muda naomba tuhusike na kichwa tajwa hapo juu!

Ukiachana na hizi ajira elfu sita alizotangaza muheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan,
Kumekua na sintofahamu na kizungumkuti juu ya namna ya utoaji wa ajira, zaidi zaidi katika kada ya walimu ambapo wizara yenye dhamana ya kushughulikia suala hili ni wizara ya elimu TAMISEMI! _Sisi walimu tulio mitaani na makaratasi yetu ya degree tunaelewa ugumu tunaopitia katika suala zima la ajira! Tukumbushane kua mwaka Jana tarehe 07/09/2020 hayati Dr JPM alitoa vibali vya ajira 13000 ambapo mwanzoni kabisa zilivumishwa kua zitakua 13526 Ambapo hatujui hizo 526 zilipoteaje! katika mchakato wake chini ya wizara ya elimu TAMISEMI zilitoka ajira za walimu 8000 ambao mpaka sasa wapo wanaendelea na kazi. Hizo 8000 Eng. Joseph Nyamhanga na jopo lake la waajiri chini ya waziri Jafo wakati huo walizitolea tamko wiki moja baadaye kua ni awamu ya kwanza na hivyo awamu ya pili ambazo ni ajira 5000 zitatolewa mapema kabla ya mwaka wa fedha wa serikali kuisha yaani 2020/21.

LAKINI CHA AJABU ni kwamba hizo ajira 5000 ukiachana na hizi 6000 alizotangaza muheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan zimekua na sintofahamu kubwa sana hazieleweki ni lini mchakato wake utaanza na majina ya walimu walioajiriwa yatatoka lini, na kama zimekwishatoka zilitokaje na katika mfumo UPI? Kama WIZARA inafanya kazi kimyakimya iweke wazi, kama walishagawana watuambie kua hizo 5000 tulishazitoa na majina watupe tuyaone!!!
Code:
*_LAKINI pia waziri mkuu Kasim Majaliwa Majaliwa wakati akijibu swali la mbunge wa same magharibi David Mathayo(ccm) mnamo tar 11/02/2021 huko bungeni kuhusu namna serikali ilivyojipanga kukabiliana na upungufu wa walimu kutokana na ongezeko la wanafunzi mashuleni alisema "serikali imekua ikiajiri Mara kwa Mara pale fursa inapopatikana ambapo hivi karibuni ilitoa ajira 13,000 ambazo awamu ya kwanza iliajiri walimu 8,000 na wiki kadhaa zilizopita iliajiri walimu 5,000"
Swali je hizo ajira elfu 5 zilitoka na kutangazwa kwa kufuata misingi gani? Je hayo majina elfu 5 yaliwekwa kwenye media gani au mtandao gani hata yasionekane kwa walimu wote walioziomba?
Kwanini mambo muhimu kama haya yanayohusu watanzania yawe kimyakimyaa? Wasomi wapo mitaani huku wanatia huruma hawajui hatima yao ni ipi! Inasikitisha sana kuona kijana wa miaka 25-26-27 ambae unaweza kukuta ndio msomi wa kwanza katika familiya na ana watu nyuma wanamtazama kama tegemeo kubwa na chachu ya maendeleo sio tu kwa familiya hata kwa TAIFA zima kwa ujumla yupo mtaani hana jambo la msingi zaidi ya kupambana na ugumu wa maisha na zaidi ni kuonekana kukata TAMAA ya maisha, kuna wengine wapo wanazingojea zile ajira ajira elfu 5 za hayati Dr JPM zitangazwe LAKINI hazijulikani zilipoishia! tunakwenda wapi Tanzania pasipo ukweli na uwazi?

Jambo lingine tarehe 06/03/2021 Mh. Rais Samia Suluhu Hassan alitoa tamko la ajira 6000 kwa walimu kufidia nafasi za wale walioacha kazi, waliostaafu na waliofariki, nanukuu alivyosema "Natambua kuna Walimu wengi tu karibu Elfu 6 au zaidi ambao wamestaafu, wamefariki n.k na kunahitajika wa kuziba nafasi hawa sio ajira mpya ni wa kuziba nafasi, Utumishi mko hapa na TAMISEMI mkalisimamie, Walimu Elfu 6 warudishwe haraka ili wakawatumikie Watanzania"

Sasa kupitia tamko hilo la rais, wizara ya elimu TAMISEMI imechukua hatua gani za HARAKA kama walivyotakiwa na muheshimiwa rais? Badala yake wanasema wataajiri mwezi wa sita, hii inaendana vipi na kasi aliyoisema rais?

ANGALIZO; Tusipokua makini hata hizo elfu sita zitapotelea JUU kwa JUU pasipo kujilikana zitakapoishia!

MAOMBI NA MAPENDEKEZO;
Sisi kama walimu tuliopo mitaani na hatuna sehemu ya kwenda kusemea shida zetu zikasikilizwa kwa urahisi tunaomba tumrudishie shida zetu muheshimiwa waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu kwa mamlaka aliyopewa na rais ayafanyie kazi haya yafuatayo bila kujali itikadi ya aina yoyote na ukubwa wala udogo wa wadhifa wa mtu katika wizara yake pasipo na upendeleo!!!

1. Walimu tulio mitaani tunajua ajira hizo ni chache na hazitatutosha LAKINI tunaomba UKWELI na UWAZI juu ya namna ya utoaji wa hizo ajira kwa kutumia njia rasmi zinazotambulika na kufikika na kila muombaji.

2. Tunapendekeza Mchakato wa utoaji wa majina ya walimu zile elfu 5 na hizi elfu 6 alizosema Muheshimiwa rais ufanyike haraka sana iwezekanavyo ili kuendana na kasi ya rais ikiwezekana kabla ya mwezi huu wa nne 2021 haujaisha!

3. Wizara ya elimu TAMISEMI iweke wazi juu ya vigezo vya kuajiri ili waombaji tuwe tunafahamu wametumia vigezo gani kama ni umri, GPA, idadi ya masomo na vituo vya kazi vilivyoombwa ijulikane ili tuendelee na mambo mengine na sio kucheleweshana!!!unadhani IPO kumbe HAIPO!

4. Tunaomba mfumo wa uchaguzi wa majina na kupanga vituo vya kazi ujulikane kama ni manual au automatic ili kuondoa UBAGUZI katika kupanga vituo vya kazi unaochukua muda mrefu! NA HII INAWEZA KUWA SABABU KUBWA YA KUZALISHWA AJIRA HEWA (MNATUFUNDISHA UZALENDO UPI SISI VIJANA AMBAO INASEMEKANA NDO TAIFA LA KESHO KAMA SIO KUFANYA KAZI KWA KUJUANA NA KUBAGUANA?)

5. Kama suala la upangaji na utoaji wa ajira limewashinda wizara ya elimu TAMISEMI basi tuwaachie mamlaka hayo UTUMISHI kupitia mfumo wa PSRS.

MWISHO:
Kada ya uwalimu imekua saturated (walimu ni wengi sana nchini) kiasi ambacho taasisi binafsi zinatuchezea kama midoli au vitenesi, ajira zimekua ngumu na ukipata hata iyo sekta binafsi unafanya kazi kwa manyanyaso yaani unafanya kazi kama MBUZI WA SADAKA alafu malipo ni kichele na muda mwingine kuzungushwa mpaka unaacha kazi!Kitendo hiki kinashusha thamani ya kada ya uwalimu na kuonekana si kitu si chochote katika jamii hii ya sasa ya UTANDAWAZI!

TUNAOMBA muheshimiwa UMMY MWALIMU kwa mamlaka uliyopewa na Rais uyafanyie kazi kwa wepesi kadri M/Mungu alivyokujaalia!

Ni SISI WALIMU WA MITAANI TULIOCHOKA KUCHEZEWA!

TUMECHOKAAAAA JAMANIII TUMECHOKAA!😣 tunaandika haya sio kwamba tunaona mbali sana kuliko viongozi wala si kwa maslahi yetu binafsi Ila ni kwa faida ya wote tusio na sauti tuliopo mitaani na kwa kutanguliza MASLAHI MAPANA YA KULITUMIKIA TAIFA LETU , tunaomba yasipuuzwe na badala yake yafanyiwe kazi sawa sawa na kasi ileile inayotakiwa kadri Mutakavyopata kibali mbele ya Mungu akhsanteni sana!
 
Back
Top Bottom