Serikali ndiyo imeshtuka, ukosefu wa dola umesababishwa na Serikali yenyewe kwa kuwabeba wachina miradi mingi

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,330
24,212
Ukosefu wa dola sasa unaathiri biashara nyingi zinazotegemea kuagiza vipuri na malighafi zinazohitajika kuagizwa nje.

Kwa miaka mingi viongozi wa serikali wamekuwa wakishinda kila kiongozi kumpata "Mchina wake" kwenye miradi mingi nchini.

Wachina wamekuwa wakipewa miradi hata inayoweza kufanywa na wazawa hapa nchini.

Hili limelalamiikiwa kwa miaka mingi sana na wananchi mbali mbali, lakini kwa vile viongozi hao walikuwa wakipewa cha juu, wakaziba masikio.

Sasa kilichotokea ni kwamba wachin si wazawa, na wao wakipata hela y madafu wanaiwinda dola ya marekani kama luba.

Matokeo yake wachina wana nunua dola hadi Tshs 2,700 kwa dola moja.

Matokeo yake dola haionekani mitaani, maana ikiingia tu, imekwapuliwa.

Hili ni tatizo serikali imejijengea yenyewe, na yenyewe inajua miradi ya wachina imetolewa vipi.

Shida hii kwa biashara za wananchi imetokana na serikali yenyewe.
 
Ni shida sana, miradi mingi Sana hata Ile midogo wanapewa wageni na transaction zinafanyika Kwa dola.

Serikali ilipaswa kuwajengea uwezo wakandarasi wa ndani na kuwawezesha mitaji ikiwa pamoja na kuwalipa Kwa wakati ili wawe na uwezo wa kujenga miradi mingi, hela na utalaam zibaki hapa.
 
Mwanzo miradi ilikuwa inachukuliwa na wazungu hali ndo ilikuwa mbaya zaid kwa sababu mikataba iliyokuwa ikitumika ni ya kimataifa (Fidic) ilikuwa lazima walipwe kwa $...tukija kwa wachina mirad karibu yote wanalipwa kwa Tsh.. sisi kandarasi za kibongo wengi hatukidhi vigezo vya kupata miradi mikubwa wanayopata wachina hapa bongo...
 
Dola haionekani mitaani,
Screenshot_20230430-113713.png
Screenshot_20231209-232805.png
 
Ni shida sana, miradi mingi Sana hata Ile midogo wanapewa wageni na transaction zinafanyika Kwa dola.

Serikali ilipaswa kuwajengea uwezo wakandarasi wa ndani na kuwawezesha mitaji ikiwa pamoja na kuwalipa Kwa wakati ili wawe na uwezo wa kujenga miradi mingi, hela na utalaam zibaki hapa.
Je, makandarasi wetu nao ni tatizo, kwa mfano, ujenzi chini ya viwango na kutozingatia muda wa kukamilisha mradi.
 
Ukosefu wa dola sasa unaathiri biashara nyingi zinazotegemea kuagiza vipuri na malighafi zinazohitajika kuagizwa nje.

Kwa miaka mingi viongozi wa serikali wamekuwa wakishinda kila kiongozi kumpata "Mchina wake" kwenye miradi mingi nchini.

Wachina wamekuwa wakipewa miradi hata inayoweza kufanywa na wazawa hapa nchini.

Hili limelalamiikiwa kwa miaka mingi sana na wananchi mbali mbali, lakini kwa vile viongozi hao walikuwa wakipewa cha juu, wakaziba masikio.

Sasa kilichotokea ni kwamba wachin si wazawa, na wao wakipata hela y madafu wanaiwinda dola ya marekani kama luba.

Matokeo yake wachina wana nunua dola hadi Tshs 2,700 kwa dola moja.

Matokeo yake dola haionekani mitaani, maana ikiingia tu, imekwapuliwa.

Hili ni tatizo serikali imejijengea yenyewe, na yenyewe inajua miradi ya wachina imetolewa vipi.

Shida hii kwa biashara za wananchi imetokana na serikali yenyewe.
Barabara ya KIBAHA--MOROGORO [Njia sita]. washapata WAchina wawili, kila mmoja kaletwa na mkubwa, kuna vikumbi hata bi'kizi hawezi ingilia ndio maana mkataba wa kuazna ujenzi hausaini.
 
Hao watalipwa kwa hela ya madafu, na kwa hela hizo nyingi watakausha dola mtaani.
Halafu "Dokta wa Uchumi" atashangaa kama sisi mbumbumbu kwa nini dola haipatikani.
 
Ukosefu wa dola sasa unaathiri biashara nyingi zinazotegemea kuagiza vipuri na malighafi zinazohitajika kuagizwa nje.

Kwa miaka mingi viongozi wa serikali wamekuwa wakishinda kila kiongozi kumpata "Mchina wake" kwenye miradi mingi nchini.

Wachina wamekuwa wakipewa miradi hata inayoweza kufanywa na wazawa hapa nchini.

Hili limelalamiikiwa kwa miaka mingi sana na wananchi mbali mbali, lakini kwa vile viongozi hao walikuwa wakipewa cha juu, wakaziba masikio.

Sasa kilichotokea ni kwamba wachin si wazawa, na wao wakipata hela y madafu wanaiwinda dola ya marekani kama luba.

Matokeo yake wachina wana nunua dola hadi Tshs 2,700 kwa dola moja.

Matokeo yake dola haionekani mitaani, maana ikiingia tu, imekwapuliwa.

Hili ni tatizo serikali imejijengea yenyewe, na yenyewe inajua miradi ya wachina imetolewa vipi.

Shida hii kwa biashara za wananchi imetokana na serikali yenyewe.
expand...
Ongeeni na Wamarekani waingie kiwandani watuchapishie makaratasi wayaite "DOLA"- Vladimir Putin.
 
Back
Top Bottom