kindikwili
JF-Expert Member
- Oct 5, 2016
- 1,862
- 2,871
Amani iwe kwenu!
Kwa wale ndugu zangu mliosoma biashara kuna somo linaitwa Strategic Management, kwa kifupi somo hili linaangazia zaidi juu ya kuanzisha, kutekeleza na kupitia au kurejea mikakati yaani kwa kimombo wanasema stategic managment is about formulation, implementation and Review / appraisal of the strategy, lengo hasa ni kupata faida endelevu dhidi ya washindani wako.
Nimetoa utangulizi huo mdogo kufuatia kile kilichotokea kwenye habari ya bundle za simu hasa data. Toka mwaka jana watumiaji walikuwa wanalalamikia gharama za juu za bundle na hasa data. Malalamiko yalikuwa makubwa ya watumiaji kutaka gharama zishuke. Kama unavyojua gharama ingeshuka mapato ya makampuni yangeshuka na serikali ingekosa kodi kwa sehemu (assume mambo mengine yabaki yalivyo/ under ceteris peribus).
Serikali ikahidi wananchi kushughulikia kero hiyo na kwamba watashusha gharama. Walichokifanya ni kuongeza garama juu zaidi ya matarajio ya watumiajia. Watumiaji badala ya kuendelea na madai yao ya awali, ikabidi waanze kulalamika walau bei zirudi kama awali.
Serikali ikaona mkakati wao wa kutoa watumiaji kwenye madai yao ya awali umetiki na kuanza kuwaomba makampuni kurudisha bei kama ilivyokuwa mwanzo. Kwa maana hiyo madai yale ya kutaka bundle zipungue bei imekufa kifo cha mende, watumiaji wamesahau na sasa wanapigana walau warudi walipokuwa wanalalamikia. Hiyo ndiyo stategic managment.
Kindikwili.