Serikali na kampuni za simu zilivyotoa watumiaji kwenye reli

kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,862
2,871
Amani iwe kwenu!

Kwa wale ndugu zangu mliosoma biashara kuna somo linaitwa Strategic Management, kwa kifupi somo hili linaangazia zaidi juu ya kuanzisha, kutekeleza na kupitia au kurejea mikakati yaani kwa kimombo wanasema stategic managment is about formulation, implementation and Review / appraisal of the strategy, lengo hasa ni kupata faida endelevu dhidi ya washindani wako.

Nimetoa utangulizi huo mdogo kufuatia kile kilichotokea kwenye habari ya bundle za simu hasa data. Toka mwaka jana watumiaji walikuwa wanalalamikia gharama za juu za bundle na hasa data. Malalamiko yalikuwa makubwa ya watumiaji kutaka gharama zishuke. Kama unavyojua gharama ingeshuka mapato ya makampuni yangeshuka na serikali ingekosa kodi kwa sehemu (assume mambo mengine yabaki yalivyo/ under ceteris peribus).

Serikali ikahidi wananchi kushughulikia kero hiyo na kwamba watashusha gharama. Walichokifanya ni kuongeza garama juu zaidi ya matarajio ya watumiajia. Watumiaji badala ya kuendelea na madai yao ya awali, ikabidi waanze kulalamika walau bei zirudi kama awali.

Serikali ikaona mkakati wao wa kutoa watumiaji kwenye madai yao ya awali umetiki na kuanza kuwaomba makampuni kurudisha bei kama ilivyokuwa mwanzo. Kwa maana hiyo madai yale ya kutaka bundle zipungue bei imekufa kifo cha mende, watumiaji wamesahau na sasa wanapigana walau warudi walipokuwa wanalalamikia. Hiyo ndiyo stategic managment.

Kindikwili.
 
Makampuni ya kibepari yanajua namna ya kuzitumikisha serikali za nchi corrupt kudhulumu haki ya wananchi wake kupata huduma Bora kwa Bei nafuu
Bahati mbaya makampuni karibia yote duniani ni ya kibepari kwasasa.
 
Blind em' for installing another problem, then come back with previous problem then handle it. U ll' get watchu want!
 
Mkuu imefunga nao ndoa ya kikristo?
Vodacom ni mtandao wa kijeuri sana! Na mdogo wake anaitwa Tigo! Ni shida. Sisi wenye line mbili tu (voda&tigo), tumeshawazoea. Bado miaka michache tu kutimiza miaja 20 tangu nilipo jiunga nao.
 
Vodacom ni mtandao wa kijeuri sana! Na mdogo wake anaitwa Tigo! Ni shida. Sisi wenye line mbili tu (voda&tigo), tumeshawazoea. Bado miaka michache tu kutimiza miaja 20 tangu nilipo jiunga nao.

Mkuu si uhame tu, bora uwe na laini moja special ya data tu!! Ambayo itakuwa nafuu nayo wakikuzingua unawazingua pia unahamia kwingine pia!
 
Kwa upande mwingine, kibiashara, kushusha bei ya bidhaa humfanya mtumiaji kutumia zaidi na matokeo ni faida kwa muuzaji kifedha na kihisia, kwani Mteja huhisi kuthaminiwa.
 
Makampuni ya kibepari yanajua namna ya kuzitumikisha serikali za nchi corrupt kudhulumu haki ya wananchi wake kupata huduma Bora kwa Bei nafuu
Uko sahihi mkuu. Hongo kubwa hutolewa na makampuni ya simu kwa wasimamizi wa huduma hizi(tcra) ili kufumbia macho wizi mkubwa ufanywao kwa wateja.
 
Makampuni ya simu mnayaonea bure kwa muongozo wa TCRA price ceiling ya MB 1 ni Tsh 9 sasa piga hesabu 1 GB inapaswa iuzwe elfu 9 kihalali kabisa.

Voda ilipandisha MB 1 mpka 4.5 Tshs ila ndio kelele zote zile je ingetumia bei halali kabisa ya serikali si ndio mngechoma ofisi zao!!

Mwenye makosa ni TCRA mitandao ya simu inauza chini sana ya bei elekezi hasa Halotel ilikua below 2 Tsh per MB
 
Na hapo ndio tatizo lilipo. TCRA ni regulator, leo kawa mpanga bei!
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom