Serikali na Hatima ya ATCL

Hivi Anne Kilango yupo jamani, yule mwanamama mbunge mzalendo.
 
Hivi Anne Kilango yupo jamani, yule mwanamama mbunge mzalendo.

Yupo hili la ATCL hajaliona wala kulisikia yuko Dodoma kapoa akitoka anaenda Jimboni kwake .

Mzalendo JK kakaa kimya itakuwa Kilango ?
 
Yupo hili la ATCL hajaliona wala kulisikia yuko Dodoma kapoa akitoka anaenda Jimboni kwake .

Mzalendo JK kakaa kimya itakuwa Kilango ?


Wanahusika kwa njia moja ama nyingine nini? Maana ndo style ya TZ. Kigogo akihusika na ufisadi au mtu wake wa karibu akihusika na ufisadi uzalendo unawekwa kando...inabaki kigugumizi.

I am wondering about huu ukimya....nakumbuka issue ya Mengi vs Masha...it took less than 24 hrs to get a response from the govt!

Kunani ATCL, mbona serikali yote kimya? mbona wabunge wote kimya? Hakuna wa kumfunga paka kengele?
 
..jamani its time kuacha kumlaumu kila kitu JK,vipi Waziri wa mawasiliano ambaye hajasema chochote mpaka sasa na hata bunge wana uwezo wa kusikiliza na kuchukua hatua yeyote juu ya ufisadi,JK ataunda tume ngapi wakati aliowapa kazi wapo kimya tuu na hawaambiwi chochote au kuwajibishwa...kuna mawaziri na kamati za bunge zina nguvu sana na matatizo kama haya yapo ndani ya uwezo wao!
 
Na huyu ulimwendesha ? Samahani kama naye pia ni rafiki yako.
 
Na huyu ulimwendesha ? Samahani kama naye pia ni rafiki yako.


- Ohh yeah! it works both ways, yaani kuna wakati washikaji wangu wananiendesha na mimi ninawaendesha, juzi nilikuwa ninamuendesha waziri wa jamhuri wa sheria, kwetu haya huwa ni ya kawaida!.

- Inaonekana watu wengi humu JF huwa mnawabeba washikaji zenu migongoni mwenu, huoni kuwa ni hatari sana hiyo? au?

- By the way Mama Kilango, amekua nje ya nchi toka mwezi uliopita na bado hajarudi, leo yupo DC.

Thanxs!
 

- juzi nilikuwa ninamuendesha waziri wa jamhuri wa sheria, kwetu haya huwa ni ya kawaida!.

Mkuu nadhani ulimuuliza kuhusu mabadiliko ya katiba tunayolilia kila siku hapa JF, pia suala la kumpunguzia raisi madaraka bila shaka wakati uansubiri taa zinazoongoza bara bara ziruhusu, ulimuuliza pia JF ingependa kuona serikali haiingilii uhuru wa mahakama....hatupendi kujua mliongelea nini...wewe kama nguzo muhimu JF utakuwa umefikisha kwa namna moja vilio vyetu...

Thanks
 
Inavyoonekana akina DPP na team yake labda hawako makini na kazi zao au hawana utaalamu na mambo ya anga ndo maana wanasua sua katika kuwafikisha bodi ya ATCL mahakamani. Pia yawezekana kabisa hawana ushahidi ingawaje sijua ni ushahidi wa namna gani wautakao ikiwa kama IATA imekwishwa sema kwamba ATCL ina makosa 500. One mistake katika ndege chanzo cha janga la ajali na kupoteza maisha ya abiria wote, makosa 500 ni kama attempted suicide ya maofisa wa ATCL wanayotaka kuifanyia jamii nzima ya wasafiri bila kujali wanatokea wapi. Bahati yao tu hakuna msafiri alilalamika kwamba ATCL wamesababisha fear na hivyo emotional suffering au negligence pia causation itakuwa vigumu kui-prove. Kama hii hakuna, ushahidi miwngine ni circumstancial ambapo unafaa kuifikisha Atcl BODY kwa mzee pilato.
 
..cha ajabu na uzembe wote huo na ufisadi wa hili shirika hakuna hata mbunge mmoja kwa kutumia kamati zao aombe uchunguzi na kuwachukulia hatua wahusika,hii kitu wanachezea maisha ya watu na pesa za walipa kodi!

Hawawezi kuunda kamati kama JF haitatupa makombora kama yale yaliyotupwa kwa EL, NK na fisadiz wengine. Nyie subirieni, haya yakifika tu mtaanza kuwasikia wabunge wakianza kudai uchunguzi. Tuko hapa mtaniambia....
 

- Nilimuuliza maswali mengi sana kama ulivyosema na hasa kuhusu mafisadi na kubadili katiba, na ni kweli nilifikisha vilio vyetu hapa na nilipewa majibu mengi ya maswali yetu hapa.

Thanxs!
 

Kwani huyo JK anachosubiri kumfuta kazi huyo Waziri na hiyo bodi yake ni nini. Ni lazima kuwepo na tume?
 
NOTE: Any off topic response will be muted ASAP. Sorry for those interested to read em comments
 
Bysel

We kweli ni mwendawazi mu kama Mattaka.Unamtetea kwa sababu ya gani. Wewe Mataka kakutuma ili uje kumsafisha humu ndani ya FORUM. ATCL walipewa hizo 13 Bil na serikali na wamezila zoooooote.
JK ameleta USHIKAJI ktk kuendesha nchi matokeo yake ni hayooooooo. We mtu alishafukuzwa kazi na RAISI kwa Manufaa ya UMMA. leo hii unamrudisha na kumpa shirika kama lile. Anachuma Chake Mapema kwani Nafasi kama hizo Haziji Mara mbili.
Inamaa hakuna watanzania wengine wenye uwezo wa kila kitu mpaka amrudishe Mattaka

Nchi haiendeshwi kwa Ushikaji
 
Siwezi nikashangaa hilo. Takriban mwaka na nusu umepita toka nilipotoa ushauri usiolipwa kwa shirika hilo na kuwaambia waangalie upya visheni na misheni yao!

Walinitumia ujumbe feki na tiketi feki ya kuhudhuria mkutano fulani nikaenda kwa ajenti wa usafiri wa ndege na kukuta hakuna kitu kama hicho. Nikawashukuru na ninawashukuru mpaka leo.

Lakini haya ndio matunda ya kukataa ushauri. Na popote pale utakapokuta matatizo ya menejimenti partly hili linasababishwa na kiongozi kichwa ngumu ambaye ama ana pokea na kukubali ushauri mbovu au hakubali ushauri wowote.

Kudonoa nilichowagawia kina Bw. Makatta wakati huo ni kwamba biahsara ya mizigo itawabeba zaidi ATCL kuliko ya abiria kwani walichelewa kulishughulikia hili. Na ninaamini hadi wa leo kuwa shirika hilo likiwa na ndege za mizigo mikubwa bado lina nafasi hasa wakati huu wa bei ya mafuta ya ndege kushuka pia.

Ili kushughulikia abiria nilitamani wanipe nauli nikazungumze na Richard Branson (Virgin Airlines) kwa siku moja tu na ningekuja na dawa ambayo ingeliwafaa. Lakini kwa jinsi tunavyopenda safari sasa naruhusu yoyote tu aende acha mimi nile ugali na mchicha bongo na kutoa ushauri usiothaminiwa wala kulipiwa! Ule unaothaminiwa na kulipiwa kama mnavyojua ndio umeliingiza shirika hapo lilipo. Je, washauri hao wana tofauti na mafisadi wa EPA!
 
SIO haki kuwalaumu kina Makatta tu hapa. Uteuzi wetu wa Bodi za Wakurugenzi Tanzania ni mbovu, mbovu, mbovu kiasi cha kutisha!

ATCL ingelikuwa na Bodi inayofanya kazi kweli kama bodi lakini sio wakala wa kulipwa bila kufanya kazi wa kisiasa haya yasingeikuta jamani.

Wa kulaumu ni serikali na washauri wake wa menejimenti na usimamizi bora wa mashirika. Wakenya na wageni wengine wanakuja nchini kwetu na kuteua bodi za wakurugenzi zenye Watanzania, safi, wachapa kazi na wabunifu lakini sisi wenyewe tunayawekea mashirika yetu 'cluster bombs' halafu yakilipuka na kujerushi kelele kama balaa! Tuamkeni!

Shrika, Kampuni, chama au taasisi yoyote ya binadamu aidha inafanya vizuri au kufanya vibaya kutegemeana na kichwa! Yaani mkuu au wakuu wa mahala hapo. Wakiwa bomu habari ndiyo hiyo---tasisisi inaanguka. Wakiwa safi ---taasisi inapaa. Kwa hiyo tuchague kati ya upenzi na ushabiki wa ksiasa tufe njaa na masikini, au tuchague watu wenye upeo na uwezo wa kuleta mabadiliko tuuupe umasikini 'byebye'!
 
Wajinga ndio waliwao

Tunapoteza TZS Ngapi kwa watalii ambao walikuwa wameshapanga safari zao kuja huku kwetu kupanda Kilimanjaro, Kutembelea mbuga za wanyama, fukwe za Bahari, miji mikogwe kama Z'bar, bagamoyo, Sadan

Serikali yetu imekaaaaaaa kimya haijamchukulia mtu yeyeto hatua za kinidhamu. Kweli ndio tunapima Accountability namna hiii

JK anafanya nini, anakaaa tu au hasomi magazeti au wasauri wake hawampi habari za huku nje ya Ikulu. Mi sipati picha. TV huwa anaaangalia kweli au huwa wanamchagulia Tv station za kuangalia?. Hasomi Internet habari mbali mbali kuhusu nchi yake.

Nisaidie jamani, huyu raisi wety ana washauri kweli madhubuti wanaoangali nchi inateketea na wao wanamficha Uozo Raisi
 
Kamati zitaundwa ngapi.???????????

Yaaani unataka kuwapa watu ulaji tena. Kamati ngapi zimeundwa na hatujaona na report kali zenye kuwachukulia Hatua kali wale waohujumu Uchumi?.

Tumechoka na haya mambo serikali ya JK inayoyafanya. Kweli tumechoka na Kiama Yao ipo njiani yaja. Hakuna Jiwe litaachwa Kuguswa
 
ATC yapigwa nyundo nyingine
*SASA YAZUIWA KUFANYA BIASHARA


Leon Bahati
 
Is Accountability finaly coming to Tanzania? Lets wait and see.


Tanzania Standard Newspapers|Home
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…