Tunawadhulumu watoto kwa makosa tuliyoyaandaa wenyeweNaongea wazi kabisa hapa. Kwa miaka mingi Serikali imekuwa ikihukumu maisha ya wahitimu wa darasa la saba kimakosa mno.
Ipo hivi...
Watendaji na wasimamizi wa elimu ya msingi wao ndio viongozi wa kuratibu cheating. Hili liko wazi kabisa na NECTA wanalijua.
Walimu wakuu wa shule za msingi hupigwa mikwara na ma RC, RAS, REO, DED, DEO, DAS, WARATIBU WA ELIMU etc. Wafanye vyovyote iwezekanavyo KUWAFAULISHA watoto. Nasisitiza KUWAFAULISHA. Na mbinu zote za kuwafaulisha huratibiwa na Walimu Wakuu na Waratibu wa Elimu katani. Wanafunzi hupokea tu maelekezo. Hawana hatia.
That being said, nawaambia NECTA na namwabia Rais Magufuli. Achieni matokeo ya vijana hao haraka. Hawahusiki.
Wajibisheni mamlaka husika, nimezitaja hapo juu. Vigezo vyote vilivyoandikwa/semwa na NECTA kuwafutia matokeo vijana hao hakuna hata kimoja kilichosababishwa na mwanafunzi. Kumbukeni hawa ni watoto wadogo sana na hufuata orders toka kwa walimu wao.
Ni muda muafaka sasa umefika, kuacha tabia ya kumfurahisha mkuu wenu. Yote haya yanafanyika kumfurahisha MAGUFULI. HII SI SAWA.
Shule zotee za uma hufake/hucheat ili tu kumpemdezesha mkuu wenu.
OMBI.
Rais Magufuli iamuru NECTA itoe matokeo ya vijana hawa 1059. Then deal with your SYSTEM.