Uchambuzi wa ukweli kuhusu Adhabu kwa watoto: Je kunafaida? Madhala yake ni nini? science jamii inasemaje?

Hisha Sorel

Senior Member
Dec 27, 2017
192
140
Note: a) Soma full article kuelewa mada (b) Chanzo zote za ushaidi zimeandikwa chini ya article d) Maneno ya kiingeleza yametumika kusaidia ugumu wa lugha.

Asante

Introduction
Watanzania wengi hulinganisha “adhabu za maumivu” na maadili. Hizi zikiwa, kitendo chochote kinachomletea mtoto maumivu; kwanzia viboko, kufinya, push up, kupigamagoti, na kadhalika. Imekuwa si ajabu kwa wazazi kuangalia shule na walimu wanaotenda haya kama sign ya mafanikio ya academia. Kwa nyumbani, adhabu hizi zimeangaliwa kama nguzo ya maadili, bila kukosa support kutoka kwa jamii.

Kiufupi
Dai la maadili mema kama zao la “adhabu za maumivu”, limeendekezwa kwa mda mrefu, na wengi kuhisi ni la ukweli. Lakini ushaidi wa kisayansi, haukubaliani. Tena ushaidi huu, unaonesha “adhabu za maumivu” kama chanzo cha kumharibu mtoto, kimwili, kisaikolojia, na kimahusiano. Zaidi ya hapo, ushaidi unaonesha adhabu hizi kama chanzo cha kushuka maadili ndani ya jamii. Kiundani zaidi, hili karatasi litalinganisha mtazamo unaoshikiliwa na wengi kuhusu “adhabu za maumivu” na kulinganisha na ushaidi wa kisayansi.

Kiurefu
Kwenye suala la maadili, msimamo ni; “adhabu za maumivu” ni chanzo cha maadili mema. Kuchambua hili jambo kunahitaji kwanza kuangalia tafsili ya maadili. Hapa, kamusi ya Kiswahili inasema; “Maadili ni mafundisho yanayotolewa katika nafasi mbalimbali, hasa katika malezi, ili kuelekeza binadamu atende namna ambayo inamjenga yeye na jamii nzima” (Oxford, 2018). Kipimo kizuri cha maadili kitazingantia, faida ya mafunzo kwenye jamii, na mtu-binafsi. Ikimaanisha, kama dai ni sahihi, “adhabu za maumivu” zitakuwa na faida kubwa kwa mtoto na kwa jamii kwa ujumla.

Tanzania ni moja ya nchi 48 zisizolinda mtoto dhidi ya “adhabu za maumivu” (EACPC, 2015). Kupitia dai, maadili ya nchi hizi yatategemewa kuwa juu; lakini ushaidi unaonesha hii si kweli, hasa hasa ukilinganisha na nchi zisizoruhusu “adhabu za maumivu”. Takwimu za prevalence of sexual violence: yani idadi ya kesi za ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia, ndani ya jamii moja kwa wakati maalumu, nchi hizi 48, ukiunganisha na Tanzania zinaongoza duniani kwa idadi za kesi (NIMH, 2017). Kwa Tanzania, asilimia 42 ya wanawake wanarepotiwa kubwakwa au kunyanyaswa kijinsia, Zimbabwe asilimia 35, Nigeria asilimia 16 (United Nations, 2015). Hii ni kinyume na matarajio, kwani ingetegemewa namba hizi kuwa chini, hasa hasa ukilinganisha na takwimu za nchi zisizotoa adhabu za maumivu.

Takwimu za ujumla za usalama, zinapanga nchi za; Iceland, New Zealand, Portugal, Austria, na Denmark; juu (UNODOC, 2010). Ikimaanisha uhalifu kwa ujumla upo chini katika nchi hizi. Zaidi ya hapo, ukilinganisha takwimu za ubakaji na unyanyasaji wa kinjinsia zinazoweka Tanzania juu; ulaya kwa ujumla, asilimia 9.2 tu! ya wanawake ndio wataripotiwa kubakwa au kudhalilishwa kijinsia (UNODOC, 2010). Na kati ya nchi salama, New Zealand, ni asilimia 2.1 tu! ya wanawake walioripoti kubwakwa au kudhalilishwa kijinsia (New zealand Police, 2018).

Sambamba na hili, kwenye ubakaji na udhaliishaji wa watoto, takwimu pia zaonyesha nchi zinazo adhibu kwa maumivu, kuongoza. Asilimia 34.4 ya watoto; wa kike million 24 na million 8.6 wa kiume ubakwa ndani ya Africa (WHO, 2010). Theluthi tatu ya watoto kubakwa Swaziland, wakati Tanzania ni asilimia 27.9 ya watoto wa kike, na asilimia 13.4 ya wakiume (Mantula & Saloojee, 2016). Takwimu hizi zinakiuka mategemeo, kwani; shangaa watoto wanalelewa kwa kuadhibiwa kwa maumivu, uhalifu ukwubwani umekuwa wa hali ya juu. Hili linaweza kuwa likisababishwa na madhala ya adhabu, kinyume na mategemeo.

Kisayansi, masomo yaliofanyika marekani yameonesha kwamba watoto waliopigwa wakiwa umri mdogo, huishia, zaidi ya wenzio, kuwa wakorofi (wakatili) (Durrant & Smith, 2010). Watoto hawa utambua uwezo wao mdogo wa kujilinda, kama sababu ya kupigwa. Mwishowe, ni vyepesi kuchukulia uonevu kama jambo la kawaida, na kuruhusu au kuishia kutumia mabavu mbeleni (Durrant & Smith, 2010). Si ajabu kuangalia wale walio chini yao kinguvu, kama nafasi ya kutekeleza matakwa yao. Ndo maana si ajabu, kwa vijana wa Africa kuangalia wanawake na watoto kama mali, badala ya binadamu wenza.

Mazoea ya unyanyasaji kama njia mbadala ya kutatua matatizo, huwa ni chanzo cha vurugu mbeleni. Tofauti na nchi zinazokemea “adhabu za maumivu”, mabavu kama suruhisho ni jambo la kawaida nchi za Africa zinazotoa ruksa. Hili linaonekana wazi pale takwimu za mauaji ya maksudi zikiangaliwa. Kwani, kiwango cha mauaji kwa nchi za kusini mwa Africa zinakadiliwa kuwa watu 60 kwenye kundi la watu lakimoja (60/100,000) (UNODOC, 2010). Tanzania, Kenya, Zimbabwe, na Sudan zikiwa zinaongoza kwa zaidi ya watu 20 kuuwawa ndani ya lakimoja (>20/100,000). Hii ni juu, ukilinganisha na chini ya kumi ndani ya watu laki moja (<10/100,000) kwa nchi nje ya Africa, wakati ulaya ikiwa chini ya watu watano ndani ya watu laki moja (5/100000) (UNODOC, 2010). Ni wazi kwamba, moja ya mafunzo ya “adhabu za maumivu” ni matumizi ya nguvu kama mbinu ya kutatua matatizo, na siyo vyombo lasmi.

Zaidi ya hapo, matokeo ya kielimu hutajwa kama sababu moja ya kuadhibu. Ikiwa, bila kumbusho la maumivu, watoto watasahahu umuhimu wa kujifunza. Hili lingekuwa sahihi, shule na nchi zinazo sukuma watoto kwa maumivu, zingeongoza ki-acedemia, kuziacha nchi zinazokwepa adhabu hizo.

Lakini, bila pingamizi, hili si kweli. Takwimu za malinganishi kati ya nchi za Africa na jirani ni ngumu kupata. Ila ukilinganisha nchi nje ya Africa, zilizo na msimamo rahisi juu ya adhabu za maumivu, na kulinganisha na nchi zilizo na msimamo mkali; mwenendo upo wazo. Mtihani wa ya PISA, unapima uwezo wa mwanafunzi kutumia Science, Mathematics, na kusoma, ili kutatua matatizo ndani ya jamii na siyo kukalili mafunzo; zinaonyesha mafanikio ya juu kwenye nchi kama Canada, finland, Sweden, na Canada; na mafinikio ya chini kwa nchi na magharibi ya Africa, uharabuni, kusini mwa Marekani, na kusini mashariki mwa Asia (OECD, 2015). Mwenendo wa takwimu waonyesha mahusiano kati ya mafunzo mbadala bila “adhabu maumivu”, na mafaninikio. Asilimia kubwa za nchi za juu, adhabu hizi ni kinyume na sheria. Hata kwa takwinmu nchini, performance ya juu kwenye matokeo ya NECTA, huenda kwa shule binafsi, zinazojulika kwa adhabu za hali ya chini (NECTA, 2016).

Ni vyepesi kufikiri uwoga, nia ya adhabu, humsukuma mwanafunzi kujikita kwenye masomo. Huu ni mtazamo wa kina kifupi; vizuizi vya mafanikio kwenye elimu ni zaidi ya mwanafunzi. Si ajabu kwa wanafunzi kukosa vifaa vya masomo, vyakula vyenye virutubisho mashuleni, walimu waliobobea kwenye stadi, support ya kutosha kutatua matatizo, mda wa kutosha wa kujisomea, na kadhalika. Zaidi ya hapo, matatizo ya akili au kimwili yanayoweza kuzia mafanikio kwenye elimu huwa hayatambuliki. Kwa ufupi, Vikwazo vya elimu bora ni vingi, na kuvitatua ni jambo linalohitaji umakini, na ushahidi, na siyo hisia za haraka. Cha kushangaza ni kwamba, mtazamo huu si ngeni, kwani si ajabu kwa team za mpira kubadilisha bench zima la ufundi ili kuleta mafanikio. Ingekua ajabu kama viboko vimetumika kusukuma wachezaji, zaidi ya hapo, ni kinyume na sheria. Hence, ni ajabu kujikita kwenye kupiga wanafunzi kila wakishindwa kufanikiwa badala ya kuuliza maswali ya kiundani zaidi.

Mpaka sasa, inaonekana kama “adhabu za maumivu” hazina faida kama wengi wanavyodhani. Lakini, shangaa huwa alitamkwi wazi, adhabu utolewa kwa mida mingine, kulidhisha mlezi au mwathirika. Maumivu yanaangaliwa kama “haki”, yani “jicho kwa jicho”. Jambo hili ufanywa kwa nia njema, na mda mwingine, kama onyo ili tendo lisirudiwe na mtoto au mwingine au yeyote. Lakini bila kujua, ushaidi unaonesha adhabu hizi ufanya madhala makubwa kwa watoto kimwili, kisaikolojia, na kimahusiano.

Ushaidi ndani ya science za kijamii unaoenesha “adhabu za maumivu” zinasababisha matokeo hasi kwa mototo kwenye vipengele vya kijamii, hisia, kifikra, au kukua kimwili. Ushaidi ni wa hali ya juu, jambo ambalo si la kawaida kwa science za kijamii (Durrant & Ensom, 2012).

Majaribio yaliofanyika marekani yemeonesha mahusiano kati ya “adhabu za maumivu” na chuki kati ya watoto, wazazi, ndugu, jamii, na wapenzi (Durrant & Ensom, 2012). Zaidi ya hapo, majibu yalionesha kuwa watoto walioadhibiwa walikua wepesi kutokuwa waamninifu, kunyanyansa wenza kwenye mahusiano (Durrant & Ensom, 2012). Majaribio haya yalihusisha watu kutoka matabaka yote ya kiuchumi na jinsia zote, lakini mwishowe, majibu yalifanana. Majaribio ya kuchapa yanaonesha watoto waliochapwa huwa na nidhamu ya mda, bila kuwepo na tofauti ya mda mrefu kati yao na wasiochapwa (Durrant & Ensom, 2012). Kinyume na hapo, Somo la mwaka 1997 lilionesha, ukizingatia uchumi, rangi ya ngozi, jinsia, na familia; watoto waliochapwa walionesha tabia nje ya maadili zaidi ukubwani, kupita wasiochapwa (Durrant & Ensom, 2012). Sambamba hilo, masomo 27 yaliochapishwa 2002, yameonesha familia zilizofunzwa njia tofauti na “adhabu za maumivu”, zilifanikiwa kupunguza tabia ngumu za watoto (Durrant & Ensom, 2012). Pamoja, masomo yameonesha “adhabu za maumivu” kama chanzo cha watoto kutenda kwa wazi vitendo nje ya maadili kama mbinu ya kujibishana na familia zao, au ku deal maumivu. Sio ajabu kwa vijana kufanya makosa maksudi ili kupingana na walezi wao.

Ki afya, somo la Canada la mwaka 2000, lilionesha mahusiano kati ya watoto waliopigwa makofi na matatizo ya akili kama; depression, anxiety, ulevi, kukata tamaa, matumizi ya dawa za kulevia na matatizo mengine na kisaiokolojia (Durrant & Ensom, 2012). Haya yamesababishwa na kuharibika kwa mahusiano ya mzazi na mtoto kisa maumivu yaliosababiswa na mzazi, na kusababisha kuongezeka kwa cortisol au kemikali nyingine kuingilia ubongo unaosimamia stress (Durrant & Ensom, 2012). Wasomi pia wamegundua kwamba maumivu yanadumisha ukuaji wa ubongo, mwishowe kushusha mafanikio ya shule. Haya yamethibitishwa na masomo (neuroimaging) yanayopima ujazo wa “grey matter” kwenye ubongo, na kuonyesha kushuka kwa ujazo pale mtoto anapopigwa. Grey matter inahusishwa na ufaulu wa mtihani wa akili wa Weschsler (Weschsler Adult Intelligence Scale III) (Durrant & Ensom, 2012). Zaidi ya hapo, “adhabu za maumivu” usababisha mabadiliko kwenye “dopaminergic regions” kwenye ubongo, zinazohusishwa na matumizi na pombe na madawa ya kulevya (Durrant & Ensom, 2012).

Ujumla
Kwa ujumla, si kweli kwamba “adhabu za maumivu” zinajenga maadili kwenye jamii; kwani ushaidi unaonesha wazi kuwa nchi zinazo adhibu hounesha maadili ya chini kulinganisha na zile sizisoadhibu. Pili, si kweli kuhusu adhabu na mafanikio ya kielimu, kwani mahusiano ya elimu bora na nchi zinazopinga “adhabu za maumivu” yapo wazi. Tatu, si ukweli kwamba kuchapa hakuna madhala, kwani ushaidi wa kisayansi unaonesha madhala kisaiokolojia, kimwili, na kifikra. Lakini ni wazi kuwa wazazi wengi hawana njia tofauti ya kufundisha wanayoifahamu tofauti na kuchapa. Hii imesababisha kwa jamii kukubali adhabu za maumivu kama njia inayokubalika kujenga maadili. Na sababu hii iliyosababisha kutokuwepo kwa tafakari ya njia tofauti ya ku-deal na watoto. Hii ni changamoto inayohitaji jibu la haraka na linalofuata ushaidi. Lakini kwa sasa, adahabu yeyote ile amabayo mtoto atakayopewa, inashauriwa; heshima ya mtoto ilindwe, na haki yake ilindwe. Adhabu isitolewe kabla ya ushaidi kusiskilizwa na kuzingatiwa; pia isitolewe kabla ya onyo; isitolewe bila kosa kutajwa na kuelezewa; isitolewe bila fundisho kuwekwa wazi; na pale ikitolewa, iwe ya haki na isiwe ya ajabu au ya maumivu. Hivi ndivyo tunavyotaka jamii yetu inendeshwe, na kama watoto ni moja ya wanajamii basi inabidi haki hizi pia ziwafikie.


References (Vyanzo)
Arain, M. et al., 2013. Maturation of the adolescent brain. Neuropsychiatric Disease and Treatment, 9, pp.449–61.

Durrant, J. & Ensom, R., 2012. Physical punishment of children: lessons from 20 years of research. Canadian Medical Association Journal, 12(182), pp.1373–77.

Durrant, J.E. & Smith, A.B., 2010. Global Pathways to Abolishing Physical Punishment: Realizing Children’s Rights. 1st ed. Routledge.

EACPC, 2015. Prohibiting all corporal punishment of children in Africa: progress and delay. [Online] (1) Available at: http://endcorporalpunishment.org/as...egional/Progress-and-delay-Africa-2015-EN.pdf [Accessed 11 Feb 2018].

Mantula, F. & Saloojee, H., 2016. Child Sexual Abuse in Zimbabwe. Journal of Child Sexual Abuse, 25(11), pp.866-80.

Ministry of Justice, 2013. Sexual violence: RESEARCH & DATA. [Online] (1.5) Available at: https://www.justice.govt.nz/justice...y-results/results-by-subject/sexual-violence/ [Accessed 11 Jan 2016].

NECTA, 2016. CSEE 2016 EXAMINATION RESULTS ENQUIRIES. [Online] Available at: http://www.necta.go.tz/results/2016/csee/index.htm [Accessed 1 Feb 2018].

New zealand Police, 2018. Data and statistics. [Online] (1) Available at: http://www.police.govt.nz/sites/default/files/publications/crime-at-a-glance-dec2017.pdf [Accessed 9 Feb 2018].

Newzealand Police, 2018. Crime at a glance. [Online] (1.5) Available at: Crime at a glance [Accessed 12 Jan 2018].

NIMH, 2017. What is Prevalence? Bethesda: National Institute of Mental Health National Institute of Mental Health.

OECD, 2015. PISA 2015 Results. [Online] (1) Available at: https://www.oecd.org/pisa/ [Accessed 13 Feb 2018].

Oxford, 2018. Maadili. [Online] (1.1) Available at: maadili | Ufafanuzi katika Kiswahili - Oxford Living Dictionaries [Accessed 11 Feb 2018].

UN, 1981. CHAPTER 16 OF THE LAWS (REVISED). [Online] Available at: http://www.un.org/depts/los/LEGISLATIONANDTREATIES/PDFFILES/TZA_penal_code.pdf [Accessed 21 Feb 2018].

United Nations, 2015. Global Database on Violence against Women. [Online] (1) Available at: http://evaw-global-database.unwomen.org/en/countries/africa [Accessed 9 Feb 2018].

UNODOC, 2010. INTERNATIONAL STATISTICS on CRIME AND JUSTICE. Vienna: United Nations Office on Drugs and Crime United Nations.

WHO, 2010. Violence and health in the WHO African region. [Online] (1) Available at: http://www.afro.who.int/en/clusters-a-programmes/dpc/mental-health-vio [Accessed 12 Feb 2018].
 
Da hii mpaka umeshakula umepumzika unakunywa kakinywaji ndo usome juu Uzi


Teh
 
Ndefu sana mkuu acha tu tuendelee kuwapa adhabu kulingana na umri wa mtoto
 
ewe roho mtakatifu nipe ndoto ya hii mada labla nitaipata yote..

mtoa mada sema Amen
 
Back
Top Bottom