Mwelekeo wa sera za Tanzania kwa kuzingatia maudhui ya Ilani ya CCM ya 2020-2025: Je serikali itaweza kutimiza ahadi hizi zote kwa wakati?

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,019
2,473
1609090412126.png

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Dk. John Pombe Joseph Magufuli

I. UTANGULIZI

  1. Uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa mwaka 2020 umekwisha, ukiwa unasindikizwa na ukosoaji mkali kutoka kwa vyama vikuu vya upinzani vya Chadema, ACT Wazalendo na CUF. CCM imepata wabunge 261 kati ya wabunge 264 wa majimbo, sawa na 98.86% Mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli, ametangazwa na NEC kama mshindi halali, na tayari ameunda serikali itakayotafsiri na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.
  2. Sera zote zilizo katika ilani za vyama vyote vya siasa, zinaweza kugawanywa, bila kubaki, katika makundi matano. Makundi hayo ni: Afya, Elimu, Ikolojia, Ofisi za uongozi, na Uchumi. Nakumbuka maeneo haya matano kwa msaada wa vokali tano za Kiswahili, yaani “A, E, I, O, U.”
  3. Kwa kuzingatia haya, katika aya zifuatazo nafupisha ahadi zote 90 nilizoziona kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 ili kuweka rejea murua itakayotusaidia kufanya ufuatiliaji na tathmini ya kazi za serikali kuanzia 01 Januari 2021.
II. AFYA: Afya ni hali ya binadamu kuwa na mwili na akili vyenye kutenda kazi zake barabara. Hali hii ni matokeo ya kuwa na kinga dhidi maradhi yanayoambukiza na yasiyoambukiza, mkamilishano thabiti kati ya nafsi na mwili, na masikilizano kati ya mwili na mazingira yake, ambapo mazingira yanahusisha makazi, malazi, chakula na jamii ya watu wanaomzunguka mhusika. Katika Ilani ya CCM (2020-2025), ahadi kuhusu afya ziko katika ibara za 81-100. Baada ya kuipitia Ilani hii, nimejiridhisha kwamba, kuna sera 16 ambazo zinapaswa kutekelezwa na serikali yake ili kukuza na kuhami afya ya kila raia.
  1. Kuna ahadi kuhusu ujenzi na ukarabati wa vituo vya huduma za afya, ushirikishwaji wa sekta binafsi katika huduma za afya, upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, upatikanaji wa watumishi na mabingwa wa kada ya afya, na sera ya mapambano dhidi ya magonjwa ya mlipuko.
  2. Pia, kuna ahadi kuhusu mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza, mapambano dhidi ya magonjwa yanayotokana na virusi kama vile VVU, upatikanaji wa mlo kamili na bora, na sera ya uduma za ustawi wa wazee.
  3. Aidha, kuna ahadi kuhusu huduma za ustawi wa watoto na familia, huduma za watu wenye ulemavu, kusimamia upatikanaji wa maji na usafi wa mazingira, kusimamia mipango miji na mipango vijiji, sera ya ujenzi wa nyumba na makazi bora, sera ya bima ya afya kwa wote, na sera ya afya ya mama na mtoto. Lakini, katika ilani hii, haikutajwa ahadi ya “bima ya afya kwa watu wote.” Hii ni ahadi ya jukwaani.
III. ELIMU: Elimu ni mchakato wa kupata taarifa, maarifa na ufundi wa kufanya utafiti na kubuni tekinolojia za kumsaidia mwanafunzi aliyefuzu kuyamudu mazingira yake ya kimaumbile, kiuchumi, kisiasa, kijamii, kiutamaduni. Katika Ilani ya CCM (2020-2025), ahadi kuhusu elimu ziko katika ibara za 78-80, na ahadi kuhusu sayansi na tekinolojia ziko katika ibara za 101-103. Baada ya kupitia ilani hii, nimeona kuwa sekta hii itaboreshwa kwa kupitia utekelezaji wa mikakati ya kisera 10.
  1. Kuna ahadi kuhusu elimu ya msingi, elimu ya sekondari , elimu ya ufundi stadi, na sera ya elimu ya Juu.
  2. Pia kuna sera za kuanzisha makampuni ya katika sekta mbalimbali ili kuendeleza sayansi, teknolojia na ubunifu; kujenga mfumo wa Taifa wa ubunifu (national innovation system); na sera ya kuendeleza vituo atamizi kwa ajili ya kukuza na kuendeleza ubunifu wa kisayansi na kitejinolojia.
  3. Kadhalika, kuna ahadi kuhusu kuhamasisha matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu katika uzalishaji, usambazaji, na utawala kwa kutumia tekinolojia ya kidijitali; kuanzisha vituo vya umahiri wa sayansi na teknolojia (centres of excellence) katika taasisi za elimu ya juu; na sera ya kuimarisha mafunzo ya walimu wa sayansi, teknolojia na ufundi katika ngazi za shule za msingi, shule za sekondari, vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi na vyuo vikuu.
IV. IKOLOJIA: Neno "ikolojia" linamaanisha mazingira. Mazingira ya binadamu yanajumuisha wanyama, mimea, wadudu, hewa, maji na vitu vyote vilivyo baki vilivyoko ardhini, angani, majini, msituni, porini, pamoja na michakato yote ya kibayolojia inayomfungamanisha kila binadamu pamoja na vitu hivi kupitia mitandao ya vyakula vya viumbe anwai (ecological food web). Katika Ilani ya CCM (2020-2025), ahadi kuhusu ikolojia ziko katika ibara ya 9B(vii). Baada ya kupitia Ilani hii, na kukagua mikakati ya kutunza mazingira iliyoko katika tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais, nimebaini kuwa, kuna mikakati 10 ya kisera inayoweza kutekelezwa ili kukuza na kuhami mfumo wa ikolojia ulio salama kwa uhai wa binadamu na viumbe baki.
  1. Kuna ahadi juu ya kuhimiza watu kuepuka kadiri inavyowezekana kutumia nishati zinazozalisha hewa ya ukaa ambayo ni chanzo kikuu cha mabadiliko ya tabia nchi; kuwekeza katika miradi ya kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi (climate adaptation strategies); na kuwekeza katika miradi ya kupunguza ukubwa wa vyanzo vya mabadiliko ya tabia nchi (climate mitigation strategies).
  2. Aidha kuna ahadi juu ya kuhifadhi uoto wa asili ulioko juu ya nchi, kuhifadhi uoto wa asili ulioko majini, kuhifadhi wanyama wa porini, kuhifadhi wanyama wa majini, kuzuia mmomonyoko wa ardhi, na kunzisha mfuko maalum kwa ajili ya utafiti, usimamizi na tathmini juu ya hali ya hewa na mabadiliko ya tabianchi.
  3. Kadhalika kuna ahadi juu ya kuzuia uchafuzi wa mazingira unaofanyika kupitia uzalishaji wa takangumu; uzuia uchafuzi wa mazingira unaofanyika kupitia uzalishaji wa takamaji; na uzuia uchafuzi wa mazingira unaofanyika kupitia uzalishaji wa takahewa.
V. OFISI ZA UTAWALA: Utawala bora ni aina ya utawala ambao unahakikisha kuwa utaratibu wa kufanya maamuzi na kutekeleza maamuzi hayo kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa jamii unazingatia misingi ya utu, uhuru, haki, ushirikishwaji, demokrasia, uwajibikaji, uhasibikaji, uwazi, tija, ufanisi, usawa mbele ya sheria, na ushiriki wa makundi yote ya jamii. Katika Ilani ya CCM (2020-2025), ahadi kuhusu ofisi za utawala bora ziko katika ibara ya 108-130. Baada ya kupitia ilani hii nimjiridhisha kuwa kuna jumla ya sera 16 zinazopaswa kutekelezwa kwa ajili ya kufanikisha dhana ya utawala bora.
  1. Kuna ahadi juu ya kuheshimu haki ya kujitawala katika ngazi za chini za serikali kwa kugatua madaraka, kusimamia maadili katika utumishi wa umma, kufanya mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi, kuheshimu misingio ya demokrasia na haki za binadamu, kuheshimu katiba na kuzingatia utawala wa matakwa ya sheria, na sera ya kuhuisha usawa wa jinsia katika sekta ya umma na sekta binafsi.
  2. Pia, kuna ahadi juu ya kuhami uhuru wa vyombo vya habari, kuheshimu uhuru wa raia kujieleza na kuwasiliana, kuhesimu uhuru wa asasi za kiraia, kulinda uhuru wa kuabudu, kulinda haki za wafanyakazi na uhuru wa vyama vya wafanyakazi, na sera ya kukabiliana na majanga ya asili kwa kuzingatia kanuni ya utawala auni (principle of subsidiarity).
  3. Kadhalika, kuna ahadi juu ya kupambana na dawa za kulevya, menejimenti ya mahusiano ya kisiasa na kiuchumi katika ngazi ya kimataifa, menejimenti ya kidemokrasia ya vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi, na sera ya kuzuia utekaji, utesaji na uteketezaji wa uhai wa raia wasio na hatia.
VI. UCHUMI: Uchumi ni mfumo unaojumuisha mambo makuu manne, yaani, michakato, kanuni za kuratibu michakato hiyo, tunu zinazowaunganisha watendaji kwa skuwaelekeza katika malengo yanayofanana, na misingi ya ustaarabu wa kugawana shida na raha za kiuchumi (processes, principles, values, and justice). Kuna michakato mitano, yaani uzalishaji, usambazaji, mauziano, utumiaji wa huduma na bidhaa, na uwekezaji (production, distribution, exchange, consumption and investment). Kuna kanuni kuu tatu zinazotumika kuratibu michakato iliyomo katika sekta ya uchumi, yaani kanuni za ushindani, ushirikiano, na uingiliaji kati kupitia mkono wa serikali ili kudhibiti madhara hasi ya ushindani na ushirikiano unaotokea sokoni (competition, cooperation, and intervention). Na kuna tunu tatu zinazohuisha malengo ya kiuchumi, yaani uhuru, mshikamano, na usawa (freedom, solidarity and equality); ambapo, tunu ya uhuru ni chimbuko la kanuni ya ushindani, tunu ya mshikamano ni chimbuko la kanuni ya ushirikiano, na tunu ya usawa ni chimbuko la kanuni ya uingiliaji kati. Katika Ilani ya CCM (2020-2025), ahadi kuhusu ahadi kuhusu ujenzi wa miundobinu ya kiuhumi ziko katika ibara ya 12-76. Baada ya kusoma ilani hii nimebainisha vipengele 38 vya kisera vinavyopaswa kufanyiwa kazi ili kuzalisha mfumo wa uchumi unaojali maslahi ya watu wote.
  1. Kuna ahadi juu ya ushirikishaji wa sekta binafsi katika uwekezaji, uwezeshaji wa wananchi kiuchumi, na kuzalisha ajira kwa vijana, kusimamia vyama vya ushirika, kilimo, ufugaji, uvuvi, viwanda, biashara na mfumo wa kodi, vituo atamizi kwa ajili ya kuzalisha wajasiriamali, na kubuni sera za kifedha zinazoruhusu mzunguko wa fedha wenye kasi kubwa ya kuhakikisha kwamba fedha inapita katika mfuko wa kila raia anayejishughulisha.
  2. Pia, kuna ahadi juu ya barabara za chini, madaraja, makalvati, mizani ya kupima magari, vivuko, bandari, reli, viwanja vya ndege, na mawasiliano ya simu.
  3. Aidha, kuna ahadi juu ya ujenzi wa barabara za juu (Flyovers) zifuatayo ili kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam, kwenye makutano ya barabara katika maeneo yafuatayo: Chang’ombe, Uhasibu, Kamata, Morocco, Mwenge, Magomeni, Tabata, Fire, Makutano ya Ally Hassan Mwinyi na United Nation, na Makutano ya Ally Hassan Mwinyi na Kinondoni. (Ilani ya CCM 2020-2025, ib. 55(e)(i)).
  4. Kadhalika, kuna ahadi juu ya nishati ya umeme, nishati ya mafuta, nishati ya gesi asilia, madini, utalii, maliasili, matumizi bora ya ardhi, na kuendesha sekta ya utamaduni, sanaa na michezo kibiashara.
VII. MUHTASARI, HITIMISHO NA MAPENDEKEZO
  1. Muhtasari: Ahadi zote zilizo katika ilani ya CCM, zinaweza kugawanywa, bila kubaki, katika makundi matano. yaani: Afya, Elimu, Ikolojia, Ofisi za uongozi, na Uchumi (A-E-I-O-U). Nimefupisha Ilani yenye kurasa 303 za maneno 103,640 katika kurasa 3 za maneno 1,507; maneno ambayo ni sawa na 1.5% ya maneno ya awali.
  2. Hitimisho: Napenda kuhitimisha kwa kusema kwamba muhtasari huu wa ahadi katika sekta za afya, elimu, ikolojia, ofisi za utawala na uchumi, utaweza kutoa fursa kwa wadau wa maendeleo kufuatilia yanayojiri katika korido za serikali kuu na serikali za mitaa kuanzia Januari mosi 2021.
  3. Mapendekezo: Ahadi ni deni na muungwana ni vitendo. Kwa hiyo, naikumbusha serikali mpya kufanya kazi kwa ari zaidi, nguvu zaid na kazi zaidi, ili siku moja Tanzania Mpya izaliwe ikiwa inafanana na Mji wa "California," kama tulivyoahidiwa wakati wa kampeni. Lakini, kusudi ndoto hiyo itimie, nashauri kwamba yafanyike marekebisho kadhaa kwa ajili ya kuboresha kasi na ufanisi wa muundo wa utawala wa nchi (pichani chini). Kwa mfano, naona kwamba, Wizara ya TAMISEMI ni dude kubwa linalopaswa kuwa na Manaibu Waziri watatu wenye majukumu tofauti yanayokamilishana. Hao ni: Naibu Waziri wa TAMISEMI CITIES, Naibu Waziri wa TAMISEMI MUNICIPALITIES na Naibu Waziri wa TAMISEMI RURAL kwa ajili ya maeneo baki. Kwa sasa, sekta za " Halmashauri, Miji na Manispaa" zinayumba sana.
Mchoro: Muundo wa Serikali ya Tanzania ukionyesha mwingiliano kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa
1609125910803.png

Chanzo:Henry A. Mollel (2010), Participation for local development: The reality of decentralization in Tanzania (Leiden: African Studies Centre, African Studies Collection, vol. 29), uk. 18. (NB: Natambua kwamba tangu 2015 majukumu ya PMO-RALG yako chini ya PO-RALG)

Kwa leo sina la ziada.

Nawatakia Mwaka Mpya wa 2021.

Karibuni Sumbawanga!

Kwetu kuchele!
 
Nitoke nje ya mada: sikufahamu lakini inaonekana wewe ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa uandishi na kujenga hoja!

Uzi wako ulivyoelezea udhaifu wa hoja za uteuzi wa baraza la mawaziri uliotaka kuzingatia hoja za kidemografia na ukanda ulinifurahisha sana.

Najifunza kupitia kwako.

Wasalam

Mwakilishi wa Ziwa Natron.
 
Asante Mwakilishi wa Ziwa Natron!
Bado huko Ziwa Natron magadi yapo?
 
View attachment 1660856
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Dk. John Pombe Joseph Magufuli

I. UTANGULIZI

  1. Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020 umekwisha. Tayari CCM imepata wabunge 261 kati ya wabunge 264 wa majimbo, sawa na 98.86%; mgombea urais wa CCM ametangazwa na NEC kama mshindi halali, na ameunda serikali itakayotafsiri Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.
  2. Sera zote zilizo katika ilani za vyama vyote vya siasa, zinaweza kugawanywa, bila kubaki, katika makundi matano. Makundi hayo ni: Afya, Elimu, Ikolojia, Ofisi za uongozi, na Uchumi. Nakumbuka maeneo haya matano kwa msaada wa vokali tano za Kiswahili, yaani “A, E, I, O, U.”
  3. Kwa kuzingatia haya, katika aya zifuatazo nafupisha ahadi zote 90 nilizoziona kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 ili kuweka rejea murua itakayotusaidia kufanya ufuatiliaji na tathmini ya kazi za serikali kuanzia 01 Januari 2021.
II. AFYA: Afya ni hali ya binadamu kuwa na mwili na akili vyenye kutenda kazi zake barabara. Hali hii ni matokeo ya kuwa na kinga dhidi maradhi yanayoambukiza na yasiyoambukiza, mkamilishano thabiti kati ya nafsi na mwili, na masikilizano kati ya mwili na mazingira yake, ambapo mazingira yanahusisha makazi, malazi, chakula na jamii ya watu wanaomzunguka mhusika. Katika Ilani ya CCM (2020-2025), ahadi kuhusu afya ziko katika ibara za 81-100. Baada ya kuipitia Ilani hii, nimejiridhisha kwamba, kuna sera 16 ambazo zinapaswa kutekelezwa na serikali yake ili kukuza na kuhami afya ya kila raia.
  1. Kuna ahadi kuhusu ujenzi na ukarabati wa vituo vya huduma za afya, ushirikishwaji wa sekta binafsi katika huduma za afya, upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, upatikanaji wa watumishi na mabingwa wa kada ya afya, na sera ya mapambano dhidi ya magonjwa ya mlipuko.
  2. Pia, kuna ahadi kuhusu mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza, mapambano dhidi ya magonjwa yanayotokana na virusi kama vile VVU, upatikanaji wa mlo kamili na bora, na sera ya uduma za ustawi wa wazee.
  3. Aidha, kuna ahadi kuhusu huduma za ustawi wa watoto na familia, huduma za watu wenye ulemavu, kusimamia upatikanaji wa maji na usafi wa mazingira, kusimamia mipango miji na mipango vijiji, sera ya ujenzi wa nyumba na makazi bora, sera ya bima ya afya kwa wote, na sera ya afya ya mama na mtoto. Lakini, katika ilani hii, haikutajwa ahadi ya “bima ya afya kwa watu wote.” Hii ni ahadi ya jukwaani.
III. ELIMU: Elimu ni mchakato wa kupata taarifa, maarifa na ufundi wa kufanya utafiti na kubuni tekinolojia za kumsaidia mwanafunzi aliyefuzu kuyamudu mazingira yake ya kimaumbile, kiuchumi, kisiasa, kijamii, kiutamaduni. Katika Ilani ya CCM (2020-2025), ahadi kuhusu elimu ziko katika ibara za 78-80, na ahadi kuhusu sayansi na tekinolojia ziko katika ibara za 101-103. Baada ya kupitia ilani hii, nimeona kuwa sekta hii itaboreshwa kwa kupitia utekelezaji wa mikakati ya kisera 10.
  1. Kuna ahadi kuhusu elimu ya msingi, elimu ya sekondari , elimu ya ufundi stadi, na sera ya elimu ya Juu.
  2. Pia kuna sera za kuanzisha makampuni ya katika sekta mbalimbali ili kuendeleza sayansi, teknolojia na ubunifu; kujenga mfumo wa Taifa wa ubunifu (national innovation system); na sera ya kuendeleza vituo atamizi kwa ajili ya kukuza na kuendeleza ubunifu wa kisayansi na kitejinolojia.
  3. Kadhalika, kuna ahadi kuhusu kuhamasisha matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu katika uzalishaji, usambazaji, na utawala kwa kutumia tekinolojia ya kidijitali; kuanzisha vituo vya umahiri wa sayansi na teknolojia (centres of excellence) katika taasisi za elimu ya juu; na sera ya kuimarisha mafunzo ya walimu wa sayansi, teknolojia na ufundi katika ngazi za shule za msingi, shule za sekondari, vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi na vyuo vikuu.
IV. IKOLOJIA: Neno "ikolojia" linamaanisha mazingira. Mazingira ya binadamu yanajumuisha wanyama, mimea, wadudu, hewa, maji na vitu vyote vilivyo baki vilivyoko ardhini, angani, majini, msituni, porini, pamoja na michakato yote ya kibayolojia inayomfungamanisha kila binadamu pamoja na vitu hivi kupitia mitandao ya vyakula vya viumbe anwai (ecological food web). Katika Ilani ya CCM (2020-2025), ahadi kuhusu ikolojia ziko katika ibara ya 9B(vii). Baada ya kupitia Ilani hii, na kukagua mikakati ya kutunza mazingira iliyoko katika tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais, nimebaini kuwa, kuna mikakati 10 ya kisera inayoweza kutekelezwa ili kukuza na kuhami mfumo wa ikolojia ulio salama kwa uhai wa binadamu na viumbe baki.
  1. Kuna ahadi juu ya kuhimiza watu kuepuka kadiri inavyowezekana kutumia nishati zinazozalisha hewa ya ukaa ambayo ni chanzo kikuu cha mabadiliko ya tabia nchi; kuwekeza katika miradi ya kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi (climate adaptation strategies); na kuwekeza katika miradi ya kupunguza ukubwa wa vyanzo vya mabadiliko ya tabia nchi (climate mitigation strategies).
  2. Aidha kuna ahadi juu ya kuhifadhi uoto wa asili ulioko juu ya nchi, kuhifadhi uoto wa asili ulioko majini, kuhifadhi wanyama wa porini, kuhifadhi wanyama wa majini, kuzuia mmomonyoko wa ardhi, na kunzisha mfuko maalum kwa ajili ya utafiti, usimamizi na tathmini juu ya hali ya hewa na mabadiliko ya tabianchi.
  3. Kadhalika kuna ahadi juu ya kuzuia uchafuzi wa mazingira unaofanyika kupitia uzalishaji wa takangumu; uzuia uchafuzi wa mazingira unaofanyika kupitia uzalishaji wa takamaji; na uzuia uchafuzi wa mazingira unaofanyika kupitia uzalishaji wa takahewa.
V. OFISI ZA UTAWALA: Utawala bora ni aina ya utawala ambao unahakikisha kuwa utaratibu wa kufanya maamuzi na kutekeleza maamuzi hayo kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa jamii unazingatia misingi ya utu, uhuru, haki, ushirikishwaji, demokrasia, uwajibikaji, uhasibikaji, uwazi, tija, ufanisi, usawa mbele ya sheria, na ushiriki wa makundi yote ya jamii. Katika Ilani ya CCM (2020-2025), ahadi kuhusu ofisi za utawala bora ziko katika ibara ya 108-130. Baada ya kupitia ilani hii nimjiridhisha kuwa kuna jumla ya sera 16 zinazopaswa kutekelezwa kwa ajili ya kufanikisha dhana ya utawala bora.
  1. Kuna ahadi juu ya kuheshimu haki ya kujitawala katika ngazi za chini za serikali kwa kugatua madaraka, kusimamia maadili katika utumishi wa umma, kufanya mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi, kuheshimu misingio ya demokrasia na haki za binadamu, kuheshimu katiba na kuzingatia utawala wa matakwa ya sheria, na sera ya kuhuisha usawa wa jinsia katika sekta ya umma na sekta binafsi.
  2. Pia, kuna ahadi juu ya kuhami uhuru wa vyombo vya habari, kuheshimu uhuru wa raia kujieleza na kuwasiliana, kuhesimu uhuru wa asasi za kiraia, kulinda uhuru wa kuabudu, kulinda haki za wafanyakazi na uhuru wa vyama vya wafanyakazi, na sera ya kukabiliana na majanga ya asili kwa kuzingatia kanuni ya utawala auni (principle of subsidiarity).
  3. Kadhalika, kuna ahadi juu ya kupambana na dawa za kulevya, menejimenti ya mahusiano ya kisiasa na kiuchumi katika ngazi ya kimataifa, menejimenti ya kidemokrasia ya vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi, na sera ya kuzuia utekaji, utesaji na uteketezaji wa uhai wa raia wasio na hatia.
VI. UCHUMI: Uchumi ni mfumo unaojumuisha mambo makuu manne, yaani, michakato, kanuni za uratibu wa michakato hiyo, tunu zinazowaunganisha watendaji, na misingi ya ustaarabu wa kiuchumi. Kuna michakato mitano, yaani uzalishaji, usambazaji, mauziano, utumiaji wa huduma na bidhaa, na uwekezaji. Kuna kanuni kuu tatu zinazotumika kuratibu michakato iliyomo katika sekta ya uchumi, yaani kanuni za ushindani, ushirikiano, na uingiliaji kati kupitia mkono wa serikali ili kudhibiti madhara ya ushindani na ushirikiano unaotokea sokoni. Katika Ilani ya CCM (2020-2025), ahadi kuhusu ofisi za utawala bora ziko katika ibara ya 12-76. Baada ya kusoma ilani hii nimebainisha vipengele 38 vya kisera vinavyopaswa kufanyiwa kazi ili kuzalisha mfumo wa uchumi unaojali maslahi ya watu wote.
  1. Kuna ahadi juu ya kubuni mzunguko wa kifedha wenye kasi kubwa ya kuhakikisha kwamba fedha inapita katika mfuko wa kila raia anayejishughulisha, ushirikishaji wa sekta binafsi katika uwekezaji, uwezeshaji wa wananchi kiuchumi, na kuzalisha ajira kwa vijana, kusimamia vyama vya ushirika, kilimo, ufugaji, uvuvi, viwanda, biashara na mfumo wa kodi, na vituo atamizi kwa ajili ya kuzalisha wajasiriamali.
  2. Pia, kuna ahadi juu ya barabara za chini, madaraja, makalvati, mizani ya kupima magari, vivuko, bandari, reli, viwanja vya ndege, na mawasiliano ya simu.
  3. Aidha, kuna ahadi juu ya ujenzi wa barabara za juu (Flyovers) zifuatayo ili kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam, kwenye makutano ya barabara katika maeneo yafuatayo: Chang’ombe, Uhasibu, Kamata, Morocco, Mwenge, Magomeni, Tabata, Fire, Makutano ya Ally Hassan Mwinyi na United Nation, na Makutano ya Ally Hassan Mwinyi na Kinondoni. (Ilani ya CCM 2020-2025, ib. 55(e)(i)).
  4. Kadhalika, kuna ahadi juu ya nishati ya umeme, nishati ya mafuta, nishati ya gesi asilia, madini, utalii, maliasili, matumizi bora ya ardhi, na kuendesha sekta ya utamaduni, sanaa na michezo kibiashara.
VII. HITIMISHO NA MAPENDEKEZO

Nimejitahidi kufupisha kitabu chenye kurasa 303 katika kurasa 3 pekee, zenye maneno 1,424. Matarajio yangu ni kwamba muhtasari huu utatoa fursa kwa wadau wa maendeleo kufuatilia yanayojiri katika korido za serikali kuu na serikali za mitaa kuanzia Januari mosi 2021. Ahadi ni deni na muungwana ni vitendo. Nawatakia Mwaka Mpya wa 2021.

Karibuni Sumbawanga!

Kwetu kuchele!
Umesikia wapi mwizi anatimiza ahadi? Mwizi ni kama jogoo. Humlaghai kuku mtembe kwa kumwita eti alipo kuna chakula. Kuku mtembe akifika, anaishia kumpanda kisha anaondoka zake. Hakuna chakula wala nini. CCM kwa kuiba kura na ahadi za kipumbavu kimetufanya Watanzania kuku mtembe. CCM, asante kwa kutupanda bila kutupa chakula.
 
Umechambua vuzuri sana ubarikiwe kwa hilo,tukirudi kwenye mada naweza kusema sioni good strategies za kuweza kutekeleza hayo yote,baadala yake ni porojo tu hakuna cha ziada .Baada ya miaka mitano utakuja kuona ninacho kisema .
 
CCM kwa kuiba kura na ahadi za kipumbavu kimetufanya Watanzania kuku mtembe.
Kauli hii inayo mapungufu ya kiepistemolojia.

Kauli kwamba chama cha "CCM" kimetoa "ahadi za kipumbavu" haikubaliwi na watu wote. Kwa hiyo, kunahitajika utetezi kwa kuweka ushahidi mezani. Kwa hakika, bandiko hili ni ushahidi dhidi ya kauli hii.

Aidha, kauli kwamba chama cha "CCM" ni "mwizi" mwenye ufundi wa "kuiba kura" haikubaliwi na watu wote. Kwa hiyo, kunahitajika utetezi kwa kuweka ushahidi mezani. Kuhusu kauli hii, hebu leta ushahidi au ibatilishe.

Karibu.
 
naweza kusema sioni good strategies za kuweza kutekeleza hayo yote,baadala yake ni porojo tu hakuna cha ziada .Baada ya miaka mitano utakuja kuona ninacho kisema .

Kauli yako ni utabiri, yaani extrapolation/prediction.

Utabiri unakuwa na msingi wa ushahidi wa kuanza nao.

Kwa mfano ili uchore mstari ulionyooka kwenye X-Y plane, unahitaji angalau ponti mbili kama vile (x,y)=(2,3) na (x,y)=(5,6). Sasa msingi wa extrapolation yako ni upi?

Weka ushahidi mezani.
 
Kauli hii inayo mapungufu ya kiepistemolojia.

kauli kwamba chama cha "CCM" kimetoa "ahadi za kipumbavu" haikubaliwi na watu wote. Kwa hiyo, kunahitajika utetezi kwa kuweka ushahidi mezani. Kwa hakika, bandiko hili ni ushahidi dhidi ya kauli hii.

Aidha, kauli kwamba chama cha "CCM" ni "mwizi" mwenye ufundi wa "kuiba kura" haikubaliwi na watu wote. Kwa hiyo, kunahitajika utetezi kwa kuweka ushahidi mezani. Kuhusu kauli hii, hebu leta ushahidi au ibatilishe.

Karibu.
Unataka ushahidi gani, kwani waliyoyatenda ccm kwa kuiba kura hukuyaona?
 
Kwamba Kura za maBEGI hazikuwepo Ila ccm inapendwa
Really????!

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
😂kulinda demokrasia
🤣kulinda uhuru wa habari
😅kuheshimu utawala Bora nk. nk.
Hadithi ya kufikirika kwa Jiwe
 
Bado ahadi za kuboresha mishahara ya wafanyakazi sijajua hii iko ukurasa wa ngapi
 
Ahadi na maendeleo ,zitatekelezwa,kwa sababu CCM wamebaki pekee yao,
Wapinzani walikuwa wanachelewesha maendeleo..
 
Unataka ushahidi gani, kwani waliyoyatenda ccm kwa kuiba kura hukuyaona?

Sikuona.

Hata kama ningeona, baada ya mimi kuandika bandiko hiki, maana yake ni kwamba, the onus of proving theft is on your side, because you have made the allegation.

Hivyo ndivyo rules of logical engagement zinavyotufundisha.

Karibu
 
Nilidhani Kaja na uchambuzi kumbe propaganda za cccm jinga kabisa

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app

Nimefanya uchambuzi kwa kutumia mfumo wa AEIOU lkn unasema huo sio uchambuzi. Kwako uchambuzi ni kitu gani na sio kitu gani?

Nisikilize vizuri kuhusu haya yafuatayo:

1. Ktk utaratibu wa kuendesha nchi, gurudumu la maendeleo lazima lisonge mbele ama kupitia mikono ya serikali halali au serikali haramu. Yaani, ni bora kuwa na serikali haramu kuliko kutokuwa na serikali kabisa. Mtaalam yeyote wa politology atakuthibitishia jamo hili.

2. Tayari CCM imetangazwa mshindi na kuunda serikali kwa ajili ya kutekeleza ilani yake. Kwa hiyo, mwelekeo wa kisera wa Taifa la Tanzania ni maudhui ya Ilani ya CCM ya 2020 - 2025, utake usitake.

3. Uhalali wa serikali ya CCM ya sasa unapingwa na Chadema wanaodai kuwa mgombea wao wa kiti cha urais alishinda na kwamba wangekuwa na wabunge wengi kuliko CCM kama kura zingehesabiwa kwa haki. The onus of proof is on their side.

4. Uwezo wa Chadema kuongoza nchi kama ikishinda uchaguzi leo unatiliwa shaka kubwa na wachambuzi wa masuala ya siasa za kidola. Sababu kuu nne zinatajwa: ukabila unaofungamana na ukanda wa kaskazini wenye kuratibiwa na watu wachache ndani ya chadema waitwao CHADEMADEFENCE MASTERS, udini unaoifungamanisha chadema na madhehebu ya ulutheri, usiasa-biashara unaoifanya chadema iendeshwe kama biashara ya chagga defense masters (yaani politico-business kama ambavyo tunaongelea agribusiness, etc), na tishio la kiusalama dhidi ya nchi kwa sababu ya ilani ya chadema kutamka kuwa wataweka rehani madini yaliyoko ardhini kama dhamana ya mikopo kutoka sehemu kadhaa duniani. Ushahidi uliopo mikononi mwangu unanifanya kuamini tuhuma hizi.

5. Katika bandiko hili mimi nineamua kuandika juu ya item no. 2 above na sio vinginevyo. Kila jambo na wakati wake. Nimeamua hivyo na ni haki yangu.

6. Kwa hiyo, tujenge hoja bila matusi wala kelele. Hoja inapanguliwa kwa hoja, na hoja mbili hazijadiliwi kwa mpigo.

7. Hivyo, ktk hayo hapo juu nitabadili mitazamo yangu kutokana na ushawishi wa hoja na sio vinginevyo.

Acha matusi ya makuli wa bandarini.
 
Kwamba Kura za maBEGI hazikuwepo Ila ccm inapendwa
Really????!

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app

Hizo taarifa ni sahihi kwa kiasi gani? Mabegi yalikutwa katika vituo vingapi kati ya vituo 800+? Na mabegi hayo yalikuwa na kura kweli? Kuna tofauti kati ya facts na hearsay. Bandiko langu linakaribisha verified data.

Karibu
 
Ukosoma ila za vyama vyetu karibu zote zinalingana na kufanana kimitazamo hivyo mjadala unakuwa nani anaouwezo wa kusimamia aliyaazimia.

Rais kikwete aliwahi kusema kuwa tatizo la mgombea hana chake juu ya ilani iweje wanakujazia mambo mengi ukahangaike nayo

Mfano hili la elimu bure mimi silikubal kabisa ni uhuni tu hii agenda ilikuwa ya chadema ya uwongo na ccm tukaingia cha kike kwa sasa haieleweki maana wazazi tunataka elimu bora sio bora elimu hii ya kwenda mbele tu
 
Wakati wa uchaguzi nilifanya comparative analysis ya ilani za CDM na CCM katika maeneo haya matano: afya, elimu, ikolojia, ofisi za utawala na uchumi.

Kulikuwepo na tofauti. Mfani, CCM walipata alama nyingi ktk sekta ya uchumi na kupata alama kidogo ktk sekta za afya, elimu na mazingira.

Na chadema walipata alama kidogo katika sekta ya uchumi na kupata alama nyingi ktk sekta ya afya, elimu na mazingira.

Ukifuatilia mwenendo wa kampeni utaona kuwa ccm walichukua sera ya bima ya afya kwa wote ili kutip mizania ya kampenj. Haikuwemo ktk ilani yao.

Kwa hiyo, kuna ufanano na utofauti wa hapa na pale.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom