Serikali msiwafutie Watoto matokeo, toeni matokeo yao haraka. Hawana hatia. Tatizo ni Mfumo

Mtoto kaibishwa mitihani kwa kutishwa. Badala ya kukamata waalimu wanawaadhibu watoto wasio na hatia.
Lazima tuwapime upya watoto kwa mitihani mingine itakayotungwa upya na adhabu ni muhimu wajue wizi na udanganyifu ni kosa maana hatutaki kizazi kitakachoona ni kawaida kufanya udanganyifu mwisho wa siku wataishia kushangilia wizi wa kura unaofanya na CCm
 
Nasikitika vyombo vya habari vipo kimya.
What is this country. !?

Na wazazi ambao watoto wao wamedhulumiwa haki hii ya kufurahia kuhitimu kwa wanao watakaa kimya..

What is this country.!?

Lakini wanasheria nguli kina Kibatala na wengineo wako wapi!?

Damn.

Mtoto huyu wa miaka 12, 13, 14 tumeathiri maisha yake yote kwa kumuita 'cheat' bila hatia yeyote.

This mustn't go unsaid..
Pole mkuu una machungu dah ,huenda kama si mwanao yamemkuta au wa jirani dah
 
Alafu haya ni matokeo ya ccm na serikali hii ya kijambazi.......
Kwa nn ccm hawajafutiwa matokeo ya wizi wa kura lkn wanawaonea watoto wadogo walioiga tu tabia za maccm?
 
Kama umefika daraa la Saba na hamjui maana ya kuna huyu mtoto huko mbele atakuwa very corrupt nawapa kongole Necta..... waalimu nao wana makosa yao kila mtu ashinde mechi yake......
Unawapa kongole kwa kuruhusu mitihani yao kuvuja? Ningekuwa mimi kqenye mamlaka huyo waziri hana kazi
 
Darasa la saba ana hatia gani? Kama vp wawape mtihani tofauti wawapime kivyao hao wanaofutiwa.
acheni kujichetua akili ninyi. msichanganye elimu na siasa. Mmewahi mark hata mitihani ninyi au mnaongea ongea tu. mnajua hata mitihani inavyotungwa, mnazijua gharama za kutunga mitihani. Mmewahi fundisha ninyi. Kama hamjui kaeni kimya acheni kuingilia kazi za watu.
 
Sina haja ya ku mark mtihani kujua process ya kuandaa mtihani. Huo ujinga wa kufuta mtihani wa darasa la saba ni hapa kwenu tu huko duniani huwezi kuusikia.

Ni upumbavu uliopitiliza. Mwisho mtakuja kifuta na darasa na nne kwakuwa uwezo wenu ndio ulipoishia. Badala ya kutafuta source mnaenda kwenye matokeo.
 
Sasa huko ni kwingine hapa ni Tanzania. Kama shule yako iliiba mtihani unategemea tukuachie achie tu. Lazima uasibiwe kwa mjibu wa sheria za Baraza la mitihani. Baraza lina sheria zake ndio hizo zinafanya kazi. Shule yako ikiiba mtihani inafutiwa matokeo hiyo ndo adhabu. Labda ungeomba waongeze adhabu za kunyongwa. Unataka wabadirishiwe mtihani kwa gharama za nani. Kwa muda upi
 
Huyo mtoto hata akiua mtu haendi jela wewe unamfutia mtihani huo ni upunguaji.

Hao wanaokaa kuwafutia watoto mitihani naona hawajawahi kuwa watoto kwenye maisha yao wamejikuta wakubwa. Kama wangejua psychological impact kwa hao watoto wasingefanya maamuzi ya kijinga.

Hii kitu watakaa nayo hawa watoto for the rest of their lives. Na itawapotezea uwazo wao wa kujiamini. Again haishangazi coming from wasomi wetu wa PHDs ambazo hazijui kufanya 2+2
 
wewe itakua shule yako iliiba mtihani.
 
Huo ndio Ukweli watajwa ndio wezi wa Mitihani kisa wanataka waonekane wanafaulisha sana
 
Mtoa mada hilo swala dr msonde leo ameongelea kupitia tbc baada ya kubanwa sana na mtangazaji majibu yake amesema hiyo imekula kwao maana hata hao wanafunzi wamefanya makosa maana kupitia seminar mbali mbali walionywa kutokufanya udanganyifu au wangetoa taarifa mapema.

Pia amesema adhabu kali itatolewa kwa waalimu pamoja na wasimamizi walio husika baada ya uchunguzi kukamilika.
Kwa taarifa kamili fatilia tbc aridhio leo jioni utasikia mengi kuhusu hilo swala.
Mtangazaji pia angemuuliza uyo msonde ,kwani waalimu hawakupewa semina kuhusu wiz wa mitihan ,sasa kama mwalim tu ameshindwa kuzingatia itakua mwanafunz
 
Hivi huko Danganyika Republic hakunaga mahakama?

Maana huwa mnanishangaza.... kila mtu anampigia magoti magufuli.

Magufuli fanya hivi, magufuli fanya vile, magufuli tunaomba choo....

Leo wewe unamuomba magufuli aiamuru NECTA?

Hizo mahakama zenu huwa ziko kwa ajili ya nini?

Ni mahakama BUTU kiasi cha kushindwa kutoa amri za kuzuia na kuagiza maafisa wa NECTA?
Tanzania hii mwenye amri zote ni Magufuli hakuna kitu kinaitwa mahakama nchi hii.

Mahakama ni tawi la ccm mahakimu na majaji ni wanachama na Mwenyekiti wao ni Magufuli.

Hao watoto juzi tu walikuwa wanasombwa kwa malori kupelekwa viwanja vya mikutano ya ccm, walivishwa na Mandela na T shirt na kofia za ccm,kwanini leo wasiachwe tu iwe sehemu ya ujira wao kujaza vichwa kwenye kampeni zao?!
 
Mitano Tenaaaa!!!!

Mmebaki peke yenu sasa maana Chadema walikua wanachelewesha maendeleo ...

Maendeleo ya elimu veeeepe!!! hiyo ni mitihani ya darasa la saba tu sikwambii vyuo vikuu ni balaaaa na nusu
 
Kuna mambo ya hovyo sana yanatokea nchini humu.

Hivi Mwl. Anakaa chooni na Majibu alafu wanawapanga watoto waende chooni kwa zamu kuchukua majibu.

Hivi hapo Kwanini tumuhukumu kijana huyu mdogo kabisa.

Lakini kwa nchi hii ilivyo ya kijinga. Hili nalo litapita. Na kamati ya ulinzi na usalama ya mitihani mkoa wataendelea kula mshahara.

Hili mimi silikubali.

MATAGA najua mpo happa. Mwambieni RAIS alitazame hili.
Kuna jirani yangu ni Mwl amenieleza hivyo hivyo, nikamshangaa sanaa ila akajitetea kwamba mbona inafanyika kila mwaka ili kuokoa shule isipate adhabu na Mwl Mkuu kuondokewa? It seems coordination inaanzia wilayani.
 
Shule ya MSINGI ni mtoto mdogo Sana....

Anapata wapi FEDHA ya kununua "dhambi" ya mtihani ULIOVUJA kama si KUWEZESHWA na wazazi/walezi?!!!

Yaani HILI LIACHWE LIPITE?!!!

Acheni zenu banaaa....

Hapo wala HAKOMOLEWI mtoto mdogo huyo UNDER 15....

Kwenda na mwendo huu wa KUFUMBIA maovu ni UZWAZWA uliopitiliza....

Dunia hii ya ELIMU eti URUHUSU ujinga wa KUVUJA/KUVUJISHWA/KUUZA NA KUNUNUA MITIHANI?!!!!pathetic.....
 
Back
Top Bottom