Nawashauri Serikali wakiweka Siasa kwenye swala hili la Ngorongoro hii mbuga baada ya miaka itakuwa tatizo. Kuwahamisha wamassai kule ni lazima kama wana nia njema. Waziri mkuu ameweka siasa zaidi. Tunaongelea watu pekee wakati tatizo kubwa ni mifugo karibu 1M. Waandishi wa habari wametenda haki kwenye hili🙏
Ndugu zetu Wamassai na Wamang'ati wamekuwa na ufugaji kiholela karibu Tanzania nzima. Kwa ufupi hawa wafugaji wanaishi kwa utaratibu wao wenyewe bila kufuata sheria yeyote. Lakini kibaya zaidi wanaharibu mazingira sana na ni lazima kuwekwe utaratibu. Huko Arusha ndiyo kabisa kumekuwa kama jagwa na sasa wameingia Ngongogoro.
Ushauri wangu ni kwa serikali kuanzisha mbuga maalumu za wafugaji. Mbuga hizi ziwe na wataalamu wa mazingira, lakini wawekewe huduma muhimu kama Watanzania wengine. Mbuga hizi za wafugaji ziwe kila pande kuu za nchi . Kwa mtazamo wangu mbuga kuu kumi zinatosha. Huko ndani watengenezewe mabwawa, kuwe na utaratibu wa mupanda miti na majani ya chakula cha mifugo. Kitu kizuri kimoja ni kwamba mchango wa kuingia huko au kodi ni hiyo hiyo mifugo. Hivyo wafugaji ni lazima wachangie mifugo kama kodi ili waweze kuwekewa huduma za mbuga na uwekezaji. Kwa ufupi serikali iwasaidie wawe na ushirika wa wafugaji ndani ya hizi mbuga maalumu. Serikali itafaidika kwa mambo yafuatayo
1. Itasaidia kulinda mazingira
2. Itasaidia wafugaji kuweza kuuza mifugo yao kwa utaratibu
3. Itapunguza migongano ya wakulima na wafugaji
4. Itasaidia kuwatambua na kuwapa vibali wafugaji
5. Itasaidia wafigaji kupata huduma kama za Afya na Elimu
6. Itasaidia serikali kupata kodi
Bila hizi tutakuwa na matatizo. Ngombe wao hawana afya nzuri, pesa hawana na wanakaa na ngombe mpaka wafe. Lakini kwa hali ya hewa inavyoendelea tutakuwa na migogoro zaidi.
Nimesikia serikali inataka kuwahamishia Handeni je kuna utaratibu gani wa kuhakikisha Handeni haiwi jagwa?
Je serikali imeweka wataalamu wa mazingira na kilimo?
Je migogoro ya wakulima wengi wa mahindi na wafugaji utaratibu gani serikali imeweka kukabili?