Serikali mkiweka siasa Ngorongoro hamtapata suluhisho

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,605
8,744
Nawashauri Serikali wakiweka Siasa kwenye swala hili la Ngorongoro hii mbuga baada ya miaka itakuwa tatizo. Kuwahamisha wamassai kule ni lazima kama wana nia njema. Waziri mkuu ameweka siasa zaidi. Tunaongelea watu pekee wakati tatizo kubwa ni mifugo karibu 1M. Waandishi wa habari wametenda haki kwenye hili🙏

Ndugu zetu Wamassai na Wamang'ati wamekuwa na ufugaji kiholela karibu Tanzania nzima. Kwa ufupi hawa wafugaji wanaishi kwa utaratibu wao wenyewe bila kufuata sheria yeyote. Lakini kibaya zaidi wanaharibu mazingira sana na ni lazima kuwekwe utaratibu. Huko Arusha ndiyo kabisa kumekuwa kama jagwa na sasa wameingia Ngongogoro.

Ushauri wangu ni kwa serikali kuanzisha mbuga maalumu za wafugaji. Mbuga hizi ziwe na wataalamu wa mazingira, lakini wawekewe huduma muhimu kama Watanzania wengine. Mbuga hizi za wafugaji ziwe kila pande kuu za nchi . Kwa mtazamo wangu mbuga kuu kumi zinatosha. Huko ndani watengenezewe mabwawa, kuwe na utaratibu wa mupanda miti na majani ya chakula cha mifugo. Kitu kizuri kimoja ni kwamba mchango wa kuingia huko au kodi ni hiyo hiyo mifugo. Hivyo wafugaji ni lazima wachangie mifugo kama kodi ili waweze kuwekewa huduma za mbuga na uwekezaji. Kwa ufupi serikali iwasaidie wawe na ushirika wa wafugaji ndani ya hizi mbuga maalumu. Serikali itafaidika kwa mambo yafuatayo

1. Itasaidia kulinda mazingira
2. Itasaidia wafugaji kuweza kuuza mifugo yao kwa utaratibu
3. Itapunguza migongano ya wakulima na wafugaji
4. Itasaidia kuwatambua na kuwapa vibali wafugaji
5. Itasaidia wafigaji kupata huduma kama za Afya na Elimu
6. Itasaidia serikali kupata kodi

Bila hizi tutakuwa na matatizo. Ngombe wao hawana afya nzuri, pesa hawana na wanakaa na ngombe mpaka wafe. Lakini kwa hali ya hewa inavyoendelea tutakuwa na migogoro zaidi.

Nimesikia serikali inataka kuwahamishia Handeni je kuna utaratibu gani wa kuhakikisha Handeni haiwi jagwa?
Je serikali imeweka wataalamu wa mazingira na kilimo?
Je migogoro ya wakulima wengi wa mahindi na wafugaji utaratibu gani serikali imeweka kukabili?
 
Mkiwaendekeza wafugaji huko huko mbeleni wataiuaa hifadhi yote,ngorongoro itabakia jina
Tu

Ova
 
Nchi hii wafugaji wanaonekana Kama wavamizi kila sehemu wakienda wanafukuzwa

Huko ngorogoro hakuna wakulima wanaishi bila tatizo wala migogoro badala yake mnataka muwatoe sijui mnataka kuwapeleka wapi?? huko ambako wataishi bila kuharibu hayo mnayoyaita mazingira yenu.

Waharibifu wakubwa wa mazingira nchi ni wakulima wala sio wafugaji, wakataji wa miti nchi hii ni wakulima sio wafugaji

Badala mpambane na wakulima wanaosababisha jangwa wanaokata miti ovyo ili wapate maeneo ya kulima mnaenda kupambana na wafugaji ambao ni watunzaji wazuri wa mazingira

Shezzy type
 
Matatizo yote ktk nchi hii yanaanzishwa na wafugaji
Nchi kubwa hii,wafugaji watafute maeneo mengine waache uvamizi wa maeneo
Mfugaji anachojali mifugo yake tu hafikiri au haoni umuhimu wa hiyo hifadhi hata ikifaa kwake sawa tu

Ova
 
Suala la Ngorongoro ni jambo mtambuka, tusiwalaumu wamasai kama ndio tatizo, tatizo ni serikali.

Wataalamu wa Ikolojia wanasema, tatizo la Ngorongoro sio uwepo wa wamasai ndani ya hifadhi (maana wamekuwepo karne zote) bali tatizo ni kuongezeka kwa shughuli za binadamu zisizohusiana na ikolojia ya Ngorongoro. Kwa mfano
1. Ujenzi wa nyumba za kisasa
2. Kuongezeka kwa wakazi wa kudumu
3. Wingi wa watalii wanaotembelea
4. Uwepo wa magari hifadhini.
5. Ujenzi wa mahoteli

Suluhisho ni nini?
Hifadhi ifungwe kuzuia shughuli zote za utalii na shughuli zote za binadamu zipigwe marufuku (ukiondoa za kitafiti tu).
 
Nchi hii wafugaji wanaonekana Kama wavamizi kila sehemu wakienda wanafukuzwa

Huko ngorogoro hakuna wakulima wanaishi bila tatizo wala migogoro badala yake mnataka muwatoe sijui mnataka kuwapeleka wapi?? huko ambako wataishi bila kuharibu hayo mnayoyaita mazingira yenu.

Waharibifu wakubwa wa mazingira nchi ni wakulima wala sio wafugaji, wakataji wa miti nchi hii ni wakulima sio wafugaji

Badala mpambane na wakulima wanaosababisha jangwa wanaokata miti ovyo ili wapate maeneo ya kulima mnaenda kupambana na wafugaji ambao ni watunzaji wazuri wa mazingira

Shezzy type

Ndiyo maana nimetoa mawazo ya kuwa na mbuga maalumu za wafugaji. Ufugaji wa mpangilio
 
Suluhisho ni nini?
Hifadhi ifungwe kuzuia shughuli zote za utalii na shughuli zote za binadamu zipigwe marufuku (ukiondoa za kitafiti tu).
Hii kali aisee...we mzenji unataka sisi wabara tukose mapato ya utalii....acha roho mbaya.
 
Matatizo yote ktk nchi hii yanaanzishwa na wafugaji
Nchi kubwa hii,wafugaji watafute maeneo mengine waache uvamizi wa maeneo
Mfugaji anachojali mifugo yake tu hafikiri au haoni umuhimu wa hiyo hifadhi hata ikifaa kwake sawa tu

Ova
Juzi nilikuwa shambani kwangu mvomero, akina mama wa kimang'ati watatu na Kijana wa miaka 15 wakaja kuomba maji ya kunywa vijana wangu wakawapa.

Pale nje ya nyumba nimepanda miembe ya muda mfupi mingi, zikaanguka embe mbili chini, aisee nusu wauwane wskigombea hizo embe. Nikawaambia vijana wangu wawaangushie maembe mengi ili wale na kweli walikula mpaka basi.

Nikawa nawauliza hivi wskipelekwa sehemu yao huko mbali na wakulima na kwenye malisho ya kutosha, malambo ya maji na huduma nyingine wataenda?

Nilishangaa sana walipojibu hawaweze kwenda kukaa peke yao huko maporini!! Nikawaambia sasa mna mifugo zaidi ya elfu tatu mtaishije na wakulima bila mgogoro??

Yaani nikabaini kwamba hilo wazo hawalitaki na ndiyo maana hii shida haiishi wakati Tanzania tuna mapori mengi sanaa.
 
Juzi nilikuwa shambani kwangu mvomero, akina mama wa kimang'ati watatu na Kijana wa miaka 15 wakaja kuomba maji ya kunywa vijana wangu wakawapa. Pale nje ya nyumba nimepanda miembe ya muda mfupi mingi, zikaanguka embe mbili chini, aisee nusu wauwane wskigombea hizo embe. Nikawaambia vijana wangu wawaangushie maembe mengi ili wale na kweli walikula mpaka basi. Nikawa nawauliza hivi wskipelekwa sehemu yao huko mbali na wakulima na kwenye malisho ya kutosha, malambo ya maji na huduma nyingine wataenda? Nilishangaa sana walipojibu hawaweze kwenda kukaa peke yao huko maporini!! Nikawaambia sasa mna mifugo zaidi ya elfu tatu mtaishije na wakulima bila mgogoro?? Yaani nikabaini kwamba hilo wazo hawalitaki na ndiyo maana hii shida haiishi wakati Tanzania tuna mapori mengi sanaa.
Siku zote wafugaji wao ndiyo wananzishaga chokochoko hadi kutokea mauaji!

Unakuta mtu ana mifugo mingi kuwalisha mtihani lazima atawaingisha kwenye mashamba,maeneo ya watu hapo ndipo shida inapoanzia

Ova
 
Juzi nilikuwa shambani kwangu mvomero, akina mama wa kimang'ati watatu na Kijana wa miaka 15 wakaja kuomba maji ya kunywa vijana wangu wakawapa. Pale nje ya nyumba nimepanda miembe ya muda mfupi mingi, zikaanguka embe mbili chini, aisee nusu wauwane wskigombea hizo embe. Nikawaambia vijana wangu wawaangushie maembe mengi ili wale na kweli walikula mpaka basi. Nikawa nawauliza hivi wskipelekwa sehemu yao huko mbali na wakulima na kwenye malisho ya kutosha, malambo ya maji na huduma nyingine wataenda? Nilishangaa sana walipojibu hawaweze kwenda kukaa peke yao huko maporini!! Nikawaambia sasa mna mifugo zaidi ya elfu tatu mtaishije na wakulima bila mgogoro?? Yaani nikabaini kwamba hilo wazo hawalitaki na ndiyo maana hii shida haiishi wakati Tanzania tuna mapori mengi sanaa.
Nakumbuka yale machafuko yaliyotokea kilosa
Wakulima na wafugaji nlikuwa kule...watu waliuana saana kitu ambacho siyo nahadisiwa
Nlishuhudiaaa kwa macho
Ndomana nasema wafugaji wajipange vizuri na mifugo yao,wakae na serikali waone namna gani
Itawapatia maeneo

Ova
 
Juzi nilikuwa shambani kwangu mvomero, akina mama wa kimang'ati watatu na Kijana wa miaka 15 wakaja kuomba maji ya kunywa vijana wangu wakawapa. Pale nje ya nyumba nimepanda miembe ya muda mfupi mingi, zikaanguka embe mbili chini, aisee nusu wauwane wskigombea hizo embe. Nikawaambia vijana wangu wawaangushie maembe mengi ili wale na kweli walikula mpaka basi. Nikawa nawauliza hivi wskipelekwa sehemu yao huko mbali na wakulima na kwenye malisho ya kutosha, malambo ya maji na huduma nyingine wataenda? Nilishangaa sana walipojibu hawaweze kwenda kukaa peke yao huko maporini!! Nikawaambia sasa mna mifugo zaidi ya elfu tatu mtaishije na wakulima bila mgogoro?? Yaani nikabaini kwamba hilo wazo hawalitaki na ndiyo maana hii shida haiishi wakati Tanzania tuna mapori mengi sanaa.
Akili zao ni Kama mifugo yao
 
Kwa nini Watanzania mna imani serikali inaweza kutatua migogoro yote ya ardhi? Nyerere aliwadanganya mkaamini inawezekana. Serikali ya Marekani imeshindwa, serikali ya Australia imeshindwa, serikali ya Israel imeshindwa, serikali za Latin America zimeshindwa, migogoro haiishi, kesi mahakamani haziishi.

Serikali ina chaguzi mbili, kutumia nguvu ya dola (might is right) kuwahamisha watu kwa nguvu liwalo na liwe au kuwalipa watu kama fidia wakihama kwa hiari yao. Lakini pia hili siyo suluhisho maana wanaohamishwa kwa nguvu wanaweza kuingia kwenye ujangili na watoto na wajuukuu wa wanaolipwa fidia kuhama wanaweza kurudi kudai tena ardhi yao.
 
Nawashauri Serikali wakiweka Siasa kwenye swala hili la Ngorongoro hii mbuga baada ya miaka itakuwa tatizo. Kuwahamisha wamassai kule ni lazima kama wana nia njema. Waziri mkuu ameweka siasa zaidi. Tunaongelea watu pekee wakati tatizo kubwa ni mifugo karibu 1M. Waandishi wa habari wametenda haki kwenye hili🙏

Ndugu zetu Wamassai na Wamang'ati wamekuwa na ufugaji kiholela karibu Tanzania nzima. Kwa ufupi hawa wafugaji wanaishi kwa utaratibu wao wenyewe bila kufuata sheria yeyote. Lakini kibaya zaidi wanaharibu mazingira sana na ni lazima kuwekwe utaratibu. Huko Arusha ndiyo kabisa kumekuwa kama jagwa na sasa wameingia Ngongogoro.

Ushauri wangu ni kwa serikali kuanzisha mbuga maalumu za wafugaji. Mbuga hizi ziwe na wataalamu wa mazingira, lakini wawekewe huduma muhimu kama Watanzania wengine. Mbuga hizi za wafugaji ziwe kila pande kuu za nchi . Kwa mtazamo wangu mbuga kuu kumi zinatosha. Huko ndani watengenezewe mabwawa, kuwe na utaratibu wa mupanda miti na majani ya chakula cha mifugo. Kitu kizuri kimoja ni kwamba mchango wa kuingia huko au kodi ni hiyo hiyo mifugo. Hivyo wafugaji ni lazima wachangie mifugo kama kodi ili waweze kuwekewa huduma za mbuga na uwekezaji. Kwa ufupi serikali iwasaidie wawe na ushirika wa wafugaji ndani ya hizi mbuga maalumu. Serikali itafaidika kwa mambo yafuatayo

1. Itasaidia kulinda mazingira
2. Itasaidia wafugaji kuweza kuuza mifugo yao kwa utaratibu
3. Itapunguza migongano ya wakulima na wafugaji
4. Itasaidia kuwatambua na kuwapa vibali wafugaji
5. Itasaidia wafigaji kupata huduma kama za Afya na Elimu
6. Itasaidia serikali kupata kodi

Bila hizi tutakuwa na matatizo. Ngombe wao hawana afya nzuri, pesa hawana na wanakaa na ngombe mpaka wafe. Lakini kwa hali ya hewa inavyoendelea tutakuwa na migogoro zaidi.

Nimesikia serikali inataka kuwahamishia Handeni je kuna utaratibu gani wa kuhakikisha Handeni haiwi jagwa?
Je serikali imeweka wataalamu wa mazingira na kilimo?
Je migogoro ya wakulima wengi wa mahindi na wafugaji utaratibu gani serikali imeweka kukabili?

Nimesikia serikali inataka kuwahamishia Handeni je kuna utaratibu gani wa kuhakikisha Handeni haiwi jagwa?
Je serikali imeweka wataalamu wa mazingira na kilimo?
Je migogoro ya wakulima wengi wa mahindi na wafugaji utaratibu gani serikali imeweka kukabili?
 
Nawashauri Serikali wakiweka Siasa kwenye swala hili la Ngorongoro hii mbuga baada ya miaka itakuwa tatizo. Kuwahamisha wamassai kule ni lazima kama wana nia njema. Waziri mkuu ameweka siasa zaidi. Tunaongelea watu pekee wakati tatizo kubwa ni mifugo karibu 1M. Waandishi wa habari wametenda haki kwenye hili🙏

Ndugu zetu Wamassai na Wamang'ati wamekuwa na ufugaji kiholela karibu Tanzania nzima. Kwa ufupi hawa wafugaji wanaishi kwa utaratibu wao wenyewe bila kufuata sheria yeyote. Lakini kibaya zaidi wanaharibu mazingira sana na ni lazima kuwekwe utaratibu. Huko Arusha ndiyo kabisa kumekuwa kama jagwa na sasa wameingia Ngongogoro.

Ushauri wangu ni kwa serikali kuanzisha mbuga maalumu za wafugaji. Mbuga hizi ziwe na wataalamu wa mazingira, lakini wawekewe huduma muhimu kama Watanzania wengine. Mbuga hizi za wafugaji ziwe kila pande kuu za nchi . Kwa mtazamo wangu mbuga kuu kumi zinatosha. Huko ndani watengenezewe mabwawa, kuwe na utaratibu wa mupanda miti na majani ya chakula cha mifugo. Kitu kizuri kimoja ni kwamba mchango wa kuingia huko au kodi ni hiyo hiyo mifugo. Hivyo wafugaji ni lazima wachangie mifugo kama kodi ili waweze kuwekewa huduma za mbuga na uwekezaji. Kwa ufupi serikali iwasaidie wawe na ushirika wa wafugaji ndani ya hizi mbuga maalumu. Serikali itafaidika kwa mambo yafuatayo

1. Itasaidia kulinda mazingira
2. Itasaidia wafugaji kuweza kuuza mifugo yao kwa utaratibu
3. Itapunguza migongano ya wakulima na wafugaji
4. Itasaidia kuwatambua na kuwapa vibali wafugaji
5. Itasaidia wafigaji kupata huduma kama za Afya na Elimu
6. Itasaidia serikali kupata kodi

Bila hizi tutakuwa na matatizo. Ngombe wao hawana afya nzuri, pesa hawana na wanakaa na ngombe mpaka wafe. Lakini kwa hali ya hewa inavyoendelea tutakuwa na migogoro zaidi.

Nimesikia serikali inataka kuwahamishia Handeni je kuna utaratibu gani wa kuhakikisha Handeni haiwi jagwa?
Je serikali imeweka wataalamu wa mazingira na kilimo?
Je migogoro ya wakulima wengi wa mahindi na wafugaji utaratibu gani serikali imeweka kukabili?

Serikali iweke wazi ngorongoro lazima watu waondolewe
 
Back
Top Bottom