Serikali kwanini isitoe elimu kwa Watanzania wote kabla ya kuingia kwenye hii Mikataba?

rodgers123

Senior Member
Jul 12, 2015
159
125
Jamani nina swali ambalo nadhani hata wabunge wetu wangejiuliza kabla ya kupitisha hili jambo.

Na wasiangalie wao wanaishi sasa waangalie na watoto na wajukuu wajao wataishi vipi huko baadae.
Maswali:

(1) Kama kila siku tunaambiwa tunategemea sana mapato ya bandari. Sasa kama bandari inapigwa mnada kwa wawekezaji. Je muwekezaji akisema mpaka arudishe pesa zake ndio serikali ianze kupata mapato , Itakuwaje..?

Naona kama waarabu watakuwa na influence kubwa kwenye serikali ya Tanzania kwenye miaka ijayo kwenye maswala ya pesa. Ama mnaonaje..?

(2) Naona kama kodi za mtaani zitaongezeka na hii itafanya maisha kuwa magumu zaidi..?
Kama muwekezaji akisema anataka arudishe pesa zake kwanza na serikali yetu itabidi itafute njia mbadala wa mapato. Tozooo zitakuja mpya ama..?

(3)Je ni kwanini serikali isianze ku raise pesa kutoka kwa watanzania kwanza.
Mfano kutangaza hisa(bond) ambazo watanzania kwa pamoja wangenunua ili nao wawe na hisa za bandari pamoja na huyu muarabu kuliko kumuachia muarabu na TPA kuweka
pesa kidogo..?

Kwani nina uhakika watu raia wa kiarabu wana hisa kwenye hii DP kampuni. Hivyo wataendelea kutajirika kupitia bandari zetu.Na watanzania mmoja mmoja asipate faida zaidi ya kulipa kodi akiingiza magari au mizigo.

(4)Serikali kwa nini isitoe elimu kwa watanzania wote kabla ya kuingia kwenye hizi deal.

Ili watanzania kwa ujumla wajue faida na hasara watakayoipata.
Maana tumeona kipindi cha nyuma mikataba inaingiwa alafu akija raisi mwingine anaisitisha na kusema tumepigwa.

Na hawa hawa wanaoipitisha sasa wanakuja kuunga mkono na kusema tumepigwa kweli.

(5)Je kama marejesho ya pesa kwa muarabu yasipotimia kwa wakati. Tumeweka rehani nini..? Tumeweka rehani mbuga zetu ?, madini .?, Mlima Kilimanjaro..?Watanzania..?
Inabidi watanzania waambiwe na kijiandaa kisaikolojia..

(6) Kwa nini hawa wanaojiita wapinzani wasionyeshe msimamo wao kwenye hili jambo kama halina manufaa ya kitaifa sasa kuliko kusubiri kipindi cha kampeni na kuwa ajenda yao ya kutuambia.

Majanga yaliyoipata Sri-lanka na bandari yake kwa kuchukua pesa za Mchina. Sri Lanka, Struggling With Debt, Hands a Major Port to China


On 20 May, the Sri Lankan parliament passed the Colombo Port City
Economic Commission Bill that lays out the country’s legal framework
governing the China-financed project built on land reclaimed from the
Sri Lankan capital’s seafront, adjoining Colombo’s port.
The bill effectively turns these 660 acres into Chinese sovereign territory.

Ni maswali tuu waliyonijia. Mwenye ufafanuzi naomba anisaidie kujua zaidi.
 
Back
Top Bottom