DP world atatoa 35% ya hisa kwa Watanzania, hii maana yake nini?

Alejandroz

JF-Expert Member
Feb 14, 2017
327
376
Hellow great thinkers

Tumeskia kwamba endapo kampuni ya DPW ikiwekeza katika bandari yetu (zetu) itatoa 35% ya hisa zake kwa watanzania ili nao wawe sehemu ya kampuni

Naomba kueleweshwa jinsi ambavyo serikali huwa inanufaika kupitia wawekezaji wanaokuja kuwekeza katika nchi

Je huwa inanufaika kwakupitia hisa inazomiliki kwenye kampuni husika iliyokuja kuwekeza (mgawanyo wa faida) pekee,, au kwakupitia kodi inayokusanywa na TRA pekee au vyote kwa pamoja?

Maana nimewaza kama ikitokea hizi 35% za hisa zikamilikiwa na watanzania (binafsi) yenyewe serikali inaenda kunufaikaje na uwekezaji huu bila kumiliki hata hisa moja?

Karibu unielimishe

Angalizo:
Naomba tusijikite zaidi kuzungumzia suala la Dp world na bandari badala yake tujikite kwenye swali
 
Uhuniuhuni tu,waweke 50 KWA 50 na sheria za nchi- zifuatwe kama wawekezaji wengine na ukomo uwepo,wasijekuja kudahi uhuru wao
 
Yaani ninakukaribisha kwangu na familia yangu, unanikuta nina vyakula vyote ghalani na vyombo vyote vya kupikia kasoro mpishi tu ndio sina
Unanijia na masharti ya kuchukua nusu na theluthi ya chakula utakachopika kisa tu mpishi umemleta wewe
 
Viongozi wetu wanalaana,sio bure
 
Back
Top Bottom